Nani keshapata? toa ushuhuda

dazu

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
365
76
Wanadamu tumekua wepesi kuomba, lakini wazito kushukuru. Napendekeza kwa wale ambao wameshafanikiwa kupata wachumba/wake/waume kupitia safu hii ni vyema wakarejea na kutoa shukrani zao ili na wengine wanaondelea kutafuta wapate moyo kwamba mambo haya yanawezekana na vilevile kuonesha moyo wa shukrani, sio kila siku kuomba tu.

Au mnaonaje waungwana?
 
mimi nilipata na nilikuja kushukuru.....na tupo pamoja hapahapa tunaliendeleza libeneke......ungependa kumjua.....?
 
Mimi nlimpata wa kwanza nikamtema. Nikapata wa pili akanitema. nikampata wa tatu nae naona anaweza kunitema au mimi kumtema. kati ya hao wote niliye mpenda sana naye kunipenda ni X-GIRLFRIEND. Lakini sasa hivi kuna ninae mfukuzia mgeni mgeni hivi. naamin huyu ndo atakuwa wa kufa na kuzika. hakuna sehemu yenye vimwana wanao elewa na kusomeka kama jf. kama anakutaka anakuambia hapo hapo kama hakutaki vilevile wanasema bila chenga. mia
 
Ni habari njema kwa wale waliopata na wakapatana.Hongereni sana kwa wale waliopata, lakini pia kwa wale ambao hatujapapa tuzidi kusonga mbele,kumbe inawezekana, JF iko juu hakuna kumung'unya maneno,asanteni sana wana JF maana na mimi natafuta mchumba (msichana mwenye miaka 22-25),nina imani nitapata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom