Naomba kufundishwa Kiswahili chenye maandishi ya Kiarabu

sasa tunatumia herufi ya kirumi(latin alphabet, kama vile a,b,ch,d) lakini kabla ya miaka 100, herufi ya kiarabu ا ب ت ilitumika kuandika kiswahili.


Wafundishe hawa waswahili wasiojua historia ya lugha yao,🤣
 
Hiyo ni Tenzi (poem) ya kiswahili cha kale (kutoka Lamu ??) katika maandishi ya kiarabu.

Nimeweza kusoma sehemu ya maneno haya:- "nini wanasibasa mafundi wa kila fani".
Ndiyo, mwandishi wa utenzi wenyewe anatoka Lamu. Huyu bwana anachukia sana herufi ya kirumi, yeye hutumia herufi ya kiarabu maishani mwake.
 
ndiyo, mwandishi wa utenzi wenyewe anatoka Lamu. huyu bwana anachukia sana herufi ya kirumi, yeye hutumia herufi ya kiarabu maishani mwake.

Naomba nikuulize swali, unahitaji kujua hayo maandishi kwa matumizi gani?

Maana kwa uelewa wangu, kati ya watu 5000 wanaojua Kiswahili unaweza kupata 1 au usipate kabisa anaeyaelewa hayo maandishi.

Sasa yatakuwa na faida gani kama utayajua na ukose watu wa kuwasiliana nao kwa kutumia maandishi hayo?
 
ndiyo. nasikia kuwa baadhi ya wazanzibari wanaelewa kiswahili kama hicho, hata nembo ya Chuo Kikuu cha Zanzibar ina herufi hizo. Je, huku kuna mzee mzanzibari anayeweza kunisaidia?
View attachment 1681760


Hayo maneno katika hiyo nembo ni maneno ya kiarabu yenye maana ya:- Chuo kikuu cha Zanzibar (Jami'ah zanjibar جامعة زنجبار).
 
Naomba nikuulize swali, unahitaji kujua hayo maandishi kwa matumizi gani?

Maana kwa uelewa wangu, kati ya watu 5000 wanaojua Kiswahili unaweza kupata 1 au usipate kabisa anaye yaelewa hayo maandishi.

Sasa yatakuwa na faida gani kama utayajua na ukose watu wa kuwasiliana nao kwa kutumia maandishi hayo?
Kwa kusudi la kusoma vitabu vya kale. Kabla ya kuja kwa wazungu, maandishi yote ya kiswahili yapo kwenye herufi ya kiarabu. Ningalifanya utafiti wa lugha na utamadini wa Kiswahili ningaliweza kuvisoma vitabu vya kale vilivyoandikwa namna hivyo.
 
kwa kusudi la kusoma vitabu vya kale. Kabla ya kuja kwa wazungu, maandishi yote ya kiswahili yapo kwenye herufi ya kiarabu. ningalifanya utafiti wa lugha na utamadini wa Kiswahili ningaliweza kuvisoma vitabu vya kale vilivyoandikwa namna hivyo.

Hapo nimekuelewa vizuri, ninatumaini utafanikiwa kumpata mwenye uelewa wa hayo mambo.
 
kwa kusudi la kusoma vitabu vya kale. Kabla ya kuja kwa wazungu, maandishi yote ya kiswahili yapo kwenye herufi ya kiarabu. ningalifanya utafiti wa lugha na utamadini wa Kiswahili ningaliweza kuvisoma vitabu vya kale vilivyoandikwa namna hivyo.


Ndugu Bakari ili uweze kusoma hiyo lugha ni lazima kwanza ujifunze kusoma kiarabu na uanze mwanzo kabisa:- ا ب ت ث ح خ----

Kwakuwa ninaona wewe ni mwepesi sana kuelewa nadhani ukipata mwalimu mzuri unaweza kujua kusoma Maandishi ya kiarabu ndani ya miezi 6 tu.
 
Ndugu Bakari ili uweze kusoma hiyo lugha ni lazima kwanza ujifunze kusoma kiarabu na uanze mwanzo kabisa:- ا ب ت ث ح خ----

Kwakuwa ninaona wewe ni mwepesi sana kuelewa nadhani ukipata mwalimu mzuri unaweza kujua kusoma Maandishi ya kiarabu ndani ya miezi 6 tu.
Kweli bwana, ufundishaji wa Kiarabu nchini China umepata maendeleo makubwa sana. Nitamtafuta mwalimu atakayenifundisha herufi hizo ili nipate ujuzi zaidi. Shukrani sana
 
View attachment 1681618
hayo ni maandishi ya kiswahili ya kale, iliyoandikwa na herufi ya kiarabu, sivyo?
8765432.jpg
 
Kama tujuavyo, Kiswahili husifiwa kama lugha ya rasmi ya Tanzania. Lakini kabla ya kusanifishwa, Kiswahili kilikuwa kimeandikwa kwenye herufi ya Kiarabu kwa muda mrefu sana. Naomba kuwauliza ninyi wapendwa wenzangu wa JF, nani mtaalamu wa lugha anaweza kunifundisha Kiswahili kilichoandikwa kwenye maandishi ya Kiarabu?

Nahitaji kukisoma kitabu chenye umri zaidi ya miaka 100, lakini nimeshindwa kuelewa kinachosema. Hebu mtaalamu yupi anisaidie! Shukran
我是坦桑尼亚人,我还在郑州大学留学,河南省。如果你需要学会咋们当地人的语言咋们俩可以联系。
微信号:k201414k
FB_IMG_1592387450118.jpg
 
Hicho kiswahili hakikuwa na kibantu?
Kiswahili ni lugha ya kibantu lakini mnamo muda mrefu uliopita kabla ya wazungu kuja, Kiswahili kiliandikwa kwenye herufi ya kiarabu. leo tunatumia a,b,ch,d, lakini kabla ya miaka 100 watu walitumia ا ب ت ث ح خ kama ishara ya matamshi ya Kiswahili.
 
Kiswahili ni lugha ya kibantu. lakini mnamo muda mrefu uliopita kabla ya wazungu kuja, Kiswahili kiliandikwa kwenye herufi ya kiarabu. leo tunatumia a,b,ch,d, lakini kabla ya miaka 100 watu walitumia ا ب ت ث ح خ kama ishara ya matamshi ya kiswahili.
Mimi nilishawahi kusikia hili suala.
Na kwa namna ulivyoelezea pia nimeelewa na kwa mtu anaetaka kujua pia atakuwa amekuelewa.
Shida ni kwamba wengine hii taarifa kwao inakuwa ngumu kuikubali si kwa sababu hawaelewi bali hawataki tu kuamini.
Nakuombea heri uweze kufanikiwa mkuu.
 
Back
Top Bottom