BabM
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 1,166
- 956
Nimekuwa najiuliza kwa miaka sasa kuhusu mkasa huu nilioushuhudia sipati jibu.
Kuna la kujifunza hapa. Ni hivi:
Jirani yetu alifariki. Alikuwa ameoa na watoto watatu wakubwa tu mmoja tukisoma naye. Hata hivyo marehemu alikuwa na michepuko kadhaa maana mtoto mmoja wa mchepuko tulikuwa pia tukisoma darasa moja na mtoto wa ndoa wakitumia ubini mmoja.
Wakati huo marehemu alikuwa na mchepuko mwingine. Kutokana na mambo ya michepuko marehemu alikosana na mkewe na akawa anaishi mwenyewe akamwachia mke nyumba nzuri na watoto. İlikuwa ni ndoa ya kanisani. Marehemu akaugua na kulazwa kcmc. hali ikawa mbaya na ndugu wakataka kumpeleka nairobi. hata hivyo marehemu kama alishajua kwamba atakufa hivyo kabla ya kuondoka akaomba mkewe aende hospitali ili akamuombe msamaha. mke bado alikuwa na hasira na akagoma.
Marehemu akajaribu kwa ushawishi wote lkn haikuwezekana. wakiwa kwenye mchakato wa kwenda nairobi akakata roho. yakasemwa mengi. kwenye msiba akaja askofu jimbo kwani jamaa alikuwa maarufu kwenye nyumba za ibada kutokana na kuwa mfanya biashara. kama kawaida kabla ya kuanza ibada ya kumuombea marehemu akasema mke wa marehemu asogee mbele ili ibada ianze. ikumbukwe kuwa msiba haukuwa kwenye nyumba yake alokuwa anaishi na mkewe bali kwenye nyumba yake ambayo alikuwa amejenga na kuweka wapangaji. Ndugu walikuwa wamefura na mke wa marehemu hawakutaka hata kumsikia.
Baada ya askofu kumwita ndugu wakaanza kupiga kele kupinga jambo hilo wakitaka azikwe kama msela. askofu hakukubali yakapita mabishano na hatimaye askofu akase mmsimamo ni mkewe ashiriki kwani ndoa haikuvunjwa vinginevyo ataondoka. ndugu wakawa wanamzomea na hivyo akasimama na kuondoka na mke wa marehemu akimfuata kwa karibu ambapo askofu alifanya kazi kubwa ya kuzuia asipigwe.
Wakaingia kwenye gari na kuondoka. Ndugu wakaleta padri kutoka sehemu nyingine na ibada zikafanyika kama kawaida. Ndio huwa najiuliza ni nani mkosaji mkuu hapa.