Nanyaro ateuliwa kuongoza CHADEMA Arusha mjini

Nanyaro ateuliwa kuongoza CHADEMA Arusha mjini

Hongera mkuu Nanyaro!!

Wapenda maendeleo hatupendi ubinafsi, chuki, kuficha ficha mambo yasiyokuwa na umuhimu wa kificha na kujifanya wewe kwa kuwa ni kiongozi basi uko juu ya sheria.

Tunapenda kuona ubunifu katika kuongoza chama, sehemu yako ya uongozi pamoja na kuwasaidia wananchi bila kuwabagua itikadi zao, kwani ukifanya hivyo utakuwa unaonyesha taswira halisi ya wafuasi wa chama (ambao wengi tuna moyo wa uzalendo), chama chetu chenyewe pamoja na kuwavutia zaidi watu waliochelewa kuungana nasi.
 
Mkuu

Hongera hakikisha unaendeleza ile dhana kwamba viongozi ni watumishi wa watu. Hivyo, maadili ya CDM yakuoongoze kila unalofikiria kufanya.
 
Kwa niaba yangu na ya lile kundi letu ninakupa PONGEZI nyingi sana kwa hatua hii!
Hii inathibitisha imani ya chama kwako!
 
Hongera sana Nanyaro, we keep you in our prayers kwa wajibu huo mpya....
 
Kwa niaba yangu na ya lile kundi letu ninakupa PONGEZI nyingi sana kwa hatua hii!
Hii inathibitisha imani ya chama kwako!

Habari yake binafsi kiongozi,

Niliwahi kuwasikia mara kadhaa wataalamu wa kiswahili toka bakita wanakuwepo redio one kila jumamosi wakisema kwamba, ukisema kwa niaba yangu inakuwa haijakaa kwenye mstari, itabidi niwatafute na bakiza kwa ufafanuzi zaidi.
 
Duuu!Huyu young kid si ndie aliwasaliti wenzake kwa kudai hakubaliani na muafaka huku alishiriki katika mchakato mzima.Bila shaka kunashinikizo la wakubwa CDM yeye kupewa nafasi hiyo.

Binafsi simkubali Nanyaro, kwangu mimi namuona kama mtu mwenye tamaa ya vingi despite of his age. Sidhani kama atawaweza wale "magwiji" ambao wamegoma kung'atuka otherwise wafukuzwe kwanza.
 
nakutakia kila la heri nanyaro, imani hujengwa moyoni na itumike kuonyesha matendo yako kwa nje. jenga chama na waunganishe na wanachama. vijana tupo nyuma yako!
 
Back
Top Bottom