Nani mwenye mamlaka ya kuruhusu mikutano ya siasa?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Ndugu zangu naomba tujadili swala hili kwa hekima na ustarabu mkubwa na tutangulize utaifa wetu kuliko kutanguliza vyama vyetu

Nani mwenye mamlaka ya kuruhusu mikutano ya kisiasa kufanyika nchini? je ni

1-Katiba ya nchi

2-Polisi

3-Msajili wa vyama vya siasa

4-Vyama vyenyewe

Mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru

Nchi huongozwa na utawala wa sheria.Kinachoruhusu mikutano ya siasa ni sheria zilizopo.Unatakiwa kupitia sheria zote zinazohusu maswala ya mikutano au mikusanyiko.Humo utazikuta sheria za msajili wa vyama,za polisi,za usalama wa taifa,za jinai nk
 
Unachotakiwa kuzingatia si katiba tu inabidi uzingatie na sheria zilizotungwa kutokana na katiba husika
Katiba haifafanui sheria hueleza kujumla jumla kwa mfano ina sema una uhuru wa kwenda popote lakini huwezi mkristo kwenda msikitini na viatu ukasema katiba inaniruhusu kwenda popote niko katika kutimiza uhuru wangu wa kikatiba!!!!

Kinachoruhusu ni sheria
 
Nchi huongozwa na utawala wa sheria.Kinachoruhusu mikutano ya siasa ni sheria zilizopo.Unatakiwa kupitia sheria zote zinazohusu maswala ya mikutano au mikusanyiko.Humo utazikuta sheria za msajili wa vyama,za polisi,za usalama wa taifa,za jinai nk
Sheria zikigongana automatically tunafuata KATIBA inasema nn
Katiba HAIJAIPA serikali wala polisi kuruhusu mikutano ya hadhara!Vyama vya siasa vinatakiwa tu viitarifu polisi kuwa vinafanya mikutano siku fulani na saa fulani!Kujulisha huko kusiwe chini ya masa 48 kabla hamja anza mkutano wenu

Anacho fanya DIKTETA UCHWARA kujipa yy nafasi ya kufanya mikutano lkn kuzuia upinzani kwa kutumia polisi ni up u u zi sana
 
Hizo sheria zipo juu ya katiba ambayo ni sheria mama?

Sheria mama inaeleza jumla ufafanuzikwa kila kipengele uko kwenye sheria.Mfano kipengele kinasema una uhuru wa kutoa mawazo yako.Lakini hata ukienda marekani huwezi andika gazetini au ukaenda kituo cha televisheni ukasema OSAMA BIN LADEN alikuwa mtu mzuri sana tena sana.Ni uhuru wako kusema lakini kuna sheria za kukubana
 
Katiba HAIJAIPA serikali wala polisi kuruhusu mikutano ya hadhara!Vyama vya siasa vinatakiwa tu viitarifu polisi kuwa vinafanya mikutano siku fulani na saa fulani!Kujulisha huko kusiwe chini ya masa 48 kabla hamja anza mkutano wenu

Polisi kazi yao sio kusimamia maslahi ya vyama vya siasa tu na ya watu wengine pia.Kwa mfano unataka kufanya maandamano, hayo maandamano yako koko hayatapitia angani yatapita barabarani kwenye barabara ambako watumiaji ni wengi.Watu wanapatia riziki zao kupitia hizo barabara lazima wapime kuhakikisha shughuli za kiuchumi za watu hazisimami kisa kupisha maandamano koko ya wanywa viroba wasiokuwa na kazi ya kufanya zaidi ya kuzurura mabarabarani.Tunaposema Polisi kuruhusu ni kuwa lazima wajihakikishie kuwa hayataleta usumbufu kwa wengine wasiohusika uwe usumbufu wa kiuchumi,kiusalama nk
 
Mbona hujadili mada kama nilivyoelekeza nimeuliza ni nani mwenye mamlaka ya kuruhusu mikutano ya siasa? halafu tuweke utaifa mbele hayo mengine koko, viroba yanatoka wapi?
 
Mkuu msamehe tu mana wengine wamekunywa maji ya bendera hata useme nini ni bure tu.
 
Back
Top Bottom