Naomba kujua kuhusu dawa ya Alkasusu

Naomba kujua kuhusu dawa ya Alkasusu

Nikipita na gari naona baadhi ya Maustadh au vijana wenye mlengo wa dini ya kiislam (nasema kiislam maana wamevaa kanzu na kujifunga vilemba kichwani) wakiwa na chupa za chai (themosi) na vijikombe vya plastic (take away) mkononi wanazunguka zunguka sehemu zenye watu wanauza.

Kwa kiasi kikubwa naona watu wanakunywa sana wamekaa na kujipanga kabisa kwenye mabenchi,
Hivi ni dawa au ni kiburudisho tuu kama kahawa au tangawizi?

Nimekosa wa kumuuliza maana nakuwa hai hai sana wakati huo naomba kujuzwa inasaidia nini.
 
Ukiona hivyo ujue wamesema inaongeza nguvu za kiume. Ukitaka uwapate wanaume wa dar waambie kitu X kinaongeza nguvu za kiume.
 
Tanzania kila mtu ni daktari anajua kuttibu, kila kitu ni dawa.

Tanzania ina madaktari wengi kuliko wagonjwa.

Hiyo utaambiwa ni dawa ya nguvu za kiume. Sasa hivi hata ukianza kuuza mavi ukasema yanatibu kitu flani lazzima watu watayala na kuamini.

Kwenye nguvu za kiume tulianza na mayai ya kware, tukaja mayai ya kenge, nazi mbichi, karanga, mihogo mibichi kama ngiri, pweza, sasa ni vumbi la kongo, nadhani kinachofuata sasa ni mavi tu.
 
Bwana guDume, mbona muongo hivo? Umeshaonekana sana unabugia al kasus.
Ina maana unakunywa kwa ajili ya ukuaji tu wa mwili?
Huwa sipend kutumia kinywaji au chakula chochote kinachosemwa kuongeza nguvu za kiume. Navichukia vitu hivi kiukweli. Ukiishi maisha mazuri inakutosha kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi jaribu VUMBI LA CONGO, sitolirudia tena, he hadi panakucha alisikika mlevi akilalamika.
 
Hicho ni kinywaji Kama vinywaji vingine.acheni kujiaminisha ujinga eti "ni mbadala wa vumbi la Kongo,& nk". An-kasus anakunywa yeyote either ni wa kiume au wa kike kwa rika zote.suala la kusema inaboost nguvu Fulani wakat wa tendo fulani its NONSENSE...cha kuzingatia ni kwamba ni kinywaji cha kipekee chenye ladha maridhawa iliyotokana na mchanganyiko wa viungo tofauti.
 
Wakuu kuna hii biashara iliyoibuka kwa kasi ya kuuza ALKASUS huku wauzaji wakiwa na majigambo yake akielezea kuhusu ufanisi wake na matunda yake mala baada ya matumizi.

Kwa wenye uzoefu naomba kujua ukweli wake na matokeo yake maana hapa nilipo sijawahi iweka mdomoni hata siku moja. Kabla sijawa mdau naomba kupata ukwel juu ya huduma hio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukila chakula bora ukashiba vizuri na afya yako ikiwa bora huna maradhi,mazoezi ya viungo,kunywa maji ya kutosha haina aja ya kufata mkumbo wa milipuko ya dawa za nguvu za kiume zinazoibuka kila siku.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Sio Dawa. Ni Kinywaji kama Chai, kinachoongezwa Viungo Kadhalika ili kuongeza utamu....!
Kuna dawa inapikwa na kuuzwa sehemu mbalimbali wanaiita alkasusu naomba kuuliza hizo dawa asili yake ni wapi na ni kweli zinatibu naomba mwenye uelewa wa hii dawa anijulishe.
===
 
Habari za jioni wakuu?

Kuna baadhi ya waheshimiwa humu Jf wanaodai kuwa Alkasus si kinywaji salama ni hatari kwa afya za wanywaji. Mimi ni mtumiaji wa kinywaji hicho cha Alkasus nakipenda na kwakweli kinanifalia sana ila sijajua ni kwajinsi gani kinamadhara.

kwahiyo nawaomba wale ambao wanaufahamu juu ya madhara ya utumiaji wa Alkasus watujuze kwa undani jinsi gani kinywaji hicho husababisha madhara na itakuwa vizuri zaidi mkitufahamisha pamoja na vitu vinavyotumika kuandaa (kutengeneza)kinywaji chenyewe, kusema tu kibaya hakifai au kukikashifu haitusaidii sisi watumiaji kuamini,

kwa uchambuzi wa kina juu ya kinywaji hicho mtakua mmetusaidia kukijua kwa undani na hivyo kukiepuka na kujinusuru na matatizo(maradhi)ambayo yanaweza kutuathiri siku za mbeleni. Asanteni, natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom