Kupotoka kwa maadili Serikali inastahili kulaumiwa

Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
783
525
Kupotoka kwa maadili mara nyingi lawama wanatupiwa wazazi na utandawazi, lakini ebu tuangalie wajibu wa serilkali kwa maana ya mhimili wa utawala wenye mamlaka ya kusema hii sawa na hii hapana.

Majuzi nilikuwa naangalia kipindi cha mkutano wa wadau wa madini kilichofanyika Geita ilinipa kutafakari, serikali inatumia pesa za walipa kodi kumualika zuchu kuja Geita kuimba wimbo wa honey ambao maudhui yake wala hayafanani na mkutano huo, hauna maadili kwa mashairi yake na sisi tunaona sawa tu.

Zamani wimbo haukutolewa hadharani mpaka upitiwe kwanza, leo wizara inaachia vitu hovyohovyo ati ni utandawazi mimi nadhani tumefika mbali Serikali muhimu sana iweke barn ya baadhi vitu tulivyo copy bila kuangalia madhara yake.

inapofikia Nchi nyingine hata kufikia kufunga baadhi ya mitandao sisi tunangoja nini mbona tumekimbilia kumsaka aliyetoa wimbo wa 'kama Nyani tu' au kwa kuwa unawasema viongozi?

Tumpe nguvu waziri Gwajima Taifa linaishia tusipo weka mikakati ya maksudi.

Napendekeza tukome kabisa kualika kwenye mikutano tena yenye wadau wa nje kuonesha wanengua viuno wakati tunahamasisha utalii wa utamaduni na tunaweza kuweka ngoma zetu.
 
Una hoja usikilizwe.
Na kama zuchu anaalikwa basi akaimbe wimbo ambao una maana kwa event yenyewe ilivyo. Iwe kiheshima zaidi..
 
Majuzi nilikuwa naangalia kipindi cha mkutano wa wadau wa madini kilichofanyika Geita ilinipa kutafakari, serikali inatumia pesa za walipa kodi kumualika zuchu kuja Geita kuimba wimbo wa honey ambao maudhui yake wala hayafanani na mkutano huo, hauna maadili kwa mashairi yake na sisi tunaona sawa tu,
Mkuu unashangaa nini hawa ndio CCM walioshindwa kila eneo!
 
Back
Top Bottom