Nani wameiba Sh480 bilioni Hazina?

Nani wameiba Sh480 bilioni Hazina?

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Tangu gazeti dada la The Citizen lichapishe mwishoni mwa wiki habari za upotevu wa Sh480 bilioni katika Wizara ya Fedha, Serikali imekaa kimya kama vile wizi huo ni tukio la kawaida, hivyo halihitaji maelezo ya kina wala ya haraka. Wananchi walitegemea kwamba Serikali ingetoa kauli haraka iwezekanavyo kuhusu mazingira ya upotevu huo na hatua inazochukua kuwawajibisha wahusika.

Tunasema kiasi hicho cha fedha zilizoibwa ni kikubwa kwa sababu ni zaidi ya bajeti ya mwaka kwa baadhi ya wizara, zikiwamo wizara kubwa kama ya Uchukuzi ambayo katika mwaka wa fedha wa 2013/14, kwa mfano ilitengewa Sh491 bilioni.

Tunaambiwa Sh480 bilioni zilizopotea katika Wizara ya Fedha zinaweza kujenga kilomita 375 za barabara kwa kiwango cha lami ikiwa ni urefu wa kutoka Dar es Salaam hadi Gairo, kilomita chache kutoka Dodoma. Tujiulize kiasi hicho cha fedha kingeweza kugharamia madawati, zahanati na madarasa mangapi kwa ajili ya wagonjwa na wanafunzi wetu.

Pamoja na ukimya wa Serikali kuhusu wizi huo, tumetiwa moyo na hatua ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), ambayo imemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuchunguza upotevu huo wa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kilitumika pasipo maelezo katika kipindi cha miaka miwili ya fedha cha 2012/13 na 2013/14.

Wasiwasi wa kamati hiyo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwapo kwa mtandao mkubwa wa wizi wa fedha za Serikali katika Wizara ya Fedha. Jambo hilo limethibitishwa na vitendo vya wizi wa kimtandao ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wake wakishirikiana na baadhi ya watendaji wa Tamisemi.

Ugumu uliopo hapa ni kwamba haijulikani kama fedha hizo zilizopotea zilitokana na kodi za wananchi au wafadhili ambao walichangia Sh842 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13. Ni sahihi kabisa kwa Kamati hiyo ya Bunge kushangazwa na kuendelea kuwapo kwa vitendo vya ufisadi serikalini, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba ripoti za CAG kila mwaka zimekuwa zikifichua wizi wa mabilioni ya fedha katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Kujirudia kwa vitendo hivyo kila mwaka ni ishara kwamba Serikali haina dhamira ya kupambana na vitendo hivyo.

Mwenendo huo wa Serikali unashangaza, hasa kutokana na ukweli kwamba mwaka 2013/14 ilikuwa na nakisi ya Sh847 bilioni katika bajeti yake. Hivyo, utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo ingekwama kama siyo kukopa mabilioni ya fedha kutoka vyanzo vya nje na ndani ya nchi.

Matokeo yake ni kuzidi kuongeza mzigo wa Deni la Taifa ambalo limefikia Sh27 trilioni sasa, huku ikishindwa kukusanya kodi na kupanua wigo wa vyanzo vya kodi. Ndiyo maana iko hoi kifedha na karibu shughuli zake zote zimesimama, huku ikisuasua kulipa mishahara ya watumishi wake.

Pamoja na hali hiyo mbaya kifedha, bado vitendo vya wizi na ufisadi serikalini vinaendelea kama tunavyoshuhudia vikishamiri katika Wizara ya Fedha. Ni jukumu la Serikali kudhibiti ubadhirifu na ufisadi miongoni mwa watumishi wake, vinginevyo uchumi wetu utazidi kudidimia. Kwa kuanzia iwasake na kuwawajibisha wote walioiba Sh480 bilioni kutoka Hazina.




MCL.
 
Kodi zetu zinafanyiwa watakavyo na si inavyostahili,,nakumbuka kale kawimbo..TANZANIA EEEH,NCHI YANGU EEEEH,...
 
Huu mzigo watu wa pale wakisaidiana na chama cha mafisadi
 
Hii ni zaidi ya zahama! Bilioni 480 wakati waalimu wanadai bilioni 50 hawajalipwa! Aibu kwa serikali ya ccm na mwenyekiti wake. Kwa hili utawakuta tuliowatuma bungeni wanachekacheka na kusinzia. Najiuliza hivi: kikwete hivi hili ndo lilikuwa lengo lako la kuomba kura zetu ukatuibie wewe na washirika wako kodi za wananchi? Mbona hamna huruma na kina mama wanateseka kwa kukosa huduma mahospitalini na watoto kukosa madawati na vitabu.
Za epa uliwasamehe, je hizi nazo utawaambia warudishe?
Unatupoteza na kutuibia badala ya kutuongoza. Nina hasira sana na ninyi 2015!
 
Aliyekabidhiwa kuzitunza fedha kazihamiisha toka mfuko wa koti na kuziweka kwenye sox
 
Waulize serikali yako tukutu ya ccm yaani hapa ndio napoumwa na kichwa nikianza kufikiria hii mijitu nimesma hivyo kwa sababu hawana maana hawa hawatutakii mema yaani mabilioni yoote hayo yanaibiwa bado meneja , secretary, wakurugenzi, na wawekaazina bado wapo tu hawajafungwa we mungu anipe uhai 2015 tutaonana.
 
Hadi kufikia Desemba, 2013, Deni la Taifa limefikia Dola za Marekani bilioni 17.10 sawa na shilingi trilioni 27.04 Kati ya kiasi hicho, Deni la Nje ni Dola za Marekani bilioni 12.79 sawa na shilingi trilioni 20.23 ambazo ni asilimia 74.81 ya Deni la Taifa. Aidha Deni la ndani ni shilingi trilioni 6.81 ambazo ni sawa na asilimia 25.19 ya Deni la Taifa . Kati ya Deni la Nje la Taifa, Dola za marekani bilioni 10.563 sawa na shilingi trilioni 16.71 ni deni la Serikali na Dola za Marekani bilioni 2.23 sawa na shilingi trilioni 3.52 ni Deni la Sekta Binafsi.

SOMA ZAIDI HAZINA
 
Ndio sababu wafanyabiashara wanagoma kulipa kodi kwani kodi zinazolipwa zinaingia mifukoni mwa wajanja wa ccm na serikali yao!!!
 
Watanzania for once ebu tuonyesheni uchungu
Si ajabu siku hizi habari kama hii kupata wachangajia 10 maana tushaifanya migumu nyoyo zetu na kufumbia macho ujambazi huu.
 
Nasema tukiendelea kucheka na hawa MaCCM hakya mungu ipo siku tutaambiwa tuhame nchi hii watu wameshanunua ardhi yote... Hapo ndipo tutajitambua!!!
 
Hadi kufikia Desemba, 2013, Deni la Taifa limefikia Dola za Marekani bilioni 17.10 sawa na shilingi trilioni 27.04 Kati ya kiasi hicho, Deni la Nje ni Dola za Marekani bilioni 12.79 sawa na shilingi trilioni 20.23 ambazo ni asilimia 74.81 ya Deni la Taifa. Aidha Deni la ndani ni shilingi trilioni 6.81 ambazo ni sawa na asilimia 25.19 ya Deni la Taifa . Kati ya Deni la Nje la Taifa, Dola za marekani bilioni 10.563 sawa na shilingi trilioni 16.71 ni deni la Serikali na Dola za Marekani bilioni 2.23 sawa na shilingi trilioni 3.52 ni Deni la Sekta Binafsi.

SOMA ZAIDI HAZINA

...tunaambiwa kuwa "Kila Mtanzania bila kujali kama ni mtoto, mzee au mfanyakazi anadaiwa Sh. 600,000/=" ...
 
Ndio sababu wafanyabiashara wanagoma kulipa kodi kwani kodi zinazolipwa zinaingia mifukoni mwa wajanja wa ccm na serikali yao!!!

Hata mie nishaanza kujisikia uvivu kulipa kodi
 
ha ha ha! Hii inchi watu wanajisevia tu. Wakishamaliza rasilimali zetu,tujiandae wataanza kuibiwa mtanzania mmoja baada ya mwingine
Tena itakua kampeni ya wizi wa nyumba hadi nyumba
 
Back
Top Bottom