Naomba kujitambulisha kisiasa kwenu wenyeji

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Napenda kuwafahamisha kwamba leo nimejiunga rasmi na JamiiForums baada ya kuwa muumini wa kusoma na kufuatilia nyuzi humu hasa za siasa kwa muda mrefu sasa. Naomba mnipokee. Naamini mmekubali kunipokea. Kabla ya kuanzisha uzi wowote ule ama kuchangia uzi uliokwisha anzishwa naomba niweke wazi msimamo wangu kisiasa hasa kwa nchi yetu tukufu Tanzania.

Kwa muda wote wa maisha yangu nimekuwa upande wa CCM tangu nikiwa kijana mdogo nikicheza chipukizi na kushiriki shughuli nyingi za kisiasa mfano maazimisho ya CCM, mbio za mwenge na yanayofanana na hayo.

Muda wote huo naweza kusema nilikuwa muumini wa mrengo wa ujamaa na nilikuwa mpenzi halisi wa siasa za Mwl Nyerere na zinazofanana nazo mfano za Julius Malema na Magufuli kwa sasa.

Ila hali imebadilika katika mawazo yangu baada ya kutembea huku na huko duniani hasa nchi za Ulaya na kujionea namna mifumo ya kitaasisi, ustawi wa jamii, uhuru wa watu na miundombinu ilivyopiga hatua kubwa zaidi katika ulimwengu huu uliostaaarabika.

Kwa sasa nimekuwa muumini wa mrengo wa kibepari ama kibeberu dhana zinazoonekana ovu na chanzo cha umasikini wa nchi yetu hali ambayo haina ukweli wowote. Ni propaganda tu ya watawala.

Ubepari ama ubeberu unaotoa uhuru wa watu kujiamulia mambo yao wenyewe na kuiwajibisha serikali ikiwa itakwenda kinyume na matakwa ya watu walioiweka madarakani.

Ubepari ama ubeberu unatoa uhuru wa kujieleza na hivyo kuchochoea ubunifu na uvumbuzi na hivyo kuwa na mawazo mengi ya biashara na hivyo kuchochea uchumi na upatikanaji wa ajira.

Ubepari ama ubeberu unaamini katika nguvu ya sekta binafsi na makampuni na kuichukulia serikali sehemu ya wadau wa kuleta maendeleo katika usawa; serikali kwenye ubeberu ni mdau kama ilivyo sekta binafsi katika governance.

Kutokana na utangulizi huu naweka wazi kwamba kwa sasa licha ya kwamba nampenda Rais Magufuli kwa kuwa ni binadamu mwenzagu, NACHUKIA SANA SERA ZAKE kama ifuatavyo.

Kujifanya anajua kila kitu na hivyo hahitaji kusikiliza wengine wanasema nini.

Kuamini kwamba serikali ni kila kitu katika governance na hivyo sekta binafsi si lolote na inapaswa kufuata serikali inataka nini.

Watu kupigwa risasi, kuuwawa na kupotea, lakini yeye akiwa kimya kiasi cha kutiliwa shaka kwamba huenda yeye ndiye mtekelezaji kupitia watu wake.

Kuminya uhuru wa kujieleza, sasa kila mtu ana hofu ya kuzungumza dhidi ya serikali

Ushamba wa kugawa hela hadharani

Kufokea na kutumbua watu hadharani ili hali anaweza kuwaita watu ofisini na kurekebisha mambo akiheshimu utu wa watu.

Kutumbua watumishi wote wenye vyeti feki ilihali anamuacha Makonda ambaye ni wazi anatumia cheti cha mtu mwingine, hii ni dhambi kubwa sana.

Ukurupukaji katika kubuni na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, barabara zote, madaraja na majengo yote yaliyojengwa chini yake akiwa waziri na sasa akiwa Rais hayana uhai wa muda mrefu, yameanza kuharibika. TAIFA LITARAJIE HASARA KUBWA NA KULAZIMIKA KUJENGA UPYA .

Kuwaminya wanasiasa wengine wasizungumze na wananchi.

HIVYO HAYA NI MACHACHE ILA YANAONESHA AINA YA HOJA ZANGU NITAKAPOKUWA NAANZISHA MADA AMA KUCHANGIA.

MWISHO, NAVUTIWA SANA NA SERA ZA CHADEMA, LISSU NAYE AMENIVUTIA SANA, ANAONEKANA NI MTU JASIRI MWENYE NIA HASA YA KUJENGA MFUMO IMARA WA UTAWALA AMBAO HAUTATEGEMEA AMRI ZA MTU MMOJA TOFAUTI ILIVYO KWA RAIS MAGUFULI.

AHSANTENI SANA
 
Wafuasi wa CCM ya Nyerere hatuhami chama tunakua kifikra na kuwa na free thinking daima na tunashauri na kutahadharisha bila woga, wasalimie hao washindani wetu kila la kheri
 
Back
Top Bottom