Gen ipi unayoiulizia? Au mwaka upi? Kuna W245 (Gen 1: 2004), W246 (Gen 2: 2011) na W247 (Gen 3: 2018), at least tuanzie hapa.
Shida ya Mercedes sio kama wenzie, izo namba ulizosema 170 na 180 hazimaanishi engine size (zamani zilikua zinamaanisha).
Yaani siku hizi 180 haimaanishi 1.8L engine kama zamani. Ingawa 170 nahisi ni naming ya zamani so ni 1.7L petrol engine, gen 1 ya miaka ya 2000s.
Ila iyo 180 utata inaweza kua 2.0L ya gen 1, au 1.5L ya gen 2, au 1.8 kwenye Gen 2 au 1.3L ya gen 3. Vurugu tupu.
Atleast mwaka ungesaidia kujua tunaongelea gari ya gen ipi.
Yote 9, kama imezidi miaka 15 ebu angalia upande mwingine. German cars zikishavuka miaka 10 tu ni mtiti, sembuse 15.