Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Leo ndio lile jina la mtu ambalo Kikwete anapendekeza awe Waziri Mkuu litawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge. Je? Ni nani ataweza kufanikiwa kunyakua nafasi hii nyeti serikalini?


Mizengo Kayanza Peter Pinda
 
Leo ndio lile jina la mtu ambalo Kikwete anapendekeza awe Waziri Mkuu litawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge. Je? Ni nani ataweza kufanikiwa kunyakua nafasi hii nyeti serikalini?
mpwa na SI-HASA wapi na wapi bana weeeee!.......
hebu diliti thread yako ya ''kinoko''
 
Zawadi ya Eid Al- Adha: Edward Lowasa...kuhani mkuu wa maf.....

Unajua tena hili gari lilipata ajali ya kisiasa. Na sasa ni wakati wa kuonyesha kuna kupanda na kushuka na kupanda!
 
hata prof hawezi kuwa waziri mkuu coz hajawahi kuwa waziri sifa za kuwa waziri mkuu lazima uwe hata naibu huko nyuma na pili uwe umechaguliwa na wananchi wa jimbo fulani pinda sifa zote anazo pro anayo moja tu pole kaka angalia kabla ya kupost kama hujui kaa kimya.......
 
jamani kuwa waziri mkuu lazima uwe katika wakati umeshawahi kuwa hata naibu waziri pili lazima uwe mbunge wa jimbo so pinda ana sifa zote mbili ila prof ana moja sooo tibaijuka hawezi kuwa waziri mkuu k kwa wakati huu haiwezekani .....
 
Pinda ni kweli anafaa, tatizo kubwa yeye ni mtaalamu wa kujibu maswali bungeni, kuchair vikao, kuzima vuguvugu kitaalamu bila mtu kujua kama kuna suluhisho au hakuna, mfano Richmond, leo hii nikikuuliza hata yale mambo serikali iliyoambiwa ishughulikie we unajua yamefikia wapi? Pia ni mwadilifu

Inapokuja utendaje wa nje wa hayo niliyotaja hapo jamaa hayupo kabisa, mpole mno. Lowasa ni mfuatiliaji mzuri ila tatizo lake uadilifu.

Dr Magufuli yeye yuko kote kote, uadilifu, kupangua hoja kwa mifano na live data, na pia ni mfuatiliaji wa mambo. Pia hana jazba ya kugombeza watu hadharani. Tukitaka TZ isonge mbele kote kote, DR MAGUFU ni mtu sahihi kwa sasa. Ila kama tunataka mtu wa kupangua hoja na kujibu maswali vizuri bungeni Pinda ni mtu sahihi kwa sasa.

Ila ujue wananchi wanataka zaidi ya hapo, kuona miradi ya serikali ikikamilika kwa wakati na pia kua na value of maney. Magufuli alipokua Ujenzi, ardi, Uvuvi na Mifugo, amefanya kazi zinazoonekana.

Hii kazi mpeni Dr Magufuli, CCM itarudi 2015 bila kuweka mabango kama mwaka huu. Ila wakimwachia huyu aliyetoka theni wajiandae kuongeza budget ya mabango ya kampeni mara 4 zaidi ifikapo 2015.

Dr Magufuli sii mchezo, Jamaa alikua anafuatilia barabara, ujenzi umefikia wapi, ameziweka kichwani, anatoa tathmini zitaisha lini, wakandarasi wazembe walipigwa chini, Samaki alikua anadeal nao mpaka watu wakazika nyavu haramu wakaweka na misalaba ukidhani marehemu kumbe nyavu za kuvulia samaki. Alishawahi kukamata magari mengi ya serikali yanayofanya shuguli binafsi, anapangua hoja kwa hoja.

Pia jamaa kasomea Sayansi, na unavyojua science haihitaji longolongo ni facts tu, kwenye science hamna uongo kabisa.

Mpeni Dr Magufuli muone, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa wilaya+Mikoa wataacha kunukia Perfume/Marashi na watachapa kazi, then wananchi nao watachapa kazi

Huyu jamaa Dr Magufu, ni mtaalamu sana, alipopewa wizara ya Ardi, cha kwanza alichokifanya alienda darasani zaidi ya miezi 3 kusoma seria za ardi na mabaraza ja miji/vijiji. Alipoanza kazi ardi palianza kua pasafi, sasa sijui aligusa maslahi ya wakubwa akuchukua muda pale akapelekwa Mifugo na Uvuvi, nako huko akafanya mambo, meli ilikamatwa hana utani na haina maana zilikua haziibi samaki ili waliokuwepo walikua hawafuatilii

Ila SISIEMU tunawajua, watafanya kituko, tusubiri.
 
mpwa na SI-HASA wapi na wapi bana weeeee!.......
hebu diliti thread yako ya ''kinoko''
Leo cjui kaamkia Airport huyu.....
Back to topic.....kwa CCM lolote lawezekana siwezi kua shehe yahya:israel:
 
Ila hilo la Membe limekuwa rumored kwa muda sasa.. lakini itakuwa ni kutangaza mgongano wa kudumu na watu wa EL kitu ambacho sidhani kama ni maslahi ya JK baada ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi. Naamini kama siyo Pinda basi hawezi kuwa EL wala mtu yeyote ambaye alikuwa wazi katika kambi zile. Hivyo atakuwa mtu ambaye alikuwa yuko neutral sana Magufuli is one, na Mwandosya is the other.
 
mwaka huu tutaona threads za aina hii nyingi sana..... Sometimes I tend to think kuna watu wanajikuta wanaandika upuuzi bila kujua kwamba ni upuuzi!!

Prof. Tibaijuka nae alipita bila kupingwa sasa utakujaje hapa bila kufanya hata homewrok ndogo kujua Tibaijuka alikuwaje mbunge? Instead unaleta speculations tu za kipuuzi hapa JF??
Mbona unaidhalilisha hii FORUM we mwanzisha mada?

CRAP..... CRAPPIER.....CRAPPIEST... Damn!!
 
Kuhusu Prof. Tibaijuka, ndiye mbunge mwenye the highest profile.

Hawa wasomi wetu wanaganga njaa tu. Huyu mama kwa level na exposure aliyonayo sikumtegemea kwamba angekuja kugombea ubunge ili angalau apate nafasi kwenye ufalme wa JK (apewe uwaziri). Hii yote inaelezea vacuum iliyopo kwa wanazuoni wetu. Si wabunifu na kazi pekee wanayoiona ya kuwaingizia kipato kirahisi ni ya kuingia kwenye siasa.

This is too low, angeweza kuanzisha taasisi ambayo ingewasaidia watanzania kuondokana na makazi duni na kuwapa elimu ya kujitegemea.

Mbaya zaidi ameingia kwenye chama kile kile cha 'business as usual' CCM!!

Binafsi namwona anafanana kwa kila kitu na kina Getrude Mongella, Mch. Lwakatare, Margareth Sitta, Batilda Buriani, Salma Kikwete, Vicky Kamata, Nakaaya Sumari, Sophia Simba, na waganga njaa wengine wengi. Sioni mwenye majibu sahihi na mbinu za kisayansi za kuwakomboa watanzania kutoka kwenye lindi la umasikini!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom