Nani wameiba Sh480 bilioni Hazina?

Nani wameiba Sh480 bilioni Hazina?

nasema tukiendelea kucheka na hawa maccm hakya mungu ipo siku tutaambiwa tuhame nchi hii watu wameshanunua ardhi yote... Hapo ndipo tutajitambua!!!

ndg:wachina wamesha pandisha bendera yao mlima kilimanjaro, sasa tusubiri kuambiwa wakimbizi,nchi ishauzwa mkuu,ihi ndio ccm hai cheki na kima wako kikazi zaidi,
 
Duh kama ni kweli sasa hii ni balaaa, hii nchi ya aina gani ambayo mwizi wa Simu ya Mchina anachomwa moto na wananchi wenye hasira kali. Lakini mkwapuaji/wakwapuaji wa Bil 480 wanatanua kwenye ofisi za umaa full kiyoyozi. Nina amini Watanzania wengi hawajui/kuelewa maana ya wizi hususani kama huu wa kimtandao, wengi wetu mpaka wamuone mwizi live anakimbizwa.

Wito, tufahamishwe kwa uhakika watu waliokwapua pesa zetu ili tuwapigie yowe la mwizi wakati wanatoka ofisini. Najua Wananchi wenye hasira kali wakishasikia mwizi kitaa wao ni kupiga tu.
 
Inakera sana afu kuna mijitu inakuja hap bila aibu eti ccm inafaa kuongoza nchi ?si aibu hii jaman nchi jiran pia wantushanga tumelishwa nin ambacho tumeshindwa kugundua serikal ya chma hiki ovu
 
nasikia nazo zilihusika kwenye kifo cha mgimwa....alikuwa anazifuatilia ati...
 
Wenye chama chao na serikali yao huwaoni katika thread kama hizi. Siasa na ushabiki wa vyama umejenga "UNAFIKI" katika kuchangia masuala kama haya. Suala la wizi wa fedha ngazi ya serikali kuu hadi huko chini imekua utamaduni. CAG almost kila mwaka wa fedha ukaguzi unaibua same scandal ila hakuna hatua kali za kisheria kwa wahusika. I am not intending to persue wananchi kufikia hatua ya kupinga haya kwa fujo/maandamano but uvumilivu una kiwango chake. Nchi inazidi kutumbukia katika umaskini mkubwa,huku billions of shillings zaibwa. Siasa za CCM na CDM zinafanya zisitutenganishe kwenye inshu kama hizi.
 
Wanagawana pale Lumumba ofisi ndogo tu. Hizo sio za kupeleka ofisi kuu. Hakuna shaka yeyote Maccm wamegawana viwanja vya kupuria ngano. Kuna wenye masilaha mazito mzito wao wakaingia kuvuna faru na tembo, mkuu wa kaya kasema anawafahamu kwa majina na anwani zao hivyo wasithubutu kupiga panga mrejesho wao.
Kuna waliowekwa pale hazina, sasa kampeleka Mwingulu kusimamia zoezi kikamilifu, akisaidiwa na yule Bwana wa Madolas na mabunduki na mabastola aliyeibiwa na kimwana kaka Malima. Hao kazi yao ni moja tu, kulinda mrejesho huo wa hazina.
Yote tisa kumi bado, Umeme umepandishwa, Maswi anachekacheka pale bandarini, kuonesha mashine mpya kumbe zimepakwa rangi. Ongezeko lote la umeme ni kuhakikisha njuluku zinaokotwa kila kona. Wanajua 2015 ni ngumu kwa ccm kurudi lakini kama wataweza kugawa njuluku za kutosha kila mgombea akawa na kifuko chake chenye minoti, kwani hapo hakuna Taa kuu kuu wala Tisi, kwani hao kila mmoja atakuwa likizo. Ukichanganya tena na mkuu wa kaya katoa ruksa kuwatenda upendavyo wapinzani. 2015 Rais wa ccm, atapitishwa kwa kura laki moja tu. Nisameheni haya ni mawazo potofu tu. Sidhani kuna mtu mwenye moyo wa kuiba fedha nyingi hivyo. Utto arudie mahesabu
 
Be serious. Billions of shillings zaibwa.

Am serious na ndio maana nimeomba picha huenda tukalikamata lijamaa, u never know pengine tupo nalo kitaa hilo lijizi, sasa ukirusha ka picha faster tunalikamata
 
  • Thanks
Reactions: 911
Watanzania for once ebu tuonyesheni uchungu
Si ajabu siku hizi habari kama hii kupata wachangajia 10 maana tushaifanya migumu nyoyo zetu na kufumbia macho ujambazi huu.


Nimejaribu kukaa karibu au kwenye vijiwe mbalimbali nikagundua kuna tatizo miongoni mwa wananchi la kuelewa serikali ni nini. Kuna watu wengi tu wanajua serikali ni kitu tofauti na wananchi na hili tatizo linaongezwa na baadhi ya viongozi wa ccm wanapokwenda vijijini na kuwapa ahadi mfano; nitawajengea barabara, au ccm imewajengea daraja.
Kuna watu wanaamini kuwa daraja la rufiji limejengwa na mkapa. kwa maana kuwa ni kwa pesa zake.

Kwahiyo akili kama hizi ndio zinachangia kwa watanzania wengi tu hata wakiambiwa mabilioni yamepotea hazina wanakuwa haiwagusi sana maana hawaelewi kuwa hizo ni pesa zao.
 
nakuxhangaa xna Admin WATAMKAMATA NANI WAKATI PESA WAMEIBA WAO!...mfano upo ww, keo na mwanao chumbana alafu walet yako imepotea ghafla! utaenda kw jirani kumuulza nan amekuibia wkt wez unao ndan?...WATANZANIA tuamke 2015
 
nasikia nazo zilihusika kwenye kifo cha mgimwa....alikuwa anazifuatilia ati...
mhh...hata mm nilisikia hizo tetesi kuwa mh yule aligundua upotefu wa fedha pale hazina na baada ya kuwajua waliofanya uwizi huo wakamuwahi kabla hajawataja
 
Magazeti yanapaswa kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuja na habari kama hizi ama waandishi wanaoandika mambo kama haya wawe na uproffesional wa kitu wanchoandika. Huvi vitu vinakuwa hoja za wakaguzi sio maana yake pesa zimeibiwa inatokana na kuchelewa kupata au kutokuwepo hati za matumizi wakati wa ukaguzi kutokana na sababu mbalimbali. Mojawapo ni pesa zinzotoka mwisho wa mwaka wakati wa kufunga mahesabu. Na si kila hoja ya ukaguzi ni wizi. Hotokea mara nyingi matumizi kuthibitishwa baada ya nyaraka husika kupatikana.
 
Bilioni 480 ni pesa nyingi kuliko iliyotengwa kwa wizara ya Mifugo.....?????????? Chadema wameiona Hii ?
 
Nimejaribu kukaa karibu au kwenye vijiwe mbalimbali nikagundua kuna tatizo miongoni mwa wananchi la kuelewa serikali ni nini. Kuna watu wengi tu wanajua serikali ni kitu tofauti na wananchi na hili tatizo linaongezwa na baadhi ya viongozi wa ccm wanapokwenda vijijini na kuwapa ahadi mfano; nitawajengea barabara, au ccm imewajengea daraja.
Kuna watu wanaamini kuwa daraja la rufiji limejengwa na mkapa. kwa maana kuwa ni kwa pesa zake.

Kwahiyo akili kama hizi ndio zinachangia kwa watanzania wengi tu hata wakiambiwa mabilioni yamepotea hazina wanakuwa haiwagusi sana maana hawaelewi kuwa hizo ni pesa zao.

CCM wamedumaza akili za Watanzania. Nguvu kubwa inahitajika katika ukombozi wa fikra
 
mhh...hata mm nilisikia hizo tetesi kuwa mh yule aligundua upotefu wa fedha pale hazina na baada ya kuwajua waliofanya uwizi huo wakamuwahi kabla hajawataja

inawezekana kabsa. bse hata familia ya Dr mgimwa walikir waz kutojua chanzo cha hcho kifo......srkl yenye mchwa mkali na viongoz dhaifu kuwah kutokea nchin tutegemee danadana na kunyamaza kweny hli jambo
 
Back
Top Bottom