MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
Mwezi wa Saba Viongozi wa dini kutoka Norway, Canada, Botswana, Afrika Kusini na Zambia waliungana na wenzao wa Tanzania (TEC/BAKWATA/CCT) kutembelea wahanga wa uhalifu unaotendwa na wawekezaji kwa kuungwa mkono na serikali katika mgodi wa North Mara na Geita. Leo ninakumbushia tu stori ya watu wa Geita. Hii story haikuanza leo bali miaka kadhaa ilopita. Viongozi wa dini wameweza kuiweka ktk kumbukumbu na waweza kuisoma hapa na kuiona hapa.Usiku wa tarehe 31 July 2007 ni usiku wa kukumbukwa kwa wengi ktk kaya zaidi ya 80 za kijiji cha New Mine wilayani Geita. Walivamiwa usiku wa manane na polisi, wakafurushwa na kisha nyumba zao kuchomwa moto. Pamoja na kutafuta haki na kupewa mahakamani serikali yao imewaacha kuteseka kwenye mahema bila msaada!
Leo hii wako kwenye mahema kama vile hakuna serikali.
Hili ni jengo la mahakama ya ardhi ambapo familia 86 zilitupwa usiku wa 31/7/2007 bila kujali kuwa kuna wazee, watoto na wakwe zao.
Na haya ndo mahema wanayoishi kwa zaidi ya miaka 4. Mpaka sasa kuna watoto kadhaa wamezaliwa ktk mahema haya. Mmoja wa viongozi wa dini aliuliza: je kila familia inayoishi hapa ina redio? Ni swali la kijinga linaloonekana kana kwamba linawasimanga hawa watu lakini nikakumbuka stori ya wanaoishi maeneo ya mabanda (slums) huko nairobi kwamba: ili baba na mama wakutane kimwili husubiri treni inapopita hapo na fasta fasta baba humrukia mke na humaliza shida zao wakati treni inapita!!! Kwa hiyo kwa jinsi mahema yalivo
.unapata picha!!!!!!!!
Pata taswira
Vyoo wanavotumia ambavyo hawakupewa na serekali bali viongozi wa dini
Kwa sasa ziko familia chini ya 30. Usiniulize sasa hivi zile zingine zaidi ya 50 ziko wapi
lakini siku moja nitaibuka na jibu!