Naomba kazi ya uzoefu huu;-

Doreen27

Member
May 9, 2021
8
75
Habari wanajamvi?

Mimi ni jinsia Ke, umri miaka 28, Elimu shahada, sekta ya afya, fani ya Uuguzi, bado sijapata leseni hivyo imekuwa ngumu kwangu kupata nafasi kwenye hospitali kwa kujishkisha muda huo nikiwa nasubiria kupata leseni yangu ambayo uwezekano wa kuipata ni mwezi wa 7 mwaka huu.
Kwa mantiki hii ninaomba kazi yeyote inayoweza kuniweka mjini ikiwemo ya fani yangu niliyosomea kwa muda huo ambao bado nasubiria kupata leseni na kuhangaikia kuipata ajira pia

Nina uzoefu huu;-

1) Naweza kuandaa na kuandika Concept notes kwa ajiri ya research proposals kwa upande wa Afya.

2) Naweza kuandaa na kuandika research proposal zinazohusiana na tafiti za afya.

3) Naweza kufanya data analysis kwa kutumia SPSS.

4) Naweza kuandaa na kuandika research report.

5) Naweza kutumia Komputa kwa ustadi.

6) Naweza kusimamia biashara vizuri na kwa uaminifu mkubwa.

8) Naweza kuwa partner kwenye biashara au kazi yoyote ile halali isiyo na athari kiafya inayoweza kuniingizia kipato na kuniwezesha kuishi.

9) Naweza kufanya kazi kwenye M-pesa, ninao uzoefu niliwahi kufanya kazi hiyo ya m-pesa mwaka 2014.

10) Naweza kukalimani lugha ya Kingereza - Swahili kwa ufasaha.

11) Naweza kutoa ushauri na nasaha kwa changamoto zote za kiafya.

12) Naweza kuuza duka la vifaa vya umeme, simu, nguo, vipodozi na maduka yanayoendana na hayo.

13) Naweza kufundisha masomo ya Chemistry, biology and Geography kuanzia form 1- form 6.

14) Ninaweza kufanya kazi kwenye clinic ya mama na mtoto kama Muuguzi/mkunga.

15) Naweza kufanya kazi ya sales representative.

Naomba mwenye kazi kati ya hizo au mwenye connection ya kazi kati ya hizo anishike mkono tafadhari, pm tuwasiliane.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom