Nilichoelewa;
MUDA
Ukiwa mtoto na Mzee una muda mwingi kwa sababu huna vutu vingi vitakavyokusumbua akili. Mtoto yeye anawaza kwenda shule na kucheza. Mzee yeye kuzungumza tu na wajukuu pamoja na kucheza bao.
Kijana hana muda kwa sababu ana vitu vingi vya kufanya na kukamilisha katika wakati mmoja. Anawaza jinsi ya kufika kazini, kuihudumia familia pamoja na Wazee, miradi ya kimaendeleo na vitu kadha wa kadha. Muda kwake ni finyu kwa mambo yake mengi inabidi aweke viporo.
PESA
Mtoto yeye hana pesa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuzitafuta. Kijana na mzee wanazo. Kijana ana nguvu nyingi za kupambana ili apate pesa. Mzee kutokana na kuutumia ujana wake vema aliziokoteza na sasa anazitumia uzeeni. Pia, vijana wake wanamtunza vema hivyo hakosi pesa za hapa na pale.
NGUVU
Mtoto pamoja na kijana wana nguvu za kutosha. Kutokana na ukweli kwamba seli za mtoto bado changa na zinaendelea kukua, mtoto ana nguvu. Kijana kutokana na kujengeka na ujana wake naye si haba, ana nguvu za kutosha. Lakini mzee, mwisho wake unakaribia. Seli zake nyingi sasa hazijizalishi na badala yake mzee anabaki dhaifu na kukosa kabisa nguvu.
Somo,
Jikubali jinsi ulivyo. Kuna mwingine ana kile lakini kingine amekikosa. Kuna wengine ni matajiri, wana fedha na maisha mazuri lakini hawana furaha. Kutwa kwao ni manung'uniko.
Kuna wengine ni maskini wa kutupwa. Wamekosa pesa lakini wana afya njema na furaha tele.
FUrahia jinsi ulivyo, wengine wamekosa kile ulichonacho.
Barikiwa.