streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 474
Nimekaa nimetafakari nikakumbuka wimbo wa Madee uitwao Hip Hop haiuzi, kiukweli ukitazama kwa kina utakuta ni kauli ya mtu aliekata tamaa na kitu anachokifanya na hii imefanya watu wengi wenye talent na aina ya mziki huu kukimbia na kutafuta kivuli katika miti mingine wakidhani msitu was Hip hop umenyauka Lakini kutokana na juhudi za watu wasiokata tamaa walihakikisha wanarudisha hadhi na heshima ya muziki huu pendwa na rika zote..tumeshuhudia wasanii kama Fid Q, Weusi, Tamaduni Music, Darasa na wengine wengi wakifanikisha mapinduzi haya. Mpaka dakika hii Music wa Hip hop ndo huko juu kutokana na wimbo wa Darasa kufanya vizuri, Wito wangu kwa wanaharakati wote nikuendelea na mapambano kuhakikisha hii hadhi tuliyonayo haishuki ili tuweze kushika usukani katika gurudumu la hii tasnia ya muziki Tanzania.