Nani kati ya Makamu wa Rais na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi analidanganya taifa kuhusu suala la Samaki?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,156
Katika siku za Karibuni, zimetolewa kauli mbili tofauti toka kwa viongozi wakubwa kabisa Katika Serikali yetu ya CCM.

Kwanza ilitolewa kauli na Makamu wa Rais, Dkt. Philipo Mpango, akiwa jijini Mwanza kikazi, ambaye aliagiza vyombo vyote vinavyozibiti maji ya kuoshea maiti yenye dawa ya chloroform, aliyodai kuwa yanatumika kuhifadhi samaki, kwa hiyo akaelezea wasiwasi wake kuwa, kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani nchini, ambao kwa maelezo yake, ongezeko hilo linatokana na ulaji huo wa samaki, ambao wanahifadhiwa kwa kutumia maji hayo ya kuhifadhia maiti.

Baada ya siku chache, akaibuka Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, tena ndani ya Bunge letu jijini Dodoma, akikanusha vikali taarifa hiyo ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, aliyoitoa na kuiita kuwa ni ya uongo na ya kufikirika!

Watanzania tunataka kuujua ukweli, Katika hili jambo nyeti Sana, linalohusu uhai wetu, je ni Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, au ni Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, ambaye amelidanganya Taifa letu?

Kuliacha jambo hili hivi hivi tu, ni kuhatarisha uhai wa mamilioni ya watanzania, ambao ni watumiaji wa samaki hao, iwapo kauli ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango itakuwa ya kweli.

Mimi binafsi ninaamini kuwa, kauli iliyotolewa na Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, siyo ya kukurupuka na itakuwa na ukweli, kwani atakuwa amepewa taarifa za uchunguzi na wataalamu wa wizara hiyo ya Mifugo na uvuvi.

Kwa kuwa jambo hili ni kubwa Sana na linahusu uhai wa mamilioni ya raia wa nchi hii, wanaotumia bidhaa hiyo ya samaki, ninapendekeza kuwa iundwe Tume huru ya kulichunguza jambo hili na matokeo ya Tume hiyo, yatolewe hadharani kwa Umma wa watanzania na itakapogundulika mmoja wao, Kati ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango au Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, amelidanganya Taifa, basi awajibike kwa kujuzulu wadhifa wake mara moja, kwa kuudanganya Umma wa watanzania 🥺

Mungu ibariki Tanzania.
 
Naibu waziri Ulega alisema taarifa ya mbunge wa Chadema mh Pareso ndio ya Uwongo
johnthebaptist
Unawezaje kusema kauli ya Mbunge wa Chadema ni ya uongo, wakati unajua kuwa huyo Mbunge aliuliza swali kutaka kupata ufafanuzi kuhusu kauli iliyotolewa na Makamu wa Rais, kuhusu maji hayo ya kuhifadhia maiti, kuwa ndiyo yanayotumika pia, kuhifadhia samaki?

Ni jambo la hatari Sana, viongozi wa CCM, kulichukulia jambo "serious" kama hilo, kulichukulia kimzahamzaha!🥺
 
Naunga mkono ukweli wa taarifa ya Dr. Mpango.
Ni kweli.

Dkt Mpango ametoa taarifa hiyo, baada ya kupenyezewa na wataalamu Kutoka wizara hiyo.

Huyu Naibu Waziri ameamua kutudanganya watanzania, Ili kulinda soko la samaki.

Lakini ni kipi cha umuhimu zaidi, ni uhai wa watanzania au ni hilo soko la samaki lisiporomoke?

Nashauri Tume huru ya kulichunguza sakata hili, iundwe mara moja, Ili ukweli ubainike
 
Katika siku za Karibuni, zimetolewa kauli mbili tofauti toka kwa viongozi wakubwa kabisa Katika Serikali yetu ya CCM.

Kwanza ilitolewa kauli na Makamu wa Rais, Dkt. Philipo Mpango, akiwa jijini Mwanza kikazi, ambaye aliagiza vyombo vyote vinavyozibiti maji ya kuoshea maiti yenye dawa ya chloroform, aliyodai kuwa yanatumika kuhifadhi samaki, kwa hiyo akaelezea wasiwasi wake kuwa, kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani nchini, ambao kwa maelezo yake, ongezeko hilo linatokana na ulaji huo wa samaki, ambao wanahifadhiwa kwa kutumia maji hayo ya kuhifadhia maiti.

Baada ya siku chache, akaibuka Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, tena ndani ya Bunge letu jijini Dodoma, akikanusha vikali taarifa hiyo ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, aliyoitoa na kuiita kuwa ni ya uongo na ya kufikirika!

Watanzania tunataka kuujua ukweli, Katika hili jambo nyeti Sana, linalohusu uhai wetu, je ni Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, au ni Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, ambaye amelidanganya Taifa letu?

Kuliacha jambo hili hivi hivi tu, ni kuhatarisha uhai wa mamilioni ya watanzania, ambao ni watumiaji wa samaki hao, iwapo kauli ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango itakuwa ya kweli.

Mimi binafsi ninaamini kuwa, kauli iliyotolewa na Naibu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, siyo ya kukurupuka na itakuwa na ukweli, kwani atakuwa amepewa taarifa za uchunguzi na wataalamu wa wizara hiyo ya Mifugo na uvuvi.

Kwa kuwa jambo hili ni kubwa Sana na linahusu uhai wa mamilioni ya raia wa nchi hii, wanaotumia bidhaa hiyo ya samaki, ninapendekeza kuwa iundwe Tume huru ya kulichunguza jambo hili na matokeo ya Tume hiyo, yatolewe hadharani kwa Umma wa watanzania na itakapogundulika mmoja wao, Kati ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango au Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, amelidanganya Taifa, basi awajibike kwa kujuzulu wadhifa wake mara moja, kwa kuudanganya Umma wa watanzania

Mungu ibariki Tanzania.
VP amekurupuka.
 
Nia ya mpango ni nzuri shida ameiwakilisha vibaya.
Angesema dawa ya kuifadhia maiti zisiharibike ndo wanatumia.NA HUO NDO UKWELI.watu wanatumia mpaka mafuta ya transfoma kukaangia chips .muache mnaua wenzenu.siku hizi unakula samaki kabaki mnofu tu LADHA HANA
 
Watanzania tunataka kuujua ukweli, Katika hili jambo nyeti Sana, linalohusu uhai wetu, je ni Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, au ni Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, ambaye amelidanganya Taifa letu?
Jiulize kwanza: Philipo yeye kalitoa wapi jambo hilo, maana hawezi kuamka tu usingizini na kwenda kulitamka alivyofanya.

Na kama haitoshi, inakuwaje Makamu akatoa taarifa nzito kiasi kile bila kuwasilianan na wizara husika katika serikali yake?
Hili ni jambo la kushangaza sana.

Sasa turudi kwenye hiyo dawa yenyewe: Haiwezi ikawa chloroform. Chloroform haitumiki kuhifadhi maiti.

Hata hivyo, chloroform ni dhaifu zaidi katika kusababisha saratani. Miaka siyo mingi sana iliyopita, chlorofrm hiyo hiyo ilikuwa ikitumika kuchanganyia dawa za binaadam, na imetumika kwa muda mrefu kiasi, na hapakuwa na wingi wa hiyo saratani. Ndiyo, baadae inadhaniwa kuwa na madhara hayo, lakini siyo kwa kiasi hicho cha kutia woga.

Bila shaka dawa inayozungumziwa hapa itakuwa Formaldehyde (Formalin), ambayo ndiyo hasa kazi yake ni kuhifadhi maiti, na haijawahi hata mara moja kutumika kwa matumizi ya binaadam kwa kumeza au kupaka. Inajulikana zaidi kuwa na madhara ya kusababisha saratani.

Na mwisho: Haya yanayotokea ni dalili wazi kabisa za taasisi zetu kutofanya kazi ipasavyo. Haiwezekani kabisa watu wawe wanatumia vitu hatarishi kwa maisha ya binaadam kirahisi namna hii bila kujulikana.
Hii ni dalili moja wapo ya nchi yetu kuwa 'Banana Republic' kwelikweli.

Ndiyo maana gonjwa hatarishi kabisa linaingia nchini, halafu wanasiasa ndio wanakuwa mstari wa mbele kupinga uwepo wa gonjwa lenyewe!

Si ajabu hata 'Panya Road' wanatamba!

Sijui ni jambo lipi tunaloweza kujivunia kama nchi kwa sasa. Labda mafanikio ya CCM kuwalaza akili waTanzania. Katika hili hakuna mfano unaotufikia sisi.
 
Dr.Mpango ni kilaza anayeyafuta kiki! PhD za kununua ni janga kwa taifa.
Hivi hajui hizo samaki zinauzwa ndani na nje ya nchi? Akiua solo LA samaki kwa kauli za vijiweni anajua athari zake?!
Hapana.
PH.D. ya Mpango, kama kweli ni ya kununua, basi hakuna tena mwenye Ph.D. katika serikali ile.

Lakini hili tuliweke pembeni, linalonishangaza na kunisikitisha mimi ni kukosekana kwa mawasiliano humo humo ndani ya serikali yenyewe. Kuna ugumu gani kwa Makamu wa Rais kuthibitisha taarifa kwanza kwa wahusika kabla ya kuisemea; hasa kwenye jambo la kutisha kama hili.

Hapana tena, katika hiyo hofu yako ya kukosa soko.
Kama jambo lenyewe kweli lipo, ni sahihi kabisa kulizungumzia bila kujali hayo masoko unayolinda wewe. Uhai wa binaadam ni muhimu zaidi kuliko hayo masoko unayoyasema hapa..
Unataka Makamu anyamaze, akae na taarifa huku akijua. hao tunaowauzia hao samaki, na raia wetu wenyewe wakiendelea kudhurika, hilo soko litakuwa na faida kwa nani?
 
Tatizo hao wote ni wanasiasa, ningefurahi kama angepatikana mtaalamu akazungumzia hilo jambo, lakini bahati mbaya wataalamu wetu nao wakati mwingine hutumiwa na wanasiasa, kwa hali hiyo, naona hili nalo litapita tu, kama yanavyopita mengine.
 
Jiulize kwanza: Philipo yeye kalitoa wapi jambo hilo, maana hawezi kuamka tu usingizini na kwenda kulitamka alivyofanya.

Na kama haitoshi, inakuwaje Makamu akatoa taarifa nzito kiasi kile bila kuwasilianan na wizara husika katika serikali yake?
Hili ni jambo la kushangaza sana.

Sasa turudi kwenye hiyo dawa yenyewe: Haiwezi ikawa chloroform. Chloroform haitumiki kuhifadhi maiti.

Hata hivyo, chloroform ni dhaifu zaidi katika kusababisha saratani. Miaka siyo mingi sana iliyopita, chlorofrm hiyo hiyo ilikuwa ikitumika kuchanganyia dawa za binaadam, na imetumika kwa muda mrefu kiasi, na hapakuwa na wingi wa hiyo saratani. Ndiyo, baadae inadhaniwa kuwa na madhara hayo, lakini siyo kwa kiasi hicho cha kutia woga.

Bila shaka dawa inayozungumziwa hapa itakuwa Formaldehyde (Formalin), ambayo ndiyo hasa kazi yake ni kuhifadhi maiti, na haijawahi hata mara moja kutumika kwa matumizi ya binaadam kwa kumeza au kupaka. Inajulikana zaidi kuwa na madhara ya kusababisha saratani.

Na mwisho: Haya yanayotokea ni dalili wazi kabisa za taasisi zetu kutofanya kazi ipasavyo. Haiwezekani kabisa watu wawe wanatumia vitu hatarishi kwa maisha ya binaadam kirahisi namna hii bila kujulikana.
Hii ni dalili moja wapo ya nchi yetu kuwa 'Banana Republic' kwelikweli.

Ndiyo maana gonjwa hatarishi kabisa linaingia nchini, halafu wanasiasa ndio wanakuwa mstari wa mbele kupinga uwepo wa gonjwa lenyewe!

Si ajabu hata 'Panya Road' wanatamba!

Sijui ni jambo lipi tunaloweza kujivunia kama nchi kwa sasa. Labda mafanikio ya CCM kuwalaza akili waTanzania. Katika hili hakuna mfano unaotufikia sisi.
Ndiyo maana, hata Mimi nimesema uwezekano wa kuwa Makamu wa Rais kuwa ndiye aliyelidanganya Taifa haupo, bali huyo Naibu Waziri wa Mifugo, ndiye anayetaka kuuficha ukweli.

Kama ndiyo hivyo, nikasema huyo Naibu Waziri anapaswa aachie ngazi mara moja!

Hatuwezi kuwa na Serikali, ambayo Vongozi wake ni waongo!
 
Bahati mbaya ni kwamba nani wa kumfunga paka kengere ikiwa kauli hiyo si ya kumpinga mkuu wa nchi Kama tulivyo shuhudia kwa ndugai.
 
Wenye Akili timamu tunajua kuwa kauli ya Dr mpango ndiyo valid kwasababu yeye ameongea baada ya kupewa taarifa iliyofanyiwa tafiti Ila Kwa vile tupo biashara pia ndiyo maana imetolewa kauli ya kulainisha ili mambo yasiwe mengi....
kwavile nchi hii ina vilaza wengi kuna MAFALA watakuja kupinga kauli ya Dr mpango
 
Back
Top Bottom