Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
@ MTU MMOJA.., Huna lolote wewe....! utakua tu na hisa richmonduli au wazee wa jembe na nyundo..! unmfananisha 6 na matoto ya njiwa..! its like comparing a lion and a cat! huyo bibi akiwa spika ndo kabisaa ataliuwa bunge, litarudi enzi ya nchinga sound. sisiem katika hizo three names walizopropose hamna anaefaa kuwa spika katika bunge hili jipya la more speed and more stundards so the only choice ni MARANDO..
 
Duru ndo hizo sasa,tusubiri tu baada ya kukosa Uspika SS ndo anaenda kwenye UPM.
Ni ndoto nzuri sana kuiota, INAPENDEZA na INALETA LADHA masikioni Kusikia hivyo! kwa maana ana maamuzi yule mzee wa G....:israel:
 
Sitta alifanikiwa sana toka mwanzo alikuja kuvuruga tu kwenye kukamilisha ishu ya richmond...........pale alionesha kuwa ni mtu asiye na msimamo lakini ile kusema ukweli alifanya kazi nzuri sana na anafaa kuwa waziri mkuu.................alikula ng'ombe mzima alafu akashindwa kumalizia mkia wa richmond kwa style ambayo ingempa heshima kubwa sana kwa wtz japo asingepata heshima ileile kutoka kwa wana ccm mafisadi..........
 
:A S-cry:Kaka 6 kama hajui ndiyo amekwisha hivyo,kama hajui asubiri mapigo ya ngoma sijui ataingia kucheza!waswahili wanasema ukiona mwenzako ananyolewa we tia maji,Shibuda Mhe. aliweza kabisa kulijua hilo ndiyo sasa anafurahia uhuru wake kisiasa.Mapigo yanayofuta siamini kama miaka 5 atavumilia,system ilishamgeuzia kibao nampa pole in advance.:tape:
 

hongera mkuu kwa kuuona ukweli, kuna watu humu wameamua kwa hiyari zao wenyewe kuwa majuha na kujilisha upepo!! eti 6 kuwa PM, mara marando kuwa spika!!. kama si upepo huo wanaokula ni nini?
 
Sitta kupewa uwaziri mkuu ni ndoto. Hilo haliwezekani! Sitta si mwana mtandao tena, aliusaliti mtandao pale aliposababisha kubwagwa kwa EL. Hata kama JK alihusika vile vile kwenye ile move (naye aliona EL anakuwa threat kwake), lazima JK ajidistance na Sitta kwa sasa. Politburo ya CCM (kamati kuu) haiwezi kamwe kumpitisha Sitta kuwa waziri mkuu. Anaweza akapewa consolation post kama ya ubalozi na vyeo vinavyofanana na hivyo, ila u-PM hata uwaziri katika serikali inayokuja hawezi kuugusa.

Mtandao uko back in action na one of them lazima awekwe mahali ambapo atakuwa na uwezo wa kujijenga. U PM ni post inayomuwezesha mtu kujiuza sana, hawezi kupewa mtu ambaye chama kimeshamtishia kumnyang'anya uanachama. Hilo halipo. Besides, kamati ya maadili ya CCM inayoongozwa na Chenge ni lazima imkubali mtu wa kuwa waziri mkuu. Kikwete hawezi ku-afford kuwakera tena allies wake, ukizingatia miaka mitano ijayo ni ya kujenga alliances za kumlinda atakapostaafu. Hana uwezo wa kufanya maamuzi yasiyokwenda na wale waliomuweka madarakani wanavyotaka.

Pinda kurudi inawezekana. Historia inaonesha kuwa mtu pekee aliyekwishashika vyeo hivyo viwili (waziri mkuu na rais) ni mwalimu peke yake. Hivyo wataalam wa 'power struggles and intrigues' katika rulling party wanajua kuwa waziri mkuu hana nafasi rahisi ya kuupata urais. Kwa hiyo wanaweza kuendelea kumwachia pinda kama compromise figure ambaye atakuwa dumped pale atakapokuwa hahitajiki tena.

EL anaweza kurudi ndani ya Govt. kwa style, kwa sababu bado ana hamu na 2015. Hiyo ndo analysis yangu.
 

Tukumbuke pia ccm nako si shwari wana hasira na machungu tangu kura za maoni walitendeana visivyo na wameiona chachu ya ufisadi inawezekana wakampinga mbunge wa ccm wakamuunga mkono marando.
 


Hapo kwenye bold nadhani ndicho kinachowatokea! Tusubiri tuone laana hii itaishia wapi
 
Kwanini ushauri huu ukuwapa CCM mapema labda wangechukulia mawazo yako seriously!!!. Hata hivyo nina wasiwasi na motive behind your comments. Kwa wapenda maendeleo wa nchi yetu, Mzee Sitta alifanya makubwa kwani bila yeye kashfa za Richmond na EPA zingebaki kusemwa kichini chini na hatua yoyote isingechukuliwa. Sitta anachukiwa tu na mafisadi kwani alitoa nafasi kwa wapinzani kuhanika uovu wao. Je na wewe ni mmoja wao? Nimeuliza tu!!!!

Tiba
 
Sita hawezi kupewa u PM, JK alishaamua ni nani. Pinda inasemekana hataki kuendelea na U PM. Hizi ni speculations tu, tusubirie
 
Ama kweli wewe hujui siasa zinavyokwenda, 6 ndo kushey, watu wanajipanga for 2015

Na huo ndio ukweli wenyewe.

Haya yaliyotokea sio surprise hata kidogo. Namshangaa 6 alipaswa kujua majaliwa ya nafasi yake hata kabla ya uchaguzi. Ameshikwa pabaya, miaka 5 ya bunge kwake itakuwa kama miaka 10.
 
mh watakuwa wamelisha sumu ili waweze kumtuliza vizuri nini...hapo akipata atajisahauu na maneno aliyokuwa anajifanya kuyapinga na kuyapigania yatapotelea hewani

Great Thinker and that identity !!! I doubt. Ni mtizamo tu wakuu.
 
Kwanza tunadhani Sitta ni safi kiasi hicho kukemea ufisadi?

Kama Sitta ni clean alikwenda kujenga zile office kule kwao za nini? Jee alijua kwamba atakuwa madarakani kwa muda gani? Na ni wazi kabisa 2015 Sitta alikuwa anajipanga kuja kulianzisha kwenye sakata la Uraisi, lakini wakubwa wameona Mbali hivyo wamemtoa Kafara kwenye ziwa Tanganyika.

Politics ya CCM ni rahisi sana kuisoma, ndio maana sielewi how wanaweza kurudi 2015. Chama kiko kwenye political bankrupcy, hakina new ideas, wala new leaders. Ni wale wale wazee ambao wameifikisha Tanzania hapa ilipo leo, failed policies and poor theories.
 
Sam six anaweza kuwa waziri wa mambo ya ndani ama naibu waziri mkuu.taarifa nilizonazo ni kwamba leo amekua na kikao kizito na mkwere akijaribu kumshawishi sam 6 akubali moja kati ya hizo chances japo sam amekua akisita na kutishia kutimkia chadema,anaona bora awe kwenye benchi la upinzani kuliko kukalia tena benchi la ccm,pia kumekua na presha toka kwa wapambanaji wa ufisadi ndani ya ccm wakiongozwa na dr.mwakyembe kumtaka sam 6 asikubali kuhongwa vyeo hivyo kulinda heshma yake,ni suala la kusubiri na kuona nini kitajiri.

Mwisho wa kuwasilisha.
 
Speculations zingine ni kuwa kuingia kwa Chenge kwenye kugombea uspika ilikuwa kama blackmail kwa JK baada ya kuonekana msimamo wake kuhusu six haueleweki (kama ilivyo kawaida yake). Sasa kundi (Mtandao mamboleo) lilishaona kuna uwezekano wa six ku-hang on kama speaker kwa hiyo wakaamua kumchomekea Andrew kwenye sakati ili kutoa statement kwa JK kwamba wako in business na six hawamtaki. JK kama ilivyo kawaida yake hataki aonekane yuko upande upi kwa hiyo compromise ikawa ni kum-dump six. Let's wait and see, lakini suala la six kupewa U-PM itakuwa ni direct slap kwenye face ya mtandao mamboleo. JK hawezi ku-afford kitu hicho asilani. Hivyo six may end-up kuambulia ka-consolation post ambako ni kadogo kuliko uwaziri! Hata uwaziri six hawezi kutia mguu kwani wapinzani wake ni wengi kuliko waungaji mkono. Wanaomuunga mkono wengi ni powerless!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…