Naomba Kama Kuna Mwenye Ufahamu na Uzoefu wa Hii Kitu!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Nilikuwa natazama Star tv, nikakumbana na kipindi kipya kilichoendeshwa na Hilal Riyami.
Kwenye kipindi hiki, Hilal alikuwa akimhoji mtu aliyejiita Dr Joseph Malemi mwenye mashine iitwayo
Nugabest. Kwa mujibu wa dokta huyo hii mashine ni kiboko kwani in uwezo wa kutibu magonjwa
mengi sana hasa yale yasioambukiza. Ametoa maelezo mengi sana ya kusisimua kuhusu mashine
hiyo.
Kwenye familia yangu kuna wagonjwa wengi sana ambao naona wataweza kutibiwa na hiyo mashine
na ninataka niwapeleke kwa huyo dokta lakini..............................

Lakini kwa jinsi nchi hii ilivyo na matapeli wa sampuli nyingi na wenye uwezo wa kupenyeza popote kuanzia ikulu
mpaka bungeni, nasita kuamua kuwapeleka wagonjwa wangu kwa huyu mtu ambaye anasema ana kituo
jijini Mwanza.

Nawaomba wanaJF wa Mwanza (@Charminglady et al)wanichunguzie hii kitu na kunieleza ukweli.
Asanteni.
 
Ceragem machine kama umewai sikia ni kitu kimoja ila soko tu ndio lemebadili jina hazitibu ila zinakupooza tu kwa muda .
 
Unadhani dawa zinapatikanaje?

Kwasababu kuna watu wamefanyiwa majaribi na yakafanya kazi.

Kwahyo ni bora uende wewe na wanafamilia yako halafu ukitibiwa ukapona tunajifunza toka kwako.
 
Back
Top Bottom