Nani huyu Ridhiwani Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani huyu Ridhiwani Kikwete?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Masanja, Jan 7, 2011.

 1. C

  Chief Masanja Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari za leo wajukuu zangu?

  ni kwa kipindi kirefu kweli nimeshuhudia huu mjadala juu ya huyu kijana mwenzenu! kama ilivyo ada yangu, leo nimeamua nijitokeze tena; pamoja na mambo mengine mengi ambayo yametokea hapa karibuni na mwaka huu mpya leo nataka nieleze kwa ufupi juu ya huyu kijana na jinsi ninavyo mjua mimi.........

  RIDHIWANI KIKWETE,kama wengin wanavyomjua alizaliwa katika hospital ya wilaya ya bagamoyo tarehe 16 mwezi wa NNE mwaka 1979. kijana huyu alizaliwa toka kwa mama AZIZA bint SABURI na baba JAKAYA MRISHO KIKWETE.

  RIDHIWANI ni kijana wa kwanza kwa wazazi hawa na alifuatiwa na mdogo wake anayejulikana kwa jina la SALAMA ambaye kwa sasa ni daktari na mwalimu pale MUHIMBILI chuoni.

  kijana huyu alianza shule ya msingi mwaka 1987 pale shule ya msingi MATANGINI,nachingwea mkoa wa LINDI.sababu kubwa za yeye kuanza shule huko ni kazi aliyokuwa akifanya baba yake kipindi hicho. ikumbukwe kuwa bwana Kikwete alikuwa katibu wa CCM ,wilayani hapo. mwaka mmoja baadae, bwana ridhiwani na baba yake waliamia MASASI,mkoa wa MTWARA.akiwa huko alijiunga na shule ya MKOMAINDO kwa masomo yake ya darasa la pili kabla hawajarudi DAR ES SAALAAM, mwaka1989 ambapo alijiunga na shule ya FORODHANI iliyopo maeneo ya posta ya zamani hadi alipomaliza darasa la saba.

  masomo ya sekondari aliyapata katika shule ya SHAABAN ROBERT na baadae MKWAWA mkoani IRINGA kabla ya kurudi DAR ES SALAAAM kwa ajili ya elimu ya juu katika CHUO KIKUUU CHA DAR ES SALAAM, sehemu ya mlimani na baadae ENGLAND,kwa masomo ya cheti cha elimu ya juu.

  KISIASA
  kisiasa kijana huyu alianza akiwa mdogo sana.historia inaanza akiwa nyumbani kwao na babu yake pale bagamoyo, ambapo alishiriki katika shughuli za kucheza gwaride kama chipukizi wa chama na hata alipokwenda huko NCHINGWEA NA MASASI aliendelea na shughuli za kucheza gwaride la chipukizi wa chama cha mapinduzi.

  mwaka 1992, alikuwa ni mmoja kati ya vijana walioshiriki kama wajumbe kwenye mkutano mkuu wa chipukizi wa ccm taifa uliofanyika mbeya ambao ulimchagua bwana RAYMOND MANGWALE kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa. ( ikumbukwe bwana RAYMOND ni katibu wa UV-CCM, mkoa wa DODOMA ,kwa sasa). hata hivyo pia, wakati wa enzi hizo za masomo ya shule ya msingi, ridhiwani atakumbukwa kama kijana aliyechangia hela nyingi kwenye mradi wa mabasi ya UV-CCM na hata kupeWa nishani na RAISI mstaafu wa AWAMU YA PILI, ALHAJI ALLY HASSAN MWINYI katika viwanja vya KARIMJEE sherehe ambazo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali na viopngozi wa serikali.

  wakati yupo sekondari aliendelea kuwa mwana harakati wa kawaida pale shuleni DAR ES SALAAM na hata baadae IRINGA.Waliosoma naye iringa wanakumbuka pilika zake na wenzake katika siasa za wanafunzi ,na michezoni.alikuwa mcheza mpira mzur sana enzi hizo.sijui siku hizi kama anacheza au bado.kumbukumbu zinaonyesha ushiriki wake katika kampeni za kufanikisha wenzake kupata nafasi za uongozi.

  wakati akiwa chuoni, alikuwa mstari wa mbele katika siasa za DARUSO. RIDHIWANI amewahi kuwa katibu wa serikali ya wanafunzi, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA WANAFUNZI WANAOTOKA NCHI ZA NJE, na baadae alikuwa MBUNGE MWAKILISHI TOKA KITIVO CHA WANAFUNZI WA SHERIA, kabla hajawa MWENYEKITI WA DARUSO-KITIVO CHA SHERIA.

  katika kipindi hiki tumeona alivyokuwa akishiriki katia siasa za wanafunzi na hata kushirikiana na wenzake kuhakikisha kuwa yale mambo wanayoyataka katika mazingira ya chuoni hapo yanakuwa vizuri.

  Wakati yupo chuoni, akiwa mwaka wa tatu, 2002 aliteuliwa kuwa MUHAMASISHAJI WA UVCCM-wilaya ya BAGAMOYO.ikumbukwe kipindi hiki ni kipindi bwana SAIDI MTANDA ambaye kwa sasa ni MBUNGE WA JIMBO LA MCHINGA,LINDI alikuwa ndiyo MWENYEKITI WA UVCCM wilaya ya bagamoyo.ufanisi wa bwana RIDHIWANI katika mambo ya shughuli za vijana ikiwemo kushirikiana na wenzake kufanya makambi ya kuwaandaa vijana kwa shughuli za jumuiya na mchango wake ulimpelekea kuchaguliwa 2004 kuwa MJUMBE WA BARAZA LA UVCCM-PWANI.ikumbukwe kuwa kipindi hiki mwenyekiti wa vijana mki=oa wa pwani alikuwa BW.KULWA SAID.

  katika uchaguzi wa ndani wa CCM , mwaka 2007 bwana RIDHIWANI lichaguliwa kwa kura nyingi , tena kwa kuongoza kwa wingi wa kura kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA (nafasi abayo anayo hadi sasa).Pamoja na hillo pia RIDHIWANI katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 lichaguliwa na vijana wenzake wa wilaya ya BAGAMOYO kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA UVCCM-TAIFA na pia MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM YA WILAYA -BAGAMOYO.

  nafasi ya ujumbe wa halmashauri ya ccm ya wilaya , inampa nafasi ya kuwawakilisha vijana wenzake ndani ya vijao vya chama ngaz ya wilaya. mwaka 2008 alichaguliwa kuwa MJUMBE WA BARAZA KUU LA VIJANA TAIFA kuwakilisha UVCCM-PWANI na kabla kikao cha baraza kuu akijamchagua yeye kuwa MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM-TAIFA.

  RIDHIWANI amekuwa akishiriki katika shughuli za vijana kila siku. kama walivyovijana wengine amekuwa mstari wa mbele kukitetea chama chake cha CCM na pia sera zake. ameshiriki katika mambo yanayohusu vijana wenzake katika makundi mbalimbali hasa yale ya wanafunzi,wanamuziki,wanamitindo,walemavu na mengoineyo mengi.

  Kichama ameshiriki kwenye mambo mengi hasa ili la kampeni za chama safari hii. yeye na wenzake akiwemo MAKAMU MWENYEKITI, KATIBU MKUU,NAIBU KATIBU MKUU na wengineo ambao waligawanyika katika makundi mbalimbali wakikinadi chama chao.kubwa zaidi ni jinsi walivyojipanga vijana hasa kukisaidia chama chao kirudi lakini Ukiacha yote ni jinsi kijana alivyokuwa mstari wa mbele kuhahakikisha mambo yanakuwa mazuri.

  RIDHIWANI amewahi wakilisha nchi yetu katika mikutano mbalimbali toka akiwa mtoto. mtakumbuka mkutano wa watoto ,ROME 1992, YES-SUMMIT MEXICO 2001,PANEL ON ENVIRONMENTAL SINGAPORE 2005,COMMONWEALTH YOUTH ORGANISATION MALTA 2007- YES-AFRICAN CAUCAS LESOTHO 2006, DEVELOPMENT AND CHALLENGE FACING RULLING PARTIES-SOUTH AFRICA 2008 na mengineyo mengi

  RIDHIWANI ameoa na mungu amemjalia mtoto mmoja wa kike anaitwa AZIZA.

  ni imani wajukuu zangu sasa mnamuelewa kidogo RIDHIWANI.tunapojadili ndani ya kitivo hiki cha waelewa nafikiri ni vyema tukaanzia hapa.kwamba ridhiwani tunayemjua anafanana hivi. na ni imani yangu kuwa kidogo kama sio kwa msaada swali '' HUYU RIDHIWANI NI NANI, ANAZUNGUMZA KAMA NANI NA ANAFANYA HIVI KAMA NANI LINAWEZA KUWA LIMEPATIWA JIBU''

  MNYONGE MNYONGENI, LAKINI HAKI YAKE..................................
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Know one can write this unless he is Ridhwan Himself

  Mbaya zaidi umekuwa kama wasifu wa marehemu!! unajichulia dogo,

  Tunachojua ni kuwa ulikua na nafasi nzuri ya kuonyesha uko tofauti na baba yako, Okonkwo alifanya hivyo!! umeonyesha wewe na baba yako akili moja, kumbuka baba yako anamaliza urais 2015 tu, baada ya hapo, pray that opposition wont win! wakishinda dogo una wakatii mgumu sana.

  usije sema sikukueleza
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unasema Ridhwani atakuwa na wakati mgumu baada ya baba yake kumaliza kipindi chake ha URAIS mnamo 2015?
   
 4. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Huyu ametumwa nini?
   
 5. m

  malamba Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unasema Ridhwani atakuwa na wakati mgumu baada ya baba yake kumaliza kipindi chake ha URAIS mnamo 2015


  Lewinski Ms Unajifanya hujui kama Mumeo fisadi. mwisho wao unakaribia, Hakuna malefu yasio na ncha.
   
 6. B

  Babasean Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeona jana akiwa anatoa tamko la UVCCM kuhusu yaliyotokea Arusha. Je yeye ni Mwenyekiti/Katibu/Mtunzahazina/Msemaje/???? wa UVCCM?
  Mbona kila UVCCM wanatoka hadharani yeye naye hakosi? na huwa msemaji mkuuu? Jamani hiii ikoje? Hawa wenzetu wakoje? Hii ni nchi ya kifalme? Nijuzeni nafasi ya Ridhiwani ktk UVCCM zaidi ya kuwa mjumbe tu wa UVCCM
   
 7. s

  smz JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haka kajamaa kana kiherehere tu, hakuna lolote, popularity haitafutwi hivyo,
   
 8. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kumbe sehemu kubwa ya maisha ya mtu huyu yamejaa 'kihelehele'!

  Ungeendelea mbele zaidi kutueleza anapata wapi pesa zinazosemekana kutumika kujenga majumba Dar, na vituo vya mafuta Morogoro. Siyo mwizi kweli?
   
 9. s

  smz JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halafu hakawezi kuchanganya na za kwake!! hiyo CV hata mtoto wa drs la 7 anagundua kuwa kaandika yeye mwenyewe. hata kama ni hivyo kweli, SO WHAT??? Tufanyeje sasa?? unataka ur@#%?? au?? Mfuate mshikaji wako, boss wako wa zamani Masha
   
 10. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  He has a done a very early political journey !...that I agree, he is a committed ccm member ! That has no doubt.....hongera Riz1.
   
 11. T

  The Future. Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtoa mada atutake radhi, kwanini anatuita sisi wajukuu zake?ana uhakika kua ana uwezo au umri mkubwa wa kuwazaa wazazi wetu?je anajua umri wa kila mwana jamvi?mi yangu ni hayo. NB.umesahau kutupa matokeo ya perfomance yake kuanzia shule ya msingi hadi chuo, anzia na madaraja aliopata na alama za ufaulu wake. Otherwise sijavutiwa na cv hiyo.
   
 12. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hayawani Kiwete?
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Chief vipi umekuwaje?
  Mambo mengine bana huwezi mwambia mtu mzima.
   
 14. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kutangazwa matokeo, Kila wakati jina lake lilikuwa halisomwi. Huyo Aziza bahati yake kama viini vya urithi vitakuwa vimechomoka toka upande mwingine.
   
 15. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145

  Aisee ulelenga kweli, unajua wakati nacoma hii post nilikuwa najiuliza hv ni nani anaweza kukumbuka historia ya tu mwingine kiasi hiki!! hata nucta? dah, isipokuwa ni yeye mwenyewe!! he, himself can do this!!!

  Chief Masanja.... hahahahahahah Makubwa haya
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ana sifa ya kushiriki kikamilifu kwenye upuuzi wa baba yake na lichama lao mafisadi kupora hata ya msingi ya watanzania siyo? Hana unyonge ni mbumbumbu tu
   
 17. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ana sifa ya kushiriki kikamilifu kwenye upuuzi wa baba yake na lichama lao la mafisadi kupora hata ya msingi ya watanzania siyo? Hana unyonge ni mbumbumbu tu
   
 18. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Basically I feel sorry for the boy, because the same thing that he thinks will get him kwenye 'KITI CHA ENZI' is what will prohibir him from the same. Because Kikwete is going to have such a shit legacy (and unless there is somekind of religious conflict in the next 25 years).. Kikwete will f@ck up and have no legacy and as a result he will never get a chance. He's screwed before he even begins... TOO BaD.. If your father is President, make sure its GHANDI...lol not Mobutu or STALIN..
   
 19. L

  LAT JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu.... kubali tu kuwa mjukuu kwa mtoa mada.... na hii ni kweli kabisa ukizingatia maisha ya humu JF....check your status... Join Date: Jan 2011...check his status.. Join Date: Feb 2007........ he is old here at JF
   
 20. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  tusipoangalia Kikwete atatubadilisha tuwe kama congo, china etc
   
Loading...