Naomba kufahamishwa matumizi ya mmea datura

Joseph Kanigi

Member
Nov 13, 2018
6
0
Nimekuwa nikiufatilia sana huu mmea lakini sijapata majibu Kama yupo anaejua matumizi yake anisaidie.

th%20(1).jpg
 
Datura stramonium aka Jimsonweed.!
Usiseme umefuatilia, ungeshapata majibu.
 
Ni mmea vamizi/ invasive plant species umevamia ngorongoro, ni sumu. Unataarifa nyingi mno labda useme unahitaji kujua zaidi kuhusiana na nini?
 
Nimekuwa nikiufatilia sana huu mmea lakini sijapata majibu Kama yupo anaejua matumizi yake anisaidie.

View attachment 2689441
Ok. Najua unaufahamu sana na pia unazo habari nyingi juu ya mmea huu. Lakini elimu haina mwisho. Jazia na haya:
1. Zamani mmea huo ulitumika kuwabaini wezi,wachawi, wauaji(Mtu aliyeua lakini kwa siri)yaani tuseme wazee waliutumia kuHypnotise wahalifu ili wafunguke na kutoa siri kwa kile wanachotuhumiwa nacho.(Wachaga waliuita mchakato huo kama kumnywesha mtuhumiwa Kimanganu).
2. Mmea huo ni mmojawapo wa mimea yenye sumu - Ni sumu(Poisonous plant).
3. Katika hali ya kawaida, mmea huo hutumika kutibu jino/meno yenye wadudu yaliyotoboka(hauhitaji kung'oa jino kama limepekechwa /toboka na linauma.
4. Mmea huo ni mmojawapo wa gugu(weed) hatari shambani kwako. Kuudhibiti mmea huo shambani kwako ni shughuli pevu.
5. Mmea huo pia hutumika kutibu mtu mwenye ukichaa(Matatizo ya afya ya akili).
NB: Kuna species mbili au zaidi hapa Tz na huota sana pembeni mwa njia, barabara lakini species yenyekutoa maua ya zambarau ndo inayotumika zaidi kitiba.
 
Achana nao mzee, bora ule ndum!! Datura (jimson weed), shrooms (magic mushroom) etc, hizo mimea ni majini kabisa hayo, kuna namna ukiyatumia kwenye meditation unaona hadi wabaya wako!
 
Ok. Najua unaufahamu sana na pia unazo habari nyingi juu ya mmea huu. Lakini elimu haina mwisho. Jazia na haya:
1. Zamani mmea huo ulitumika kuwabaini wezi,wachawi, wauaji(Mtu aliyeua lakini kwa siri)yaani tuseme wazee waliutumia kuHypnotise wahalifu ili wafunguke na kutoa siri kwa kile wanachotuhumiwa nacho.(Wachaga waliuita mchakato huo kama kumnywesha mtuhumiwa Kimanganu).
2. Mmea huo ni mmojawapo wa mimea yenye sumu - Ni sumu(Poisonous plant).
3. Katika hali ya kawaida, mmea huo hutumika kutibu jino/meno yenye wadudu yaliyotoboka(hauhitaji kung'oa jino kama limepekechwa /toboka na linauma.
4. Mmea huo ni mmojawapo wa gugu(weed) hatari shambani kwako. Kuudhibiti mmea huo shambani kwako ni shughuli pevu.
5. Mmea huo pia hutumika kutibu mtu mwenye ukichaa(Matatizo ya afya ya akili).
NB: Kuna species mbili au zaidi hapa Tz na huota sana pembeni mwa njia, barabara lakini species yenyekutoa maua ya zambarau ndo inayotumika zaidi kitiba.
Nashukuru , Sana na Kama jino lililotoboka hutumikaje mkuu,
 
Ni mchakato unaohitaji uangalifu kwani unahitaji kuzichoma mbegu zake na kisha kuuruhusu moshi wake uingie kinywani lakini bila kuuvuta kama sigara. Papo hapo unakuwa umetega chujio (chujio la chuma) juu ya chombo utakachokitumia kuziunguza mbegu hizo. Moshi utokao kwenye mbegu hizo zitakazokuwa zinaungua utaupitisha kwenye kitu kama vile bomba ili uingie mdomoni kisha unaurudisha nje kuelekea kwenye chujio. Kazi ya chujio ni kuwanasa wadudu watakaotoka mdomoni (kwenye meno/jino) wasiangukie kwenye moto ili uweze kuwaona kwa macho.
 
Ubarikiwe kiongozi ,
 
Huo mmea Ni sumu mbaya Sana if ingested. Majimaji yake yakidondokea kwenye ulimi, ulimi unavimba na kuzuia hewa kuingia mwilini. Yani unakufa umejiona.
Weka mbali Sana na watoto.
 
Loooh salaleee 🙆!! Wafa wagenda hivi hivi unajiona. Huo Kwakweli ni stay away plant ☘️.
 
Back
Top Bottom