Kwa kauelew kangu kadogo, kwenye ×, ni vitu ambavyo huna kwa wakati huo,na kwenye √ ni vitu ambavyo unaweza kuvifanya kutokana na umri ulionao.na wakati ulionao. Kuanzia udogo mpaka uzee
Ni vitu au mambo ya kuwa navyo ktk kipindi au mda usika kwa mfn mtoto anamda na nguvu nyingi lkn kijana au mda kwake ni mfinyu sana mana mambo yamekuwa mengi kila akiangalia mda anaona km vile aimtoshi lkn pesa na nguvu anaweza kuwa nazo za kutosha,ktk umri wa uzeeni nao pia mda na pesa ulizotengeneza ujanani au kwa kuudumiwa na familia zipo lkn nguvu ya kufanya shughuli mwenyewe kwa ufanisi akuna.
Ndo uelewa wangu kuusu picha iyo.
MUDA
Ukiwa mtoto na Mzee una muda mwingi kwa sababu huna vutu vingi vitakavyokusumbua akili. Mtoto yeye anawaza kwenda shule na kucheza. Mzee yeye kuzungumza tu na wajukuu pamoja na kucheza bao.
Kijana hana muda kwa sababu ana vitu vingi vya kufanya na kukamilisha katika wakati mmoja. Anawaza jinsi ya kufika kazini, kuihudumia familia pamoja na Wazee, miradi ya kimaendeleo na vitu kadha wa kadha. Muda kwake ni finyu kwa mambo yake mengi inabidi aweke viporo.
PESA
Mtoto yeye hana pesa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuzitafuta. Kijana na mzee wanazo. Kijana ana nguvu nyingi za kupambana ili apate pesa. Mzee kutokana na kuutumia ujana wake vema aliziokoteza na sasa anazitumia uzeeni. Pia, vijana wake wanamtunza vema hivyo hakosi pesa za hapa na pale.
NGUVU
Mtoto pamoja na kijana wana nguvu za kutosha. Kutokana na ukweli kwamba seli za mtoto bado changa na zinaendelea kukua, mtoto ana nguvu. Kijana kutokana na kujengeka na ujana wake naye si haba, ana nguvu za kutosha. Lakini mzee, mwisho wake unakaribia. Seli zake nyingi sasa hazijizalishi na badala yake mzee anabaki dhaifu na kukosa kabisa nguvu.
Somo,
Jikubali jinsi ulivyo. Kuna mwingine ana kile lakini kingine amekikosa. Kuna wengine ni matajiri, wana fedha na maisha mazuri lakini hawana furaha. Kutwa kwao ni manung'uniko.
Kuna wengine ni maskini wa kutupwa. Wamekosa pesa lakini wana afya njema na furaha tele.
FUrahia jinsi ulivyo, wengine wamekosa kile ulichonacho.
Yes mon, be grateful with life in all stages of your life.
When you are a kid you have Time and Energy but no sources to earn.
Though there are some smart kids out there make more money than most of adults in their 30s.
The image on the center is an adult man. He looks very busy man. He is in his 30s and life seems promising. Nothing can stops him making some $1m when he reaches 40 . He has MONEY and ENERGY but no TIME.
Image on the right is an old age man. He is in 80s. He has Money and Time but his body is tired because of old age.
Good for him he spent his early years well. He has Money...... Money can fix few problems also money can buy you a very good lifestyle. Ask Mzee Mengi utajifunza kitu.
Nyama ya ulimi na mapochopocho pocho mengine kibao
Khakhaakhaaaaa miye teinaaaaaaaaaaaaaaaaaaa lol
I do love this kijana Smart911 very much yani mpaka sijielewiiii Smart911 you know vile nakupenda eeeh!
Nyama ya ulimi na mapochopocho pocho mengine kibao
Khakhaakhaaaaa miye teinaaaaaaaaaaaaaaaaaaa lol
I do love this kijana Smart911 very much yani mpaka sijielewiiii Smart911 you know vile nakupenda eeeh!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.