Nani wa kulaumiwa?

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,052
Mwezi wa Saba Viongozi wa dini kutoka Norway, Canada, Botswana, Afrika Kusini na Zambia waliungana na wenzao wa Tanzania (TEC/BAKWATA/CCT) kutembelea wahanga wa uhalifu unaotendwa na wawekezaji kwa kuungwa mkono na serikali katika mgodi wa North Mara na Geita. Leo ninakumbushia tu stori ya watu wa Geita. Hii story haikuanza leo bali miaka kadhaa ilopita. Viongozi wa dini wameweza kuiweka ktk kumbukumbu na waweza kuisoma hapa na kuiona hapa.
Usiku wa tarehe 31 July 2007 ni usiku wa kukumbukwa kwa wengi ktk kaya zaidi ya 80 za kijiji cha New Mine wilayani Geita. Walivamiwa usiku wa manane na polisi, wakafurushwa na kisha nyumba zao kuchomwa moto. Pamoja na kutafuta haki na kupewa mahakamani serikali yao imewaacha kuteseka kwenye mahema bila msaada!Leo hii wako kwenye mahema kama vile hakuna serikali.​

Hili ni jengo la mahakama ya ardhi ambapo familia 86 zilitupwa usiku wa 31/7/2007 bila kujali kuwa kuna wazee, watoto na wakwe zao.​
Na haya ndo mahema wanayoishi kwa zaidi ya miaka 4. Mpaka sasa kuna watoto kadhaa wamezaliwa ktk mahema haya. Mmoja wa viongozi wa dini aliuliza: je kila familia inayoishi hapa ina redio? Ni swali la kijinga linaloonekana kana kwamba linawasimanga hawa watu lakini nikakumbuka stori ya wanaoishi maeneo ya mabanda (slums) huko nairobi kwamba: ili baba na mama wakutane kimwili husubiri treni inapopita hapo na fasta fasta baba humrukia mke na humaliza shida zao wakati treni inapita!!! Kwa hiyo kwa jinsi mahema yalivo….unapata picha!!!!!!!!
Pata taswira
wlEmoticon-sadsmile%25255B2%25255D.png

Vyoo wanavotumia ambavyo hawakupewa na serekali bali viongozi wa dini​
Kwa sasa ziko familia chini ya 30. Usiniulize sasa hivi zile zingine zaidi ya 50 ziko wapi…lakini siku moja nitaibuka na jibu!​
 
Kijana huyu ni mmojawapo wa wahanga wa udhalimu wa wawekezaji.
Ana miaka 13, na hajawahi kuona darasa la pili. Alisoma darasa la kwanza na baada ya wazazi wake kufia kwenye ‘kambi ya wakimbizi wa ndani (Internally displaced persons-IDPs)' hapa Geita akalazimika kuacha shule ili kumtunza bibi/nyanya yake. Anatamani aanze shule hata kama ni chekechea
wlEmoticon-sadsmile%25255B2%25255D.png

Mpaka lini haya yataendelea?
 
Wenyeji wanayaita MAGWANGALA…masalia ya mawe toka mgodini (waste rock) yanayouzwa kwa kiroba sh 4000-5000. Kisha huletwa hapa Nyankumbu kwa ajili ya kupondwa, kusagwa na kisha kuoshwa na kupata dhahabu.
Wapondaji ni nani? Wengi ni akina mama na watoto! Ukitaka kujua ama kuona utumikishwaji wa watoto…njoo hapa utajionea.
Pata taswira
wlEmoticon-sadsmile%25255B2%25255D.png

Afya za wanawake, watoto na vijana zi mashakani!​Ukifika pahala hapa na ukasikia kelele za ‘krasha' hapo utadhani ni boeing inaondoka uwanjani!
wlEmoticon-sadsmile%25255B2%25255D.png
 
CCM ndio wa kulaumiwa, Wamesha uza nchi. Sasa Watanganyika ni watumwa katika ardhi yao.
 
Mwezi wa Saba Viongozi wa dini kutoka Norway, Canada, Botswana, Afrika Kusini na Zambia waliungana na wenzao wa Tanzania (TEC/BAKWATA/CCT) kutembelea wahanga wa uhalifu unaotendwa na wawekezaji kwa kuungwa mkono na serikali katika mgodi wa North Mara na Geita. Leo ninakumbushia tu stori ya watu wa Geita. Hii story haikuanza leo bali miaka kadhaa ilopita. Viongozi wa dini wameweza kuiweka ktk kumbukumbu na waweza kuisoma hapa na kuiona hapa.
Usiku wa tarehe 31 July 2007 ni usiku wa kukumbukwa kwa wengi ktk kaya zaidi ya 80 za kijiji cha New Mine wilayani Geita. Walivamiwa usiku wa manane na polisi, wakafurushwa na kisha nyumba zao kuchomwa moto. Pamoja na kutafuta haki na kupewa mahakamani serikali yao imewaacha kuteseka kwenye mahema bila msaada!Leo hii wako kwenye mahema kama vile hakuna serikali.​

Hili ni jengo la mahakama ya ardhi ambapo familia 86 zilitupwa usiku wa 31/7/2007 bila kujali kuwa kuna wazee, watoto na wakwe zao.​
Na haya ndo mahema wanayoishi kwa zaidi ya miaka 4. Mpaka sasa kuna watoto kadhaa wamezaliwa ktk mahema haya. Mmoja wa viongozi wa dini aliuliza: je kila familia inayoishi hapa ina redio? Ni swali la kijinga linaloonekana kana kwamba linawasimanga hawa watu lakini nikakumbuka stori ya wanaoishi maeneo ya mabanda (slums) huko nairobi kwamba: ili baba na mama wakutane kimwili husubiri treni inapopita hapo na fasta fasta baba humrukia mke na humaliza shida zao wakati treni inapita!!! Kwa hiyo kwa jinsi mahema yalivo….unapata picha!!!!!!!!
Pata taswira
wlEmoticon-sadsmile%255B2%255D.png

Vyoo wanavotumia ambavyo hawakupewa na serekali bali viongozi wa dini​
Kwa sasa ziko familia chini ya 30. Usiniulize sasa hivi zile zingine zaidi ya 50 ziko wapi…lakini siku moja nitaibuka na jibu!​

Watu wa Igunga wana saa 24 za kupima IQ zao.
 
Very sad news very sad pictures I have never seen them before hakika hii ni Tanzania pia ?
 
Mapicha hayo wanatumia sana NGO na makanisa kuombea msaada kwa wafadhili unaweza ukawapa
 
Very sad news very sad pictures I have never seen them before hakika hii ni Tanzania pia ?

Nenda kwenye machimbo ya mbuguni (arusha) hali iko hivyo hivyo..unaweza kuchukua hizi picha kuombea msaada (NGO na Makanisa mengi) yanafanya hivyo
 
Inaniumiza sana basi tu,ombeni na msaada wa silaha tupambane na hawa wanaotufanya watumwa kwenye nchi ye2,unajua bora ufe ukipambana kuliko kuish maisha yote ukiwa hivyo.Hivi hakuna mtu wa kuanzisha tuje hata bila malipo?
 
Dah....hivi ni kweli watanzania tumekubali kuwa watumwa ktk ardhi yetu kiasi hiki?? It hurts
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom