Naomba kujua kuhusu dawa ya Alkasusu

Naomba kujua kuhusu dawa ya Alkasusu

Beatus david

Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
27
Reaction score
9
Kuna dawa inapikwa na kuuzwa sehemu mbalimbali wanaiita alkasusu naomba kuuliza hizo dawa asili yake ni wapi na ni kweli zinatibu naomba mwenye uelewa wa hii dawa anijulishe.
===
Amani iwe kwenu waungwana, pamoja na wafungwa waliosamehewa karibuni uraiani, japo kuna yule mmoja hataki kabisa nadhani kuna kitu hajajua.

Kukaa gerezani kwa takribani miaka 20 ni mengi yameendelea huku duniani ikiwa ni pamoja na mabadiliko na gunduzi mbalimbali, katika hili tujipongeze sote, kwa kuanza ni hawa wakazi wa Dasilamu.

Basi bwana ikawa jioni moja nimekaa kwenye kituo cha daladala nikitafakari namna ya kufika kambini baada ya pilika za hapa na pale, jamaa mmoja alisogea na kukaa karibu yangu huku mkononi ameshikilia ‘chupa za chai’ almaarufu ‘thermos’ kama nne au tano hivi; kuna harufu fulani nzuri ilinijia puani na kunitambulisha kuwa kuna maziwa ndani ya chupa hizo.

Ili kuanzisha stori nikaamua tu kumuuliza jamaa kama anauza chupa hizo, naye bila kusita akajibu kuwa anauza ‘alkasusu’ sio chupa. Nilikuwa nimewahi kusikia hii kitu hivyo nikapata shauku kutaka kuijua vema.

Nikaomba kujua ni nini hasa, akanitajia na vitu vinavyochanganywa kuwa ni pamoja na maziwa, hiliki, tangawizi, mdarasini, karafuu na vingine kadhaa nimesahau nikajikuta natamani kupata huduma hii ila nahisi nilimkera kwa maswali akaona kejeli akarukia daladala huyo akatokomea.

Sasa basi, nimeleta kwenu ili tupeane uzoefu kuhusu faida na changamoto zake kwa maana hii kitu inasifika kuwa ni ‘booster’ moja matata kwenye mambo yetu kwa kuzingatia kuwa mchanganyiko wake ni vyakula halisi hivyo usalama kiafya ni uhakika.

Hebu tupeane elimu pamoja na mrejesho kwa waliofanikiwa kuitumia, na kama kweli inafaa basi tufundishane namna ya kuandaa nyumbani hapa lengo sio kuua biashara ya watu. Najuta kumkera jamaa muuzaji huenda ningeleta shule humu na mrejesho.

NB: Wale mabingwa wa kupiga ‘show za kibabe’ hamtopungukiwa kitu mkichangia hapa, na sio kwamba tunachangia basi tuna upungufu, ni elimu tu na pongezi kwa ugunduzi.

Karibuni wakuu, alkasusu.
 
Wagaga njoo swali lenu hili, sisi wauguzi si daraja letu.
 
Wakuu sahau kuhusu kahawa hii ALKASUS ni Moto wa kuotea mbali mchuzi wa pweza uende shule.
 
Huwa sipend kutumia kinywaji au chakula chochote kinachosemwa kuongeza nguvu za kiume. Navichukia vitu hivi kiukweli. Ukiishi maisha mazuri inakutosha kabisa.
Lakin hivi ni vyakula asilia tu mkuu
 
Ukizoea hivyo vitu vina athari kisaikolojia.hata ukiamini tu kuwa maji yanakuongezea nguvu za kiume.ukija kosa maji unaweza shindwa piga game.unajua sex ina involve psychology pia.nfdo maana binafsi sitaki kuhusisha na chochote ili wakat wowote ikitakiwa kucheza game nacheza bila ku boost

Vipi kuhusu kupiga K-Vant kabla ya game?
 
Back
Top Bottom