Nani kapita hapa?

Iruru

JF-Expert Member
Jan 27, 2014
1,471
2,889
Ndanda+Mates+2004-06+20170514_143401.jpg
wale tuliopita haya maeneo tujikumbushe yale mazuri na hata mabaya pia! I love the place....
 
Ndanda sec hapo miaka hiyo mkuu alikuwa Mwasi,makamu Mtauka,third master Ismail na academic master Bonge la mtu sasa ni marehemu.Ngoma kubwa ni lizangati
 
Ndanda sec hapo miaka hiyo mkuu alikuwa Mwasi,makamu Mtauka,third master Ismail na academic master Bonge la mtu sasa ni marehemu.Ngoma kubwa ni lizangati
Mkuu miaka gani hiyo hahaaa...mie nilipita hapo mkuu akiwa jamaa fukani hivi anaitwa mlaponi, second Mzee hassan na third master gowelle, mengi nayakumbuka, ikiwa ni pamoja na source, kiwanda cha mawe na juice cha wabenedoctine, wasichana manesi warembo bila kilisahau lizngati hahaaa
 
Peruree ruleee ndanda boys peru peru ndanda boys.
2006-2008 kilimanjaro-mawenzi room 21 tuliita horizon deep.

Tv room mv bukoba .
Lecture room ukumbi wa Manchester.
Head Master ..Mzee Mmoja ivi (mlemavu flani)
Makamu nadhani alikuwa Sowone.
Makota G (rip)
Halafu kuna Muhidin (Mjahidina)
Kulikuwa na kimadam flani ivi kilikuwa laboratory, achana na mama tesha.

Yumba Kabobo,alikuwa mtata balaa
 
Mzee Milinga (H/M)
Akamuachia jamaa mmoja ivi alitokea Mahiwa
 
Peruree ruleee ndanda boys peru peru ndanda boys.
2006-2008 kilimanjaro-mawenzi room 21 tuliita horizon deep.

Tv room mv bukoba .
Lecture room ukumbi wa Manchester.
Head Master ..Mzee Mmoja ivi (mlemavu flani)
Makamu nadhani alikuwa Sowone.
Makota G (rip)
Halafu kuna Muhidin (Mjahidina)
Kulikuwa na kimadam flani ivi kilikuwa laboratory, achana na mama tesha.

Yumba Kabobo,alikuwa mtata balaa
Mkuu huyo headmaster bila shaka ni milliba, sisi tuliingia hapo 2004-2006, wakati huo ilikuwa bado mchanganyiko. Tulipiga kitu cha mbaazi mpaka tukang'ooka meno ilihali washikaji wa chidya boys mambo safi wakati wa maboresho sekondari; mmes, tukaanzisha kunji, head master alikuwa mlaponi. Safari ilianza saa tisa usiku kuelekea kwa mkuu wa wilaya masasi. Bahati mbaya kulikuwa na msafara wa mwinyi masasi alikuwa akija kwenya kampeni za kikwete-2005, tukazuiwa na defender kama kumi hivi, mkuu wa polisi wakati ule omari mahita. Tulipokaidi amri tukapokea kipigo sana ila kutokana na wingi wetu wakashindwa kutuzuia. Tukafika masasi, tupeleka kilio chetu na baadaye tukarudishwa shuleni na karandinga za polisi. Hatimaye mlaponi akaondoka na milinga akaletwa! Tukapiga nyali mfululuzo hadi febr-2006 tulipoondoka. Tulimaliza tu na shule ikafungwa kwa kuishiwa Chakula. All in all ndanda is the best school, kule cube, mizizi, kusimamisha minazi jadi ya wazee wa lizangati sana hahaaa
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Hii sehemu naona wengi hawaijui au hawaikumbuki, maana kila mtu anaongea lugha yake kama watu wa mnara wa babeli…
 
Back
Top Bottom