Nani mkubwa kati ya Mkurugenzi wa TISS na IGP?

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,553
Reaction score
57,843
Nauliza tu maana kiutendaji Mkurugenzi wa TISS anampa maagizo mengi IGP kuliko IGP anavyompa maagizo Mkurugenzi wa TISS.

Inakuwaje mtu katika utambulisho anatangulia kutambulishwa IGP?

Huu ni ubovu wa katiba au Kuna changamoto juu ya uanzishwaji wa TISS ?

Wanasheria nielewesheni!!
 
Mkuu wa jeshi la Polisi ni mtekelezaji wa sheria za nchi! Law enforcement unit is second largest unit in a country baada ya Jeshi! Huyo Mombo hawezi mpa maagizo IGP na anaongoza idara ambayo mkuu wake ni Rais!
 
Nauliza tu maana kiutendaji Mkurugenzi wa TISS anampa maagizo mengi IGP kuliko IGP anavyompa maagizo Mkurugenzi wa TISS.

Inakuwaje mtu katika utambulisho anatangulia kutambulishwa IGP?

Huu ni ubovu wa katiba au Kuna changamoto juu ya uanzishwaji wa TISS ?

Wanasheria nielewesheni!!
We fanya mambo yako huna unachojua.
 
DGTIS hawezi kumpa maelekezo IGP , kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama Ki seniority akitoka mkuu wa majeshi CDF anaefata ni IGP kwahiyo IGP ni mkubwa kwa DGTIS, hata kwenye vikao vya Rais huwa wanajipanga ki seniority akitoka CDF anafata IGP.

Isipokua kazi ya TIS ni kutafuta taarifa kiutaratibu hawaruhusiwi kukamata ukamataji wowote wanaoufanya ni kinyume na sheria , kwahiyo baada ya kutafuta taarifa ndo zinatolewa kwenye vyombo vingine vya ulinzi ili zifanyiwe kazi ikiwepo kukamata ikiwa itahitajika, kwahiyo DGTIS hamna namna anaweza kumpa maelekezo IGP, yeye atapeleka taarifa kwa Rais , alafu Rais ndo ataangalia hayo maelekezo ayashushe kwa mkuu yupi wa vyombo vya usalama kama CDF, IGP au CGP
 
Nauliza tu maana kiutendaji Mkurugenzi wa TISS anampa maagizo mengi IGP kuliko IGP anavyompa maagizo Mkurugenzi wa TISS.

Inakuwaje mtu katika utambulisho anatangulia kutambulishwa IGP?

Huu ni ubovu wa katiba au Kuna changamoto juu ya uanzishwaji wa TISS ?

Wanasheria nielewesheni!!
Kwenye hierachy ya vyombo kwa nchi yetu TISS inafuata baada ya Polisi. Mkurugenzi wa hiyo idara ni equivalent na CP wa Polisi.
Ndiyo maana CP wa Polisi Diwani Athumani aliwahi kuwa Mkurugenzi wa hiyo idara.
Wakuu wengi wa vyombo ukiondoa TPDF level zao ni sawa na Commissioners of Police (CP's) rejea CP Andengenye ambaye alienda kuwa CGF Jeshi la Zimamoto na uokoaji, CP Hamduni ambaye alienda kuwa Mkurungenzi wa PCCB.
 
Wote ni wakuu wa taasisi. Wana hadhi sawa. Sidhani kama ni kweli DGIS 'anampa maagizo' IGP.

Kuna taratibu rasmi za mawasiliano na namna ya kupeana ushirikiano. Unapotakiwa kutoa ushirikiano kwa mujibu wa sheria haimaanishi huyo unayempa ushirikiano no 'mkubwa'.

RPC anaweza 'kutakiwa' kwa mujibu wa taratibu ampe ushirikiano afisa mdogo kabisa wa taasisi nyingine ya serikali na akafanya hivyo. Hilo halimfanyi afisa huyo mdogo kuwa 'mkubwa'.
 
Nauliza tu maana kiutendaji Mkurugenzi wa TISS anampa maagizo mengi IGP kuliko IGP anavyompa maagizo Mkurugenzi wa TISS.

Inakuwaje mtu katika utambulisho anatangulia kutambulishwa IGP?

Huu ni ubovu wa katiba au Kuna changamoto juu ya uanzishwaji wa TISS ?

Wanasheria nielewesheni!!
Itifaki imezingatiwa.
 
Back
Top Bottom