Nani kawadanganyeni kuwa Uganda Cranes ( Timu ya Taifa ya Uganda ) itatuachia mwakani mwezi Machi kuna Uwanja wa Taifa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,128
Tena kwa taarifa yenu sasa ni kwamba kama kuna mechi ngumu kwa Taifa Stars na ambayo tukijiandaa nayo sana tutafungwa Goli chache sana 3 ila tukifanya maandalizi ya zima moto kuna hatari ya Kubugizwa / Kufungwa kati ya Goli 7 au 9 Uwanja wa Taifa mwakani mwezi Machi.

Yaani kabisa Uganda Cranes wachafue rekodi yao ya kutokufungwa eti waiachie au wafungwe na Taifa Stars yetu tena hii hii ya Mabeki ' wabovu ' na ' washamba ' akina Ally Sonso na Abdallah Kheri? Labda siyo Uganda Cranes ninayoijua Mimi.

Na hapa wala tusidanganyane na najua ukweli huu utakuwa ni mchungu Kwenu ila kwa wenye akili sawasawa na wanaoujua mpira vyema ni kwamba Safari yetu ya kwenda AFCON nchini Cameroon mwakani imehitimishwa / imezikwa rasmi leo pale Jijini Maseru nchini Lesotho.

Nimewasikia Watangazaji ' Wanafiki ' wa Redio za Tanzania wakijifanya kuwapa moyo Watanzania kuwa eti bado tuna nafasi ila GENTAMYCINE a.k.a Mzee wa Kunyoosha na Kunyooka daima nasema hapa hapa na leo hii hii kuwa tujipange kwa Michuano ya AFCON na mwaka 2021 na tuwekeze nguvu sasa kwa Timu ya Vijana labda huko tunaweza tukabahatisha kwa michuano ya karibuni japo na kwenyewe pia nimeshaanza kuona tatizo hasa kwa upande wa Wachezaji wake ambao kwa sasa na Wao wameshaanza kuwa na Majipu / Maringo na kujiona kuwa tayari nao wamefanikiwa Kimpira wakati ukweli ni kwamba bado hawajui lolote na wanatakiwa kuendelea Kujifunza na Kukomaa zaidi.

Ushindi wa Taifa Stars kwa Uganda Cranes mwezi Machi mwakani ni sare ( draw ) pekee ila siyo kuwafunga na hapa naweza hata kusema bila Kupepesa macho, Kumung'unya maneno wala Kutikisa masikio kwa baada ya matokeo ya Kufungwa na Lesotho kwa Taifa Stars nawaona kabisa Cape Verde ambao hapo awali tulikuwa tunawacheka kuwa wanaenda Kupindua Meza na Wao sasa ndiyo wataungana na Uganda katika Kundi letu na Kufuzu kwenda AFCON mwakani huko Cameroon.

Taifa Stars ikitoka Sare na Uganda Cranes halafu Cape Verde akamfunga Lesotho Kwake Jijini Praia atakuwa na alama Saba ( 7 ) huku Sisi tukiwa na alama zetu Sita ( 6 ) hivyo tutabaki Kuendelea na Ligi yetu hii mbovu ya Mafarasi wakubwa Watatu tu huku wengine wakilia njaa tu na hata Timu zao Kukosa nauli.

Kocha mwenye akili timamu kabisa hawezi kumuacha nje Tanzania Midfield Maestro kwa sasa Jonas Gerald Mkude na kumpanga Himid Mao Mkami ambaye sijawahi Kumkubali na sitokuja Kumkubali kwani hajui mpira bali anabahatisha tu. Utamwekaje nje Faisal Toto halafu kuwaingiza Watu kama akina John Boko na Shiza Kichuya dakika za mwisho kabisa? Hivi huyu Kocha wenu / wetu Amunike anavuta Bange / Bangi au?

Tumevuna tulichopanda na namuomba Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ally Hassan Mwinyi atuongezee neno lingine baada ya lile la ' laana ' alilotuachia kuwa Sisi daima tutaendelea tu kuwa Kichwa cha Mwendawazimu kwani kwa Upomboyo / Upuuzi uliopo tunastahili kupewa kila aina ya majina na laana.

Nawasilisha.
 
Mkuu umemsikia kocha alipohojiwa?Ameulizwa kwanini hukuwaingiza Kichuya,Feisal Toto na Boko mapema.?Jibu lake ilicheza Taifa Stars sio Simba!!
Kweli kocha makini anaweza kujibu utumbo hivyo?
Tuna safari ndefu. Nakubaliana na wewe timu ingepangwa vizuri tungekuwa tumesha qualify baada ya mechi ya leo.
Timu haina midfielders nani awalishe washambuliaji?
Walinzi 8 timu itashinda vipi?
 
Katika vitu ambavyo Uganda hawataweza kufanya ujinga ni kuwalegezea stars kwa sababu wanajua fika kwamba katika mechi ambazo zitakuwa zinachunguzwa kwa umakini na CAF ni hii ya stars na uganda. Na wakijaribu kufanya upumbavu wa kuwaachia Tanzania watapigwa ban kama sieraleone. Ko watajitahid kucheza kwa kadri ya wanavyoweza ili kuogopa adhabu ya CAF. Na waganda wakicheza vizuri hat kwa kiwango cha % 50 bado watatufunga goli nyingi sana!
 
Mmmhhh nawasiwasi kama mtz
 
Huyo Kocha nilishaanza ' Kumchukia ' na ' Kutomkubali ' mapema sana na bahati nzuri kuna hadi ' Uzi ' niliuanzisha hapa wa kumsema na nikasema kuwa hatufai. Kuna Mchezaji mmoja ' Mwandamizi ' kabisa ni Mwanangu / Rafiki yangu pamoja na Kiongozi mmoja ndani ya Taifa Stars wameshangaa kuona kwamba yaani Siku zote Kumi ( 10 ) walizokaa Kambi Kocha alikuwa anawapa Mazoezi magumu utadhani Wanaenda Kupigana Vita kama vya Tanzania na Nduli Amini wa Uganda hadi Wao wakawa wanashangaa.

Na sasa nikuibieni Siri kuwa kama mliangalia Mpira vizuri leo mtagundua ya kwamba ' Body Language ' za Wachezaji wengi wa Taifa Stars zilikuwa zinaonyesha kabisa kuwa walikuwa na ' Fatigue ' ya Mazoezi magumu na ya Kukomoana ya Kocha Amunike hali ambayo iliwafanya Wachezaji wengi wasiwe na Utimamu wa Miili yao kwa 100%.

Huyu Kocha wenu Amunike asidhani hata Sisi akina GENTAMYCINE labda hatujawahi Kukipiga / Kucheza mpira hata kama siyo wa Kiwango alichokifikia Yeye lakini angalau nasi pia huko tulikopita Mashuleni, Mitaani na Kidogo Vyuoni tuliweza Kusumbua na Kusifika kwa Kujua Kucheza mpira vile vile hivyo asidhani nasi hatuwezi Kuusoma mpira na Kumshauri.

Kapombe alikuwa ana wabadala wawili akina Ramadhani Kessy na Salum Kimenya kwanini Yeye akaenda Kutupangia tena kwa Kutujaribia Beki Abdallah Kheri nafasi ya Beki ya Kulia? Mtu kama Gadiel Michael hakuna asiyejua kuwa kuwa ' naturally ' ni Beki wa Kushoto kwanini sasa analazimisha Kumpanga Left Wing? Na kama labda alikuwa ana shida ya Beki wa Kushoto ili kuleta Uwiano sawa kwanini basi hakumuita Mohammed Hussein Zimbwe jr a.k.a Tshabalala?

Hivi kwa ' Form ' ya sasa ya Ibrahim Ajib Migomba ( wenyewe tuliokaa nae Ilala Bungoni, Ilala Boma kwa Masela wa Ashanti United Wazee wa Mitumba na hadi Kucheza nae pale Viwanja wa Msimbazi Center tunamjua kwa jina lake la Utani la Mido ) ni Mtu wa Kutoitwa kweli Taifa Stars na Amunike? Hivi kwa mfano kwa mechi kama ya Lesotho akina Shabaan Iddi Chilunda na John Boko wangekuwa mbele ya Ibrahim Ajib na kwa uchezaji wa Ajib hasa zile pasi zake za ' mitupuo ' au ' macho kumchuzi ' huku akiuchezea mpira anavyoutaka ( dictating the ball ) hawa Lesotho wangepumua kweli pale Kwao?

Kuna Vitu vinaudhi na vinakera mno! Natamani Kuandika hapa ' Msonyo ' wa Kimaandishi ila siuwezi tu. Amunike ametuzingua!
 
Katika vitu ambavyo Uganda hawataweza kufanya ujinga ni kuwalegezea stars kwa sababu wanajua fika kwamba katika mechi ambazo zitakuwa zinachunguzwa kwa umakini na CAF ni hii ya stars na uganda. Na wakijaribu kufanya upumbavu wa kuwaachia Tanzania watapigwa ban kama sieraleone. Ko watajitahid kucheza kwa kadri ya wanavyoweza ili kuogopa adhabu ya CAF. Na waganda wakicheza vizuri hat kwa kiwango cha % 50 bado watatufunga goli nyingi sana!

Umemaliza kila Kitu Mkuu, Safi sana na huwa napenda Kukutana na Watu Werevu / Vichwa / Vipanga kama Wewe hapa Jamvini.
 
Jonas Gerald Mkude alistahili kuanza hii mechi, Ajibu pengine mbele yao angekuwepo Chilunda na Bocco tungeweza kupata matokeo, kingine nilichokiona leo ni defense line ya stars kufanya makosa mengi sana ya kizembe, hii mechi kama Lesotho wangekuwa vizuri tungepigwa ata tatu, Agrey Morris pamoja na ukongwe wake anatoa maboko ya kutosha.
 
Jonas Gerald Mkude alistahili kuanza hii mechi, Ajibu nae vile vile angefanya, pengine mbele yao angekuwepo Chilunda na Bocco tungeweza kupata matokeo, kingine nilichokiona leo ni defense line ya stars kufanya makosa mengi sana ya kizembe, hii mechi kama Lesotho wangekuwa vizuri tungepigwa ata tatu, Agrey Morris pamoja na ukongwe wake anatoa maboko ya kutosha, poor Tanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom