RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,332
- 10,540
Lakini wanaume wa Dar nani kawaroga?? Wanaume wa mikoani tunakula ugali maharage nyie mnakula chips hadi mnaandaa matamasha ya kula chips mayai? Hivi hizi heshima kwenye ndoa zenu zitaletwa na ngumi? Jipangeni aisee.....watu wanahamasishana kula ugali wa dona,ugali wa muhogo...nyie mnatuletea vituko gani? Kuweni sirias aisee mnatutia aibu. Huku kwetu Nzega chips mayai inatumika kama mboga wakati wa kula dona nyie mnakula na mnalalia! Halafu baada ya miaka mnaanza kukimbilia kwa DR. MWAKA. Jaman acheni hizi aibu.