genus
Senior Member
- Dec 28, 2015
- 167
- 69
Nimekuwa hapa mwanza kwa muda, kuna vitu huwa navishangaa jinsi vinavyoendeshwa, kuna ukiukwaji mwingi wa sheria na taratibu sijui ni kwa sababu wakazi wake ni wapole sana au ni kutokufahamu haki zao.
Mfano kuna msiba umetokea hapa karibu na sehemu ninayoishi barabara Balewa ni kama mita 600 kifika gate la kuingia hospital ya mkoa Sekouture, katika hali isiyokuwa ya kawaida wafiwa wamepanga mawe na magogo barabarani wakafunga njia barabara ya lami haipitiki hata kwa boda boda, cha kushangaza ni zaidi ya saa 48 tangu barabara imefungwa, sasa najiuliza nani kawapa kibali cha kufunga barabara muda wote huo?
Mbona viashiria vya kufunga barabara havizingatii sheria za barabarani? au na penyewe mpaka aje Magu aagize kama barabara ya Airport?
Najaribu kufikilia kuwa ile barabara niya muhimu sana na moja ya msaada wake mkubwa ni kupitisha magari ya wagonjwa kuingia hospital au kuwapeleka Bugando.
Jamani tunawaomba wahusika wachukuliwe hatua.