Naomba kufahamu wizi wa magari unafanyikaje

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Habari wakuu.

Kuna kitu hua nashindwa kukielewa hasa wizi wa magari.

Je wizi wa gari unafanyikaje kama gari imefungwa.

Je unakutamwizi ana funguo ya ziada ama nini kinafanyika.

Je kwa gari ambazo ni keyless za push to start pia zinaibiwaje maana nyingine kama hujaingia na ufunguo haiondoki.

Naomba kufahamishwa wizi unafanyikaje.

Ahsante.
 
Kuna dada mmoja alikua anadrive harrier..bas akawa anampelekea kaka mmoja aioshe...anamwachia anarudi zake kazini...huyu dogo alikua form 6 leaver hana mishe....
Anahvyodai walitokea wakaka wakamwambia huu ndo utajiri wako... wakamfundisha ulaghai...naskia kichonga key ni dk 1...so wakachonga key wakamchorea ramani fresh...mwaka.jana dada wa watu kaibiwa gari akiwa kazini...
Naskia ni risk mno kumwachia gari na keys muosha magari..wanachonga keys unakuja ibiwa siku isiyo na jina....dogo yuko ndani mpka leo
 
Habari wakuu.

Kuna kitu hua nashindwa kukielewa hasa wizi wa magari.

Je wizi wa gari unafanyikaje kama gari imefungwa.

Je unakutamwizi ana funguo ya ziada ama nini kinafanyika.

Je kwa gari ambazo ni keyless za push to start pia zinaibiwaje maana nyingine kama hujaingia na ufunguo haiondoki.

Naomba kufahamishwa wizi unafanyikaje.

Ahsante.
1. Alarm system...kuna kifaa chenye nguvu kubwa zaidi ya alarm uliyofunga hicho kikisetiwa alarm yako inakuwa boko watu wanafanya yao
2. Kwenye carwash na garage za uchochoroni, ukiacha funguo vijana wasio waaminifu wanaikandamiza kwenye kipande cha sabuni au wanaichora kwenye karatasi wanawapa wezi wakachonge nyingine, kifuatacho hapo ni kilio
3.Keyless/push start wanakuwa na kijimtambo kidogo cha kuhack hiyo system na kui command watakavyo, baada ya hapo wanaamua tu sasa wafanye nini kwenye hiyo gari
4. Japo kwa uchache sana, unavamiwa na kuporwa gari live
 
Ndugu Hakimu Mfawidhi kila nikijaribu kutafakari swali lako akili inaniambia kama uliibiwa IST sasa kwa maumivu uyapatayo unataka ku revenge kwa kung'oa V8 ya mheshimiwa mmoja hapo mtaa wa tatu.
Samahani lakini ni mawazo tu
😂😂😂Hapana mkuu. Siendeshi IST na wala sijawahi kumiliki IST.

Nimetaka tu kujua inakuaje mtu hana funguo halafu anaiba gari.
 
Kuingia ndani ya gari lililofungwa huwa ni rahisi sana haichukui sekunde kumi...sasa mtu akishaingia ndani ya gari kitakachofuata ni kukata waya wa funguo then wanaonganisha nyaya chuma kinasepa
Wanaingiaje mkuu.
 
😂😂😂Hapana mkuu. Siendeshi IST na wala sijawahi kumiliki IST.

Nimetaka tu kujua inakuaje mtu hana funguo halafu anaiba gari.
Kama ilivyo waache wafu wawazike wafu wenzao ndivyo vivyo hivyo waache wenye fani wafanye kwa ufanisi wa fani zao.
 
Kuingia ndani ya gari lililofungwa huwa ni rahisi sana haichukui sekunde kumi...sasa mtu akishaingia ndani ya gari kitakachofuata ni kukata waya wa funguo then wanaonganisha nyaya chuma kinasepa

Huwa naona sana kwenye movie,kumbe inawezekana?
 
Back
Top Bottom