Naomba kufahamu SIWA ile ya bungeni inamaanisha nini?

florence

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
423
161
Habari zenu wana JF
Kuuliza sio ujinga wajameni, nimekuwa nikiwauliza watu tofauti tofauti lakini kilamtu anajibu lake.
leo nimeamua niulize hapa naimani nitapata majibu sahihi.
Ile wanaita SIWA inayowekwa mbele ya spika wa bunge ina maana gani? na kazi yake ni nini?
Asanteni kwa kunielewesha
 
Ni matunda ya ukoloni tu haina maana yoyote labda kama SIWA hiyo ingetengenezwa kwa kinyago cha mnyama kama twiga, faru au simba ikiwa ni kuutangaza utalii wetu. Na katika hili la ukoloni hakuna nchi iliyopona. Watakujibu kwamba ni katika mabunge yote ya Jumuiya ya Madola, ndiyo nini, si kukumbuka mkoloni wetu. Mara vifimbo vya malkia , yote haya ni ukoloni uleule.
Lakini inawezekana SIWA ina faida kwa kutoa ajira maana hapo bungeni liwe la Tanzania ama la Afrika Mashariki wapo watu wameajiriwa kubeba hilo li chuma, ndiyo kazi yao tu! Mungu akupe nini?
 
Mkuu ndio maa a serikali wameamua kuweka division 5, maana majibu kama haya Ni shida tupu
 
Habari zenu wana JF
Kuuliza sio ujinga wajameni, nimekuwa nikiwauliza watu tofauti tofauti lakini kilamtu anajibu lake.
leo nimeamua niulize hapa naimani nitapata majibu sahihi.
Ile wanaita SIWA inayowekwa mbele ya spika wa bunge ina maana gani? na kazi yake ni nini?
Asanteni kwa kunielewesha

Katika historia ya kudai kusikilizwa, walalahoi wa Uingreza ambao utawaliwa na ukoo wa kifalme, walitaka na wao wawe na nchango wao katika sheria zinazowahusu. Katika kutafuta namna ya kufikisha matakwa yao kwa watawala wao, yaani Mfalme na watu wake, wakamtuma mmoja wao aende kama msemaji wao yaani spika. Msemaji huyo alikuwa anaogopa sana maana mfalme alikuwa na vyombo vya dola. Akalazimishwa na wenzake na walipokubaliwa kukutana na kujadiliana kuhusu namna ya kutawaliwa, na siyo namna ya kujitawala, wakawa wanaweka alama maalum ya uwakilishaji wa Mtawala. Hapa kwetu kama alivyosema mchangiaji mmoja ni matunda ya ukoloni ulitaka akili na mifumo yetu ya kufikiri. TUNAKOSA UBUNIFU NA UTAMADUNI NDIYO MAANA TUNAISHI KAMA VIVULI VYA WENGINE.
 
Tuseme hivi: kuwepo siwa ni ishara ya bunge kuendelea na shughuli zake na kulinda uhuru wa mbunge kuchangia. Tuseme hivi ni kama makabila yetu hapa nchini mtu akiingia ndani ya nyumba ANAKITA mkuki kizingiti cha nyumba kuonyesha kuwa yumo ndani ya nyumba anahitaji utulivu!!
 
Katika historia ya kudai kusikilizwa, walalahoi wa Uingreza ambao utawaliwa na ukoo wa kifalme, walitaka na wao wawe na nchango wao katika sheria zinazowahusu. Katika kutafuta namna ya kufikisha matakwa yao kwa watawala wao, yaani Mfalme na watu wake, wakamtuma mmoja wao aende kama msemaji wao yaani spika. Msemaji huyo alikuwa anaogopa sana maana mfalme alikuwa na vyombo vya dola. Akalazimishwa na wenzake na walipokubaliwa kukutana na kujadiliana kuhusu namna ya kutawaliwa, na siyo namna ya kujitawala, wakawa wanaweka alama maalum ya uwakilishaji wa Mtawala. Hapa kwetu kama alivyosema mchangiaji mmoja ni matunda ya ukoloni ulitaka akili na mifumo yetu ya kufikiri. TUNAKOSA UBUNIFU NA UTAMADUNI NDIYO MAANA TUNAISHI KAMA VIVULI VYA WENGINE.

Walau sisi tuliacha kumvalisha Spika wetu haya Mawigi. Wenzetu kule Kenya bad wanaendeleza kasumba. Marehemu Adam Sapi Mkwawa alipokuwa Spika alikataa kabisa kuvaa wigi kwa kuwa sio utamaduni wetu.

thumbnail.php
 
BADO HAITOSHI KWA WATU WENYE UTASHI KIUTENDAJI, (executive free will) ACHILIA MBALI UTASHI KISIASA. TUNAKOSA YOTE MAWILI.
 
Lile Siwa la dhahabu linalowekwa bungeni ili kuashiria kuanza kwa kikao cha bunge ni ishara nzito mno ya minyororo ya kikoloni.
Napendekeza utamaduni wa kubeba hiyo Siwa tuuache mara moja,maana inatukumbusha ukubwa wa mkandamizi wetu na udogo wa uhuru wetu.
 
ile siwa ni kama mungu wa baniani maana halina sababu yoyote kuliheshimu na kuliinamia ni kumkosea mungu
 
Back
Top Bottom