Naomba kujua, mali za Hermanus Stayn zilizotaifishwa 1983, ziko wapi au nani anazimiliki leo hii?

Kwa mawazo yangu.....ndege zitakuwa zilishatoweka kwa sababu ya kukosa usimamilizi na matunzo. Mashamba huenda yalikuwa chini ya umiliki wa serikali (kipindi cha Nyerere; kama ilivyokuwa kwa mashamba mengine yote yaliyotaifishwa) na baada ya ubinafsishaji kugonga hodi, yakachukuliwa na wajanja wachache.
Nataka kujua hao wajanja waliomilikishwa hizo mali za Hermanus Stayn, hata kama zimebaki screpa, tuonyeshwe screpa ziko wapi, kama waliuza pesa ziko wapi? Wao ndio wamlipe hilo salio, sisi watupe ndege yetu kabla hatujakasirika...!!!
 
Back
Top Bottom