Naomba kuelimishwa kuhusu ufagaji wa samaki ziwa Victoria

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,190
Kumekuwa na ufugaji mkubwa wa samaki katika Ziwa Victoria. Kwa takwimu nilizo nazo asilimia 80 ya wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria kwa sasa wanatumia samaki hawa wa kufugwa kama chakula chao tofauti na hapo zamani.

Chakula cha samaki hawa kinatengenezwa na ndugu zetu Wachina. Hatujui wanatumia mchanganyko gani katika kutengeneza chakula hiki na sijui kama Serikali ina mkono wake katika kuhakikisha kuwa chakula kinachotengenezwa ni safi na salama.

Nimetonywa na mvuvi mmoja kuwa samaki wasiofugwa bahati mbaya wanapokaribia vizimba hivi hupata harufu mbaya na hukimbia mbali sana mpaka hata kilomita 40 kuepuka harufu hiyo.

Ni vema sasa Serikali(Idara ya Uvuvi) ikatoka na kuhabarisha wananchi wa Kanda ya Ziwa kuhusu usalama wa samaki hawa ikichukuliwa kuwa watengenezaji wa vyakula ni Wachina ambao kwa kiasi kikubwa ni wajajnja sana na shida yao ni faida kubwa. Tuchukue tahadhari tusije tukawa Taifa la mazezeta kutokana na hawa samaki wa kufugwa.

Nawasilisha.
 
Mkuu BwanaSamaki012 naomba maelezo yako ya kina kama kuna ukweli wowote kwenye hayo maandishi niliyo ya Bold. ahsante sana
 
Sato wengi sana sasa hivi mpaka nilishagaili kula sato ni weusi mno kuashiria something is wrong
Hujui kuna sato weusi zaidi,blue,wekundu na wamabaka? Utakuwa hujawahi kuvua au kuishi ziwani.
Kiasili hao weusi unao wazungumzia wewe ndo watamu na mara nyingi wavuvi hula hao supu yake ni kama maziwa fresh nzito na ikipoa juu hubaki na utando.

Wanao fuata ni bhugulusi wao ni wekundu ila sio watamu sana kivile ila wananyama nyingi wale wenye ublue ndo watamu zaidi ila hawakuwi na wana mifupa mikali.
 
Sato wengi sana sasa hivi mpaka nilishagaili kula sato ni weusi mno kuashiria something is wrong
Unashangaa nini sasa! Hao wanaofugwa ndio wanaosafirishwa! Sisi wa ziwani tunakula wanaotoka visiwa vya Sozigwa!
 
Back
Top Bottom