Naomba kufahamu wasifu wa Aron Kagurumujuli, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,653
218,143
Inasemekana huyu ndio Mkurugenzi wa kwanza kuwahi kuwepo kwenye Manispaa ya jiji la DSM na kutokomea na Viapo vya mawakala wa chama cha siasa walioapa kihalali ili kusimamia chama chao kwenye vituo vya kupigia kura kama sheria inavyoelekeza.

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba , kama atatekeleza mipango yake anayoipanga gizani kuhusiana na uchaguzi wa Kinondoni , basi jina lake laweza kuingia kwenye kitabu cha kumbukumbu za Watanzania watakaokumbukwa kwa kitambo kirefu

Kutokana na uzito wa aibu aliyojitwisha kijasiri ili kuokoa chama chake cha ccm , nimeona nije kwenu ili tumfahamu vizuri mtu huyu mtiririko wa utendaji wake pote alipopita ikiwa ni pamoja na kiwango cha elimu yake pamoja na shule alizopitia .

Natanguliza shukrani .
 
Mkuu nioneshe ni kifungu gani cha sheria ya uchaguzi kinasema mawakala wataondoka na viapo vyao nyumbani.
Chadema mnatengeneza tension na hofu isio na maana,wakala akishapata barua ya uteuzi iliopigwa muhuri shughuli imeisha,hayo makaratasi ya kuapa sio muhimu tena,acheni kuwahadaa wafuasi wenu
 
Tangu lini mmekuwa mkibaki na viapo vya hao mawakala? Kama ni makaratasi si muwape, kama makaratasi hayo sio muhimu, kwanini mnayang'ang'ania?
 
Mmefumaniwa vibaya sana kudadeki !
 
Mkuu nioneshe ni kifungu gani cha sheria ya uchaguzi kinasema mawakala wataondoka na viapo vyao nyumbani.
Chadema mnatengeneza tension na hofu isio na maana,wakala akishapata barua ya uteuzi iliopigwa muhuri shughuli imeisha,hayo makaratasi ya kuapa sio muhimu tena,acheni kuwahadaa wafuasi wenu
Na wewe tuoneshe kifungu cha sheria ambacho kinasema ukishaapa usiondoke na kiapo
 
Inasemekana huyu ndio Mkurugenzi wa kwanza kuwahi kuwepo kwenye Manispaa ya jiji la DSM na kutokomea na Viapo vya mawakala wa chama cha siasa walioapa kihalali ili kusimamia chama chao kwenye vituo vya kupigia kura kama sheria inavyoelekeza.

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba , kama atatekeleza mipango yake anayoipanga gizani kuhusiana na uchaguzi wa Kinondoni , basi jina lake laweza kuingia kwenye kitabu cha kumbukumbu za Watanzania watakaokumbukwa kwa kitambo kirefu

Kutokana na uzito wa aibu aliyojitwisha kijasiri ili kuokoa chama chake cha ccm , nimeona nije kwenu ili tumfahamu vizuri mtu huyu mtiririko wa utendaji wake pote alipopita ikiwa ni pamoja na kiwango cha elimu yake pamoja na shule alizopitia .

Natanguliza shukrani .
Ninachojua ni mhitimu wa BED (Adult Education) UDSM class of 2006
 
Tangu lini mmekuwa mkibaki na viapo vya hao mawakala? Kama ni makaratasi si muwape, kama makaratasi hayo sio muhimu, kwanini mnayang'ang'ania?
Unapoteza muda na wafia chama makinikia hao. Hizo ndio mbinu zao za ushindi wanajua walishachokwa.
 
Mkuu nioneshe ni kifungu gani cha sheria ya uchaguzi kinasema mawakala wataondoka na viapo vyao nyumbani.
Chadema mnatengeneza tension na hofu isio na maana,wakala akishapata barua ya uteuzi iliopigwa muhuri shughuli imeisha,hayo makaratasi ya kuapa sio muhimu tena,acheni kuwahadaa wafuasi wenu
Tension lazima iwepo kwa sababu ya tabia za kihuni zinazofanywa na hawa watu. Au we unajifanya hujui,sheria ni kufanya anachotaka mfalme kutoka chattle.Kwani mara ngapi mawakala wa upinzani wametimuliwa pmj na kuwa na barua kwa kisingizio cha hawakuapishwa?Ndicho kilichotokea kwenye uchaguzi wa madiwani.Mtulia hauzuki atashinda kwa sabab mfalme ameamua başı!!!!!!
 
Back
Top Bottom