Nani kawadanganyeni kuwa Uganda Cranes ( Timu ya Taifa ya Uganda ) itatuachia mwakani mwezi Machi kuna Uwanja wa Taifa?

Ulichokiandika ndicho kilikuwa kichwani mwangu pia.Tatizo ni kocha,wachezaji au kitu gani?....Lesotho wametrain siku 2 tu!
 
Tutaenda afcon watz na ugonjwa wa kukata tamaa mapema. Kama tulitoa draw na uganda kwao huku kwetu kwa nini cuf washangae tukimfunga? Kumbukeni maseru kuna namba tulizikosa akiwemo sammata kapombe nyoni na banda. Wakiwemo hao uganda atalala tu. Pia lesotho kwa cape verde hatoki salama pale. Tusiwe na wasi mwaka huu wetu. Kocha arekebishe tu upangaj wa timu naona bado
 
Mwenyeji anapewa tiketi ya ushiriki moja kwa moja acha porojo za kijiweni.

Sina uhakika sana,namuona Cameroun naye yupo kwenye makundi anapambana kufa na kupona.Sasa sijajua kama kundi hilo zinatoka Timu tatu kwani Cameroun anaonekana kupata nafasi za juu 1-2.Je angekuwa kashika mkia bado angeshiriki.Ngoja nifiatilie,nitarudi ndugu shoes
 
Ukiwa mwenyeji tiketi unayo tayari mkononi.
Sina uhakika sana,namuona Cameroun naye yupo kwenye makundi anapambana kufa na kupona.Sasa sijajua kama kundi hilo zinatoka Timu tatu kwani Cameroun anaonekana kupata nafasi za juu 1-2.Je angekuwa kashika mkia bado angeshiriki.Ngoja nifiatilie,nitarudi ndugu shoes
 
Huyo Kocha nilishaanza ' Kumchukia ' na ' Kutomkubali ' mapema sana na bahati nzuri kuna hadi ' Uzi ' niliuanzisha hapa wa kumsema na nikasema kuwa hatufai. Kuna Mchezaji mmoja ' Mwandamizi ' kabisa ni Mwanangu / Rafiki yangu pamoja na Kiongozi mmoja ndani ya Taifa Stars wameshangaa kuona kwamba yaani Siku zote Kumi ( 10 ) walizokaa Kambi Kocha alikuwa anawapa Mazoezi magumu utadhani Wanaenda Kupigana Vita kama vya Tanzania na Nduli Amini wa Uganda hadi Wao wakawa wanashangaa.

Na sasa nikuibieni Siri kuwa kama mliangalia Mpira vizuri leo mtagundua ya kwamba ' Body Language ' za Wachezaji wengi wa Taifa Stars zilikuwa zinaonyesha kabisa kuwa walikuwa na ' Fatigue ' ya Mazoezi magumu na ya Kukomoana ya Kocha Amunike hali ambayo iliwafanya Wachezaji wengi wasiwe na Utimamu wa Miili yao kwa 100%.

Huyu Kocha wenu Amunike asidhani hata Sisi akina GENTAMYCINE labda hatujawahi Kukipiga / Kucheza mpira hata kama siyo wa Kiwango alichokifikia Yeye lakini angalau nasi pia huko tulikopita Mashuleni, Mitaani na Kidogo Vyuoni tuliweza Kusumbua na Kusifika kwa Kujua Kucheza mpira vile vile hivyo asidhani nasi hatuwezi Kuusoma mpira na Kumshauri.

Kapombe alikuwa ana wabadala wawili akina Ramadhani Kessy na Salum Kimenya kwanini Yeye akaenda Kutupangia tena kwa Kutujaribia Beki Abdallah Kheri nafasi ya Beki ya Kulia? Mtu kama Gadiel Michael hakuna asiyejua kuwa kuwa ' naturally ' ni Beki wa Kushoto kwanini sasa analazimisha Kumpanga Left Wing? Na kama labda alikuwa ana shida ya Beki wa Kushoto ili kuleta Uwiano sawa kwanini basi hakumuita Mohammed Hussein Zimbwe jr a.k.a Tshabalala?

Hivi kwa ' Form ' ya sasa ya Ibrahim Ajib Migomba ( wenyewe tuliokaa nae Ilala Bungoni, Ilala Boma kwa Masela wa Ashanti United Wazee wa Mitumba na hadi Kucheza nae pale Viwanja wa Msimbazi Center tunamjua kwa jina lake la Utani la Mido ) ni Mtu wa Kutoitwa kweli Taifa Stars na Amunike? Hivi kwa mfano kwa mechi kama ya Lesotho akina Shabaan Iddi Chilunda na John Boko wangekuwa mbele ya Ibrahim Ajib na kwa uchezaji wa Ajib hasa zile pasi zake za ' mitupuo ' au ' macho kumchuzi ' huku akiuchezea mpira anavyoutaka ( dictating the ball ) hawa Lesotho wangepumua kweli pale Kwao?

Kuna Vitu vinaudhi na vinakera mno! Natamani Kuandika hapa ' Msonyo ' wa Kimaandishi ila siuwezi tu. Amunike ametuzingua!
Gentamycine mie toka jana sijapona hasira na stress alizonisababishia yule kocha muovu mshenzi kabisa ambaye amehodhi wachezaje wazuri kabisa wa kutuvusha anaishia kupanga madudu anayoyajua yeye na waliomtuma.
Nina waswas kapewa fedha na wa lesotho yule
 
Gentamycine mie toka jana sijapona hasira na stress alizonisababishia yule kocha muovu mshenzi kabisa ambaye amehodhi wachezaje wazuri kabisa wa kutuvusha anaishia kupanga madudu anayoyajua yeye na waliomtuma.
Nina waswas kapewa fedha na wa lesotho yule

Pole sana Mkuu.
 
Tena kwa taarifa yenu sasa ni kwamba kama kuna mechi ngumu kwa Taifa Stars na ambayo tukijiandaa nayo sana tutafungwa Goli chache sana 3 ila tukifanya maandalizi ya zima moto kuna hatari ya Kubugizwa / Kufungwa kati ya Goli 7 au 9 Uwanja wa Taifa mwakani mwezi Machi.

Yaani kabisa Uganda Cranes wachafue rekodi yao ya kutokufungwa eti waiachie au wafungwe na Taifa Stars yetu tena hii hii ya Mabeki ' wabovu ' na ' washamba ' akina Ally Sonso na Abdallah Kheri? Labda siyo Uganda Cranes ninayoijua Mimi.

Na hapa wala tusidanganyane na najua ukweli huu utakuwa ni mchungu Kwenu ila kwa wenye akili sawasawa na wanaoujua mpira vyema ni kwamba Safari yetu ya kwenda AFCON nchini Cameroon mwakani imehitimishwa / imezikwa rasmi leo pale Jijini Maseru nchini Lesotho.

Nimewasikia Watangazaji ' Wanafiki ' wa Redio za Tanzania wakijifanya kuwapa moyo Watanzania kuwa eti bado tuna nafasi ila GENTAMYCINE a.k.a Mzee wa Kunyoosha na Kunyooka daima nasema hapa hapa na leo hii hii kuwa tujipange kwa Michuano ya AFCON na mwaka 2021 na tuwekeze nguvu sasa kwa Timu ya Vijana labda huko tunaweza tukabahatisha kwa michuano ya karibuni japo na kwenyewe pia nimeshaanza kuona tatizo hasa kwa upande wa Wachezaji wake ambao kwa sasa na Wao wameshaanza kuwa na Majipu / Maringo na kujiona kuwa tayari nao wamefanikiwa Kimpira wakati ukweli ni kwamba bado hawajui lolote na wanatakiwa kuendelea Kujifunza na Kukomaa zaidi.

Ushindi wa Taifa Stars kwa Uganda Cranes mwezi Machi mwakani ni sare ( draw ) pekee ila siyo kuwafunga na hapa naweza hata kusema bila Kupepesa macho, Kumung'unya maneno wala Kutikisa masikio kwa baada ya matokeo ya Kufungwa na Lesotho kwa Taifa Stars nawaona kabisa Cape Verde ambao hapo awali tulikuwa tunawacheka kuwa wanaenda Kupindua Meza na Wao sasa ndiyo wataungana na Uganda katika Kundi letu na Kufuzu kwenda AFCON mwakani huko Cameroon.

Taifa Stars ikitoka Sare na Uganda Cranes halafu Cape Verde akamfunga Lesotho Kwake Jijini Praia atakuwa na alama Saba ( 7 ) huku Sisi tukiwa na alama zetu Sita ( 6 ) hivyo tutabaki Kuendelea na Ligi yetu hii mbovu ya Mafarasi wakubwa Watatu tu huku wengine wakilia njaa tu na hata Timu zao Kukosa nauli.

Kocha mwenye akili timamu kabisa hawezi kumuacha nje Tanzania Midfield Maestro kwa sasa Jonas Gerald Mkude na kumpanga Himid Mao Mkami ambaye sijawahi Kumkubali na sitokuja Kumkubali kwani hajui mpira bali anabahatisha tu. Utamwekaje nje Faisal Toto halafu kuwaingiza Watu kama akina John Boko na Shiza Kichuya dakika za mwisho kabisa? Hivi huyu Kocha wenu / wetu Amunike anavuta Bange / Bangi au?

Tumevuna tulichopanda na namuomba Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ally Hassan Mwinyi atuongezee neno lingine baada ya lile la ' laana ' alilotuachia kuwa Sisi daima tutaendelea tu kuwa Kichwa cha Mwendawazimu kwani kwa Upomboyo / Upuuzi uliopo tunastahili kupewa kila aina ya majina na laana.

Nawasilisha.
Wahenga walishamaliza kuwa ...Ng'ombe hanenepi siku ya mnada........hakuna namna ambavyo watu wanasubiri mpaka siku za mwisho ndo wanaweka nguvu katika mchezo halafu wategemee miujiza. Matokeo ya Mpira ni mikakati ya muda mrefu, sio propaganda na maneno ya midomoni. Aidha, hali ya Tanzania ambayo watu wana wasi wasi ya maisha, haitoi hali ya utulivu kwa wachezaji na viongozi kutulia na kuwaza michezo. Hakuna mtu wa kuwaza michezo ilhali hana uhakika wa kesho.
 
Cameroon alikua 50/50 anaweza kunyang'anywa uandaaji, kutokana na wasiwasi mambo ya uchaguzi na maandalizi kwa ujumla, kwahiyo akatakiwa kupambana

Hapo sasa nimekuelewa,kwa kuwa nilikuwa sioni logic ya yeye kuhangaika na kusaka hizo nafasi mbili wakati yeye ni mwenyewe.Thanks bro.Na mimi nimesikia kuna sintofahamu kati ya Cameroun-Anglophone vs Cameroun Francophone.Bado nina hasira na michezaji mizembe ya Taifa stars.Michezaji minne imekaa kwenye mstari wa goli na mpira unaipita baada ya kipa kuuparaza badala ya kupiga ngumi mpira na mbaya sana kona ya kujitakia mabeki wawili wakiwa peke yao mmoja anaamua kuutoa mpira kona iliyozaa goli……………..
 
Yule mwalimu hata sijui alikiwa anakusudia nn..cjaelewa hadi ss hiv.
Ile gem sisi tulitakiwa kushinda, sasa yy kutupangia timu wakabaji watupu ndio vp?!
Hiv kwa nn kulia asingecheza nyoni, kushoto gadiel kati mkude na faisal shavu kulia msuva,kushoto kichuya na kati bocco na chilunga?!
Ile gem ndio pekee ilikuwa ya uhakika na kupambana mpaka mwisho kupata point 3, kwa nn asingetumia silaha zake zote?! Ss wale wakabaji bila hata c. Striker?! Jamaa akatufanyia kusudi kutunyima hii nafasi.
Nafsi imehamanika sana kwa matokeo ya kujitakia ya huyu mwalimu.
 
Yule mwalimu hata sijui alikiwa anakusudia nn..cjaelewa hadi ss hiv.
Ile gem sisi tulitakiwa kushinda, sasa yy kutupangia timu wakabaji watupu ndio vp?!
Hiv kwa nn kulia asingecheza nyoni, kushoto gadiel kati mkude na faisal shavu kulia msuva,kushoto kichuya na kati bocco na chilunga?!
Ile gem ndio pekee ilikuwa ya uhakika na kupambana mpaka mwisho kupata point 3, kwa nn asingetumia silaha zake zote?! Ss wale wakabaji bila hata c. Striker?! Jamaa akatufanyia kusudi kutunyima hii nafasi.
Nafsi imehamanika sana kwa matokeo ya kujitakia ya huyu mwalimu.

Angepanga moja ya Kikosi hiki yote haya yasingemkuta ila kwa sasa atuvumilie tu tumpe ' makavu ' yetu ' mubashara ' ili atujue Watanzania na akienda Kwao nchini Nigeria akawasimulie vizuri. Mpuuzi kabisa huyu Kocha na ndiyo maana sikumkubali tokea alipoteuliwa baada ya Kuziangalia vizuri ' CV ' zake hasa kwa Timu alizozifundisha katika nchi mbalimbali.

1. Aishi Manula

2. Shomari Kapombe / Salum Kimenya
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondan
6. Jonas Mkude
7. Simon Msuva
8. Abubakary Salum / Faisal Salum
9. Thomas Ulimwengu / Shaaban Chilunda
10. John Boko
11. Shiza Kichuya


au

1. Aishi Manula

2. Ramadhan Kessy / Salum Kimenya
3. Abdi Banda / Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondan
6. Jonas Mkude
7. Simon Msuva
8. Faisal Salum / Abubakary Salum
9. Shaaban Chilunda / Thomas Ulimwengu
10. John Boko

11. Shiza Kichuya

Yaani kwa hasira / jazba nilizokuwa nazo nimeshindwa kabisa ' Kumbandua / Kumtunuku ' Utamu wa Kitandani Demu wangu tokea jana ile hadi sasa. Mkuyenge wangu nao ' umenuna ' kabisa kwa matokeo haya ya Kukera / Kuudhi kabisa.
 
Huyu angeatkiwa akutane na mabegi yake airport ya kwao huko hakuna hata haja ya kurudi tena Tanzania.

Na nashangaa mpaka sasa hili bado halijafanyika Mkuu au sijui wanataka Kwanza atue Jijini Dar es Salaam ili ' tumpopoe ' Kwanza na Mawe kisha akishapata manundu na ngeu ndipo arudi Kwao Abuja / Lagos!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom