Hizi ndizo Sheria saba (7) Mpya za Kombe la Dunia

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,414
Reaction score
15,452
Miongoni mwa mabadiliko makubwa yatakayotumika katika Kombe la Dunia la 2026 ni:

1. sheria ya kuhesabu sekunde tano kwa mipira ya kurushwa. Ikiwa mchezaji atachelewesha kwa makusudi kuurudisha mpira mchezoni baada ya muda huo kuisha, mwamuzi anaweza kuipa timu pinzani haki ya kurusha mpira huo.

Sheria kama hiyo itatumika pia kwenye mipira ya golikiki (Sekunde tano kwa mpira wa golikiki). Endapo timu itajaribu kupoteza muda kwa kuchelewesha kuanza tena mchezo, mwamuzi anaweza kuipa timu pinzani kona kama adhabu. Lengo ni kupunguza tabia ya kupoteza muda hasa katika dakika za mwisho za mechi.

2. Mabadiliko mengine yanahusu mabadiliko ya wachezaji. Mchezaji anayefanyiwa mabadiliko (sub), atakuwa na sekunde 10 tu kufika nje kupitia njia ya karibu zaidi.
Akichelewesha zaidi ya muda huo, mchezaji mbadala hataruhusiwa kuingia mara moja na timu italazimika kucheza ikiwa pungufu kwa muda dakika moja.

3. Kwa upande wa matibabu ya majeruhi, mchezaji anayepatiwa huduma ya kitabibu atalazimika kubaki nje ya uwanja kwa sekunde 60 kabla ya kuruhusiwa kurejea kucheza, isipokuwa katika mazingira maalumu kama majeraha ya kipa au pale ambapo mpinzani amepewa kadi ya njano au nyekundu.

4. Kufunika mdomo huku ukizungumza:

Aidha, mchezaji atakayefunika mdomo wake kwa mkono, jezi au njia nyingine wakati wa kuzungumza au kubishana na mpinzani anaweza kuadhibiwa kwa kadi nyekundu, hatua inayolenga kuongeza uwazi na kuzuia tabia zinazoweza kuficha mawasiliano ya wachezaji, hasa matusi na ubaguzi wa rangi.

5. VAR pia imepewa mamlaka mapya. Waamuzi wa video sasa wataweza kuchunguza kama kona au mpira wa adhabu umetolewa kwa usahihi kabla ya mchezo kuendelea, na pia wataweza kupitia uamuzi wa kadi ya pili ya njano uliosababisha mchezaji kutolewa uwanjani. Hata hivyo, kadi za njano za kawaida hazitaangaliwa na VAR.

6 Teknolojia ya usaidizi wa Video (VAR) katika mipira ya adhabu na kona. Hapo awali, matukio ya faulo yaliyotokea kabla ya mpira kuchezwa rasmi hayakuweza kuchunguzwa na VAR, jambo lililozua malalamiko.

Kwa sasa, IFAB imekubali mabadiliko yanayoruhusu VAR kuchunguza makosa yanayotokea kabla ya mpira kuchezwa, ikiwa tukio hilo linaathiri moja kwa moja matokeo ya mchezo kama bao, penalti au adhabu ya kinidhamu.

Hii ina maana kuwa iwapo itabainika kulikuwa na faulo kabla ya kona au mpira wa adhabu kupigwa, mwamuzi anaweza kuamuru mpira urudiwe tena.

7 Wakati golikipa au mchezaji anaanguka na matibabu yanaendelea, wachezaji hawataruhusiwa kwenda kwenye benchi la ufundi kupata maelekezo ya kocha.
Badala yake watabaki uwanjani au kukusanyika katikati ya uwanja. Waamuzi watazuia timu kutumia kusimama kwa mchezo kama “timeout” ya kupata maelekezo ya kiufundi

FIFA inasema mabadiliko haya yote yanalenga kufanya Kombe la Dunia la 2026 kuwa la haki zaidi, la kasi zaidi na lenye kupunguza malalamiko kuhusu maamuzi ya waamuzi, huku likihakikisha soka linabaki kuwa mchezo wa ushindani na burudani duniani.

Kwa ufupi
FIFA imethibitisha rasmi baadhi ya mabadiliko ya sheria yatakayotumika katika Kombe la Dunia 2026:

Muda wa kurusha mpira wa pembeni (sekunde 5)
Mchezaji anatakiwa kurusha mpira ndani ya sekunde tano. Akichelewesha kwa makusudi, timu pinzani inaweza kupewa mpira huo.

Muda wa kupiga goli kiki (sekunde 5)
Sheria hii inalenga kupunguza upotevu wa muda. Timu ikichelewesha kwa makusudi, mpira unaweza kutolewa kuwa kona kwa wapinzani.

Mabadiliko ya wachezaji (sekunde 10)
Mchezaji anayetolewa anatakiwa kutoka uwanjani ndani ya sekunde 10 kupitia eneo la karibu zaidi. Asipofanya hivyo, mchezaji wa akiba hataruhusiwa kuingia kwa angalau dakika moja na timu italazimika kucheza ikiwa na wachezaji 10.

Matibabu nje ya uwanja (sekunde 60)
Mchezaji anayepatiwa matibabu atatakiwa kubaki nje ya uwanja kwa sekunde 60 kabla ya kurejea. Walinda mlango, majeraha maalumu au matukio yanayosababisha mpinzani kupewa kadi havitahusika na sheria hii.

Kufunika mdomo wakati wa mabishano
Mchezaji anayefunika mdomo kwa makusudi wakati wa mabishano na mpinzani anaweza kupewa kadi nyekundu.

VAR kukagua maamuzi ya kona
Teknolojia ya VAR inaweza kutumika kuthibitisha kama kona ilitolewa kwa usahihi, mradi ukaguzi ufanyike haraka kabla mchezo haujaanza tena.

Ukaguzi wa kadi ya pili ya njano
Kadi ya pili ya njano inayosababisha mchezaji kutolewa nje inaweza kukaguliwa, lakini VAR haitatumika kuangalia matukio yanayoweza kupelekea kutolewa kwa kadi ya pili ya njano.
 
Miongoni mwa mabadiliko makubwa yatakayotumika katika Kombe la Dunia la 2026 ni:

1. sheria ya kuhesabu sekunde tano kwa mipira ya kurushwa. Ikiwa mchezaji atachelewesha kwa makusudi kuurudisha mpira mchezoni baada ya muda huo kuisha, mwamuzi anaweza kuipa timu pinzani haki ya kurusha mpira huo.

Sheria kama hiyo itatumika pia kwenye mipira ya golikiki (Sekunde tano kwa mpira wa golikiki). Endapo timu itajaribu kupoteza muda kwa kuchelewesha kuanza tena mchezo, mwamuzi anaweza kuipa timu pinzani kona kama adhabu. Lengo ni kupunguza tabia ya kupoteza muda hasa katika dakika za mwisho za mechi.

2. Mabadiliko mengine yanahusu mabadiliko ya wachezaji. Mchezaji anayefanyiwa mabadiliko (sub), atakuwa na sekunde 10 tu kufika nje kupitia njia ya karibu zaidi.
Akichelewesha zaidi ya muda huo, mchezaji mbadala hataruhusiwa kuingia mara moja na timu italazimika kucheza ikiwa pungufu kwa muda dakika moja.

3. Kwa upande wa matibabu ya majeruhi, mchezaji anayepatiwa huduma ya kitabibu atalazimika kubaki nje ya uwanja kwa sekunde 60 kabla ya kuruhusiwa kurejea kucheza, isipokuwa katika mazingira maalumu kama majeraha ya kipa au pale ambapo mpinzani amepewa kadi ya njano au nyekundu.

4. Kufunika mdomo huku ukizungumza:

Aidha, mchezaji atakayefunika mdomo wake kwa mkono, jezi au njia nyingine wakati wa kuzungumza au kubishana na mpinzani anaweza kuadhibiwa kwa kadi nyekundu, hatua inayolenga kuongeza uwazi na kuzuia tabia zinazoweza kuficha mawasiliano ya wachezaji, hasa matusi na ubaguzi wa rangi.

5. VAR pia imepewa mamlaka mapya. Waamuzi wa video sasa wataweza kuchunguza kama kona au mpira wa adhabu umetolewa kwa usahihi kabla ya mchezo kuendelea, na pia wataweza kupitia uamuzi wa kadi ya pili ya njano uliosababisha mchezaji kutolewa uwanjani. Hata hivyo, kadi za njano za kawaida hazitaangaliwa na VAR.
6 Teknolojia ya usaidizi wa Video (VAR) katika mipira ya adhabu na kona. Hapo awali, matukio ya faulo yaliyotokea kabla ya mpira kuchezwa rasmi hayakuweza kuchunguzwa na VAR, jambo lililozua malalamiko.

Kwa sasa, IFAB imekubali mabadiliko yanayoruhusu VAR kuchunguza makosa yanayotokea kabla ya mpira kuchezwa, ikiwa tukio hilo linaathiri moja kwa moja matokeo ya mchezo kama bao, penalti au adhabu ya kinidhamu.

Hii ina maana kuwa iwapo itabainika kulikuwa na faulo kabla ya kona au mpira wa adhabu kupigwa, mwamuzi anaweza kuamuru mpira urudiwe tena.

FIFA inasema mabadiliko haya yote yanalenga kufanya Kombe la Dunia la 2026 kuwa la haki zaidi, la kasi zaidi na lenye kupunguza malalamiko kuhusu maamuzi ya waamuzi, huku likihakikisha soka linabaki kuwa mchezo wa ushindani na burudani duniani.
Games zitakuwa za speed
 
Izi sheria zinapaswa zije kutumia kwenye games na warabu africa

Kuna watu wanawaonea wivu waarabu, semeni tu ukweli waarabu wanalijua soka....na morocco 🇲🇦 anaenda kuwashangaza.....senegal anatoka mapema.

Argentina 🇦🇷 💪🏽
Morocco 🇲🇦 💪🏽
Spain 🇪🇸 💪🏽
 
Back
Top Bottom