uwiiiiiiii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 341
- 365
Hakika mwanamke ni wakuthaminiwa na kuheshimiwa katika jamii, japo leo mwanamke anakandamizwa na mfumo dume unamkandamiza kijinsia kiukweli bado wanawake tuna wajibu mkubwa sana.
Katika siku mbili zilizopita mwanangu ameumwa sana usiku mchana hali ilikuwa mbaya sana, japo nilimpatia dawa kwa haraka jinsi dawa zilivyokuwa zikifanya kazi alikuwa anachemka sana mtu usingizi hauji kabisa, kama mama nilijikuta natafakari upendo wa mama kwa mwanae pia jinsi mama zetu walivyokuwa wanatulea.
Jamani tuwathamini sana mama zetu maana kuwaheshimu, Nachoshangaa wanaume wengi wanawadharau wanawake na kuwanyanyasa, lakini tukumbuke ndio hao waliotulea, kutufundisha, kutulinda, kututunza, hata huyo aliyekuzalia watoto anashahili heshima kubwa.
Leo tuna janga kwa waume zetu hawalioni hili wao ni kutapanya na michepuko tu mwanamke kwake kama takataka mchepuko wa thamani, hata watoto kwao hawawaoni wa thamani kama michepuko, ukiangalia thamani ya mtoto na mchepuko unakuta hana mapenzi kwa uzao wake.
Hivi ni laana ama? Nashindwa kuelewa wakuu