Naomba kufahamu sheria kuhusu kurudisha bidhaa yenye warrant

resonanceiduufu

Senior Member
Jul 29, 2016
112
62
Naweza kuchukua hatua gani ikiwa mwenye duka amekataa kupokea bidhaa aliyoniuzia kwa "warranty"? Tafadhali naomba msaada.
 
Subiri makonda au magufuli akihutubia ukajilize then upewe nafasi ya kuongea. Nakuhakikishia tv yako utalipwa mbili mpya hapo hapo. Kwani mkuu umenunua bidhaa gani
 
Vigezo na masharti ya warranty ni vipi??

Maana isije ikawa umekiuka masharti ya hiyo warranty...
Vigezo vyote ninavyo, na nimerudisha bidhaa within 48 hrs na warranty ni 12 months... Mwenye duka anatumia mabavu hadi wafanyakazi wake wanamshangaa kwa analolifanya "anasema tatizo ni Fulani kwenye kifaa" Ila hatoi msaada wowote wala conclusion kama nasaidiwa au sisaidiwi!...
Alijua wazi kuwa tatizo lingejitokeza ila kulitatua inakula kwake!
... Na Mimi sitaki ile kwangu! Ndo maana nauliza kuhusu sheria ya warranty!
 
Ngoja waje mkuu.. m imeshanitokea hii yaan mwenye duka anakuruka as if hajakuuzia
 
Vigezo vyote ninavyo, na nimerudisha bidhaa within 48 hrs na warranty ni 12 months... Mwenye duka anatumia mabavu hadi wafanyakazi wake wanamshangaa kwa analolifanya "anasema tatizo ni Fulani kwenye kifaa" Ila hatoi msaada wowote wala conclusion kama nasaidiwa au sisaidiwi!...
Alijua wazi kuwa tatizo lingejitokeza ila kulitatua inakula kwake!
... Na Mimi sitaki ile kwangu! Ndo maana nauliza kuhusu sheria ya warranty!
Kimsingi uhusiano wenu ni wa kimkataba, kwa maelezo hayo uliyonipa waweza fungua kesi ya madai kwa mafanikio tunza ushahidi muhimu...
 
Asante sana!
Ushahidi nilionao ni "riceipt" inayoonesha kiasi nilichonunua + warranty yake! Pia wakati nanunua nilikuwa na wenzangu wawili 2!

Shukran kwa msaada wako!
 
Receipt ni ya mashine au kanjanja

Sent from my SM-G955F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom