Naogopa kuomba kazi.

Tanganyika1

JF-Expert Member
May 10, 2011
422
86
wana jamii nikianza kuwaza issue za ajira yaani nakosa raha kabisa hasa pale napoona vijana wamefaulu vizuri alafu bado wanasaga kisisgino na bahasha zao mikononi....mimi GPA yangu iko chini ya 3.0, natamani kuomba kazi ila nakata tamaa....sasa haya maisha mpaka lini? hali ni ngumu mtaani. Naomba ushauri wana jamii, nifanyeje?
 
Mkuu,
sio kila ajira inaangalia GPA..
Angalia fani yako inahitaji uwe na utaalamu upi, jaribu kuangalia ni skills gani zinahitajika, then angalia namna ya kujiendeleza na kufikia viwango vinavyohitajika kwenye soko la ajira.
 
Mkuu,
sio kila ajira inaangalia GPA..
Angalia fani yako inahitaji uwe na utaalamu upi, jaribu kuangalia ni skills gani zinahitajika, then angalia namna ya kujiendeleza na kufikia viwango vinavyohitajika kwenye soko la ajira.

well said i concour with u
 
GPA mwisho wake unaishia mlangoni unapotoka darasani, Kitaa hakina cha GPA. Peleka maombi utapata kazi. Gamba halimtupi msomi!
 
Watu wenye GPA kubwa wengine huwa hawawezi kazi, hawajui kujieleza. Jaribu bahati yako usiogope GPA.
Angalia ajira zilizopo sokoni hata kama sizo ulizosomea uombe ili kujitengenezea channels huko mbele.
Tafuta skills za ziada, waweza jifunza computer na lugha za kigeni.
Pia waweza kuomba sehemu kuvolunteer hiyo ni katika kujijengea mazingira mazuri ya kuja kuombea kazi pindi kipindi ulichoomba kuvolunteer kitakapoisha ingawa isikuwekee guarantee ya kuajiriwa.
Kila la heri. Nenda ofisi kwa ofisi. Ofisi zingine waweza kwenda kama visitor halaf next time ukadondosha barua yako.
Usiogope. Kuogopa ni kujirudisha nyuma.
 
Wengine wanafaulu vizuri mitihani ila hawajui kujieleza katika interview na wengine CV na cover letter mabomu tu.

Kama ulivyoelezwa hapo juu ni angalia na kila kazi unayoifatilia inakuwa na mambo yake tofauti najua wengi wakikosa kazi ya walichosomea wanaangalia hata kwingine

Cha muhimu pia soma sana mtandaoni google unachotaka kama interview prep do's and don't etc skills za kazi ... Na mengi zaidi chakachua utapata mengi utakayojifunza

Usiogope nakumbuka lecturer wangu mzungu nchini kwao alisemaga mnapoenda tafuta kazi ukituma CV 100 tegemea 3-5 ndio watakupa at least interview sasa natumaini unaelewa hapo na mie huwa nashauri watu kutokata tamaa na ninashukuru wengi niliwaambia ndugu zangu wa apply big jobs hapa TZ bila woga na ni mabosi.
Goodluck
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
elimu sio cheti its about competance and performance,hizo GPA SI UNAKUMBUKA PALE MDIGRII UDSM -MWENDO NI KUDESA,COPY MAJIBU YA JAMAA WA MIAKA YA NYUMA,SEMINA UNADANDIA KWA KUNDI LA VICHWA.MTIHANA MNAJIPANGA KICHWA NA ZUZU HAPO LAZIMA GPA JUU
KWA WADADA-BOYFRIEND NA1 KWA AJILI YA TEST-BOYFRIEND NA 2 TAKE HOME AND LIBRARY TEST. BOYFRIEND 3 SEMINA LEADER BOYFRIEND NA 4 LECTURER ,BOYFRIEND NO 5 MTOKO BOYFRIEND NO 6 MSOSI MABIBO HAPO GPA LAZIMA IWE JUU
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mbona unaogopa bure ndugu ...fanya reference ya raisi wako wa sasa GPA yake namna gani kisha anza kutuma applications kama chizi...
jiamini tu utapata kazi..
 
Mpendw, Usiogope! Usiogope hata maandiko matakatifu yanasema usiogope mara 360. Bora wewe unaogopa GPA kuna wenzio wana hali mbaya zaidi na wanahangaika bila wasiwasi wowote.Sasa mimi
huwa nawachekesha wenzangu wanaoogopa kutuma application wakiona kazi inahitaji lamda mastaz na yeye ana degree huwu haendelei hata kuisoma hata kama ni proffesional yake. mimi huwa naomba hata wangesema diploma, mastaz twende kaz. usiogope kukosa, ogopa kutothubutu kujaribu. siku moja mambo yatakuwa poaaaaaaaa.
 
mkuu kwanza pole na msongo huo wa jinsi ya kupata ajira.Lakini pili fahamu kuwa waajiri walio wengi hususani kwa kipindi hiki chenye utitiri wa vyuo vikuu hawaangalii suala la GPA.Kubwa linalowashuhulisha ni namna ulivyo andaa barua ya maombi,CV na kuzingatia masharti ya maombi.Baada ya hapo wataweka jalalani zisizokuwa na sifa kisha kuwaita kwenye usaili waliofaulu awamu ya kwanza.Mwisho mwenye uwezo mzuri wa kujiuza kwenye usaili atapewa ajira iwapo hakuna urasimu.Jiamini yeyeto anaweza bila GPA.
 
mie nafahamu GPA ni kama unataka kufundisha ndio mara nyingi wanaitizama hiyo lakini kazi kama kaziisiyo ya kufundisha aaaaaah hakuna kitu kama hicho
 
watu wana GPA za 3.8 hawana kazi hapo utasemaje? hakuna mambo ya kuangalia GPA's kazini
 
mambo ya GPA mtupie mukandara usoni hukohuko UD na wala usije nayo huku mtaani please!

mkuu, mimi kazi yangu ya kwanza kula mshahara niliapply kazi iliyokuwa ikitaka masters na mimi nikiwa ndo kwanza hata transcript ya ka-Bcom sijapata, nazurura tu kitaa nikiwa na statement of results! ka-bcom kwnyewe GPA japo haikuwa ya kichovu kiviiiiiiile, but haikuwa ya kutisha hata kidogo. nilinyaka job kama sina akili nzuri na nikaanza kula tumilioni tuchache hata ikafikia nikakataa kazi ya NMB headquarters! kufumba na kufumbua nilnyaka scholarship! hakuna mtu majuu anyeuliza GPA wala nini. upo hapo? we mwaga cv mtaani kama huna akili nzuri acha kutishiwa nyau ya GPA
 
mkuu GPA ya darasani na GPA za mtaani tofauti kabisa. GPA ya mtaani ni kujiamini kuwa unaweza, km umeanza kuwa na hofu ya kazi ni dhahiri hata GPA yako ya kitaa ipo below 2. embu pata taska bariiidi ili uipandishe kidogo. (nimeweka na utani kidogo, lakini usijali kazi utapata, JIAMINI kwanza.)
 
Back
Top Bottom