Naomba kujua kuhusu kufunga ndoa kanisani.

Naomba kujua kuhusu kufunga ndoa kanisani.

tendo la ndoa navyojua ni kukutana kimwili kwa watu walio oana.

Kwahiyo Kama ndoa ni kukutana kimwili kanisani mnaenda kukutania?

Au mnaenda kufunga kukutana kimwili?
Kwani ndoa na kuoana kipi kinaanza?

Mm nafikiri kanisani mnaenda kuhalalisha kujamiiana na kufanya matangazo kwa watu wawajue.
 
Ninavyojua Biblia inasema kijana atawaacha wazazi wake na ataambatana na mkewe nao watakua mwili mmoja,je ni wapi Biblia inasema lazma ukafunge ndoa kanisani?je km mm nimependana na bint,tumekubaliana na tunaishi pamoja kwa upendo na amani bila kufunga ndoa kuna dhambi yoyote hapo?mi naomba kujua ni wap biblia inataka tukafunge ndoa kanisani?msing wa hyo dhana unatoka wap?naomba nielimishwe.

Mkuu naona watu wanakurushia tuhuma na mameno mengi lakini swali lako ni la msingi na nna amini hata baadhi ya wakristo wengi hawana jibu licha ya kutaka lipuuzwe.

Sina mstari wa moja kwa moja unaohusu sherehe ya harusi au jinsi gani ifanyike licha ya ukweli kwamba Biblia imejaa mistari inayoelezea umuhimu wa ndoa tangu mwanzo.

Inategemea unaongelea dhehebu gani, kwa sababu licha ya kwamba ndoa inafungwa kanisani lakini kile cheti kinatoka serikalini.
Na kuna taratibu zake kama vile tangazo litoke siku ngapi kabla ya siku ya harusi.

Kwa ufupi niseme, kila dhehebu wamekuja na utaratibu wao (Mapokeo) ya jinsi wanavyotaka waumini wao waishi kutokana na misingi ya hilo dhehebu. Ndio maana kuna wengine wanabatiza kwa maji mengi, wengine wanabatiza watoto, wengine wanaabudu siku ya Jumapili na wengine siku ya Jumamosi n.k

Kama wewe ni mkristo na uko kwenye mojawapo ya makanisa ya kikristo, ni lazima ukubaliane na utaratibu waliojiwekea.
 
Ndugu,Mungu alipotuumba ametupa binadamu Hekima,wanyama wengine wote hawana,ametupa ujuzi na maharifa,mbona umeuliza kuhusu kufunga ndoa kanisani lakini hujauliza kwanini Unatakiwa utangaze ndoa yako wiki 3? Utaratibu uliowekwa na wanadamu kwa ufunuo wa hekima ya Mungu na jambo ambalo linampa Mungu utukufu sioni kama ni dhambi,kabla ya kuuliza swali hebu jaribu kujijibu,kufunga ndoa uchochoroni na kanisani which is best? Au kuna dhambi unaiona pale unapifunga ndoa kanisani? Yesu alisema ya Mungu mpe Mungu na ya Kaisari mpe kaisari,alimaanisha kuna taratibu za kidunia ambazo ni njema unatakiwa utii.
 
Unajua kua biblia imekataza uzinzi na uasherati

Ukitafakari hilo utapata jibu la swali lako
 
Wewe ni mkristu kweli maana sikutegemea ungeuliza swali kama hilo. Hata kama kwenye biblia haijaandikwa lakini ndoa ni sakramenti kama ilivyo ubatizo, upadri, ekaristi n.k na hivyo kuna utaratibu wa utoaji wa sakramenti yoyote ile. Kuchukuana na kuanza kuishi siyo ndoa bali unataka kuhalalisha uasherati na kwa amri za Mungu unavunja amri ya sita.

Jibu limetulia kama ya kwenye mtungi..
 
Mkuu naona watu wanakurushia tuhuma na mameno mengi lakini swali lako ni la msingi na nna amini hata baadhi ya wakristo wengi hawana jibu licha ya kutaka lipuuzwe.

Sina mstari wa moja kwa moja unaohusu sherehe ya harusi au jinsi gani ifanyike licha ya ukweli kwamba Biblia imejaa mistari inayoelezea umuhimu wa ndoa tangu mwanzo.

Inategemea unaongelea dhehebu gani, kwa sababu licha ya kwamba ndoa inafungwa kanisani lakini kile cheti kinatoka serikalini.
Na kuna taratibu zake kama vile tangazo litoke siku ngapi kabla ya siku ya harusi.

Kwa ufupi niseme, kila dhehebu wamekuja na utaratibu wao (Mapokeo) ya jinsi wanavyotaka waumini wao waishi kutokana na misingi ya hilo dhehebu. Ndio maana kuna wengine wanabatiza kwa maji mengi, wengine wanabatiza watoto, wengine wanaabudu siku ya Jumapili na wengine siku ya Jumamosi n.k

Kama wewe ni mkristo na uko kwenye mojawapo ya makanisa ya kikristo, ni lazima ukubaliane na utaratibu waliojiwekea.

bora ww umejibu
wengine wanazunguka tu
cc Eiyer
com zis way
 
^^
Sidhani kama kuna neno lenye maelekezo hayo lililo moja kwa moja.
Nachofahamu ni kuwa huo ni utaratibu wa mahali husika kama njia ya kupata uhalali wa mahusiano yatakayotambulika na jamii nzima.
Hata hivyo ukiona hilo la nyumba za ibaada zinakunyima uhuru, zipo njia nyingine mfano ndoa za kimila, ndoa za serikalini..
Kupendana haitoshi ila kuhalalisha inapendeza
^^
 
Himidin,Samaritani,hongeren sana na wachangiaji wengne walionipa majib mazuri.nimepata wazo zuri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom