Nisaidieni nafasi ya kazi

Nisaidieni nafasi ya kazi

urusername

Member
Joined
Feb 11, 2023
Posts
8
Reaction score
11
Habari zenu wakubwa!

Naomba msipuuzie andiko langu, tafadhali!!

Niliyepo mbele yenu ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 22, mkazi wa Dar Es Salaam - Tanzania.
Naandika makala hii mbele yenu kwa lengo moja tu - la kusaidiwa kupata nafasi ya kazi.
Kidato cha nne ndio ukomo wa elimu rasmi niliyobahatika kuipata katika safari yangu ya kimasomo ( cheti ninacho).

Aina ya kazi ninayoomba kusaidiwa kuipata ni - Kazi isiyoumiza
- Sababu nilipata matatizo ya kiafya, yaliyopelekea kufanyiwa OP maeneo fulani hivi mwilini. Kuna wakati napata maumivu na hata uvimbe hujitokeza, hasa pale nifanyapo kazi ngumu inayohitaji kuinama na kuinuka muda wote - inayohusisha kunyanyua vitu vizito kwa muda mrefu sana.


Ujuzi binafsi
Pia, ninao ujuzi usio rasmi kama vile:
- Kutumia computer kwa usahihi ikiwemo na programu zake kama vile Office (microsoft, onlyoffice) pamoja na Adobe Illustrator (kwa kiwango fulani).

Viambatanisho
Ninayo kadi ya Nida, ondoa shaka juu yangu kwa sababu imebeba taarifa zangu zote zenye uhakika 100%.
Pia, ninaishi kwenye makazi ya kudumu (permant address), kwa hiyo wakubwa ondoeni shaka ya kusema wapi pakunipata.
Naweza nikaleta hata barua ya utambulisho ikiwa kama utanihitaji nifanye hivyo.

Udhamini
Kwenye upande wa wadhamini, nipo naye mmoja tu, ambaye ni mama yangu. Hii ikiwa kama utahitaji niwe na mdhamini (sina mdhani mwengine zaidi ya huyo).

Wakubwa, nimehangaika sana tena sana!! kutafuta kazi bila matumaini, hata nikibahatika kuzipata zinakuwa zinanipashida kiasi za kiafya.
Wakubwa naomba mniamini, mimi ni kijana muaminifu sana na wala situmii kilevi chochote kile - pombe, betting, sigara.

Asanteni sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom