Nani huyu Ridhiwani Kikwete?

Nani huyu Ridhiwani Kikwete?

"Great Minds Discuss Ideas; Average Minds Discuss Events; Small Minds Discuss People."... Naomba leo niiweke pembeni kidogo hii quote, ili nichangie, afterall he is a public figure.

Actually thruought my academic years at mlimani, nilikua najua tu kuwa Ridhiwani ni mtoto wa Raisi na anasoma sheria. Nothing more. Then alipomaliza chuo, ahead of me, nikaanza kumsikia more than usual, kumbuka nilikua nae chuo kimoja ila nilikua simsikii, lakini kaondoka chuo, yaani kaenda even further from me, halafu naanza kumsikia through the media. that is really questionable. Dont blame me for my bias-ness. Watoto wote wa viongozi au public figures are expected to do more, atleast kuonyesha some agressve-ness and seek their personal portion, contribution and potential ili hata mtu akisema we bwana si ulisaidiwa, unao uwezo wa kujibu, sawa sikatai nilisaidiwa hili na hili kwa sababu sio kosa langu kuzaliwa hivo lakini hata mimi binafsi nilifanya hili na hili. LABDA TUMSIFIE KWA KUTOKUDISCO NA KUTOKUWA NA KASHFA CHUONI. MAN THIS CREDIT IS ALL I CAN GIVE HIM and this by the way has nothing to do with leadership.

Oooh nilisahau kusema pia niliendelea kumsikia zaidi baada ya kutangaza kuoa kwa sababu alimuoa Arafa, jirani yetu Makumbusho... she is a nice girl though, if you get to know her.

Juzi through Michuzi nimeona January Makamba akitangaza website yake ya watu wa Bumbuli, January Makamba.com, nilienda kusoma historia yake. I must say that, huyu ndugu yeye nilikua namsikia sikia ila na yeye ni baada ya kulauch in to politics, ila watu wakawa wanasema " kuna watu wamesoma nae huyu Galanos na Forest Hill, he is a hard worker". This is according to people, but atleast there was something to hear. Sasa nilioenda kusoma story yake, sawa i was still biased, kwa sababu yeye ni mtoto wa kiongozi, ila kama nilivosema mwanzo ndani ya nepotism and favouritism, you still see kuwa huyu mtu hata kama angekua hana vitegauchumi na hizi ngazi zote, asingeaibika. Alivoona jina lake halikutokea form 4, kama mtoto wa kiongozi there were still so many options to explore, ila alienda forest hill akawa anasoma A-level na kureseat at the same time, huyu alikua na vision yake ya kutokuharibu mambo, so hata kama uwezo alikua nao, sehemu zilizomuhitaji ainame uvunguni he did so. Pia wakati anasubiri kuingia chuo, alienda kasulu kigoma kwenye refugee camps kufanya kazi kama registration clerk, haya basi alitaftiwa lakini the descriptions of what He did there single him out. Kwani kazi za Dar zilikuwa zimeisha, ni malengo tu, mi skatai kusaidiwa, maana hata mimi ningezaliwa na Raisi, jamani hiyo haina ubishi ningesaidiwa tu, but there is that additional quality that no one can add, and Ridhiwani lacks this a big deal. *Ila hakutaja form 6 alipata ngapi, kasema tu I succeeded. hehehe...Sijui alifeli zaidi ikabidi aende marekani? Mi sjui.Pia kasema ile kazi ya kasulu ilimpatia fedha flani akapata na scholarship ambayo hajaitaja, akapata ada za kwenda kusoma Marekani, pia huko anasema aliosha wazee, kuangalia wagonjwa....*

Haya, Kaenda Marekani kwa mashaka, sawa, lakini kafight mpaka kapublish, wangapi masters wanamaliza bila kupublish. Pia alipata internship at the Carter Center, na kupelekwa Sierra Leone(Je Baba yake pia alichangia hili?). Yaani anaonekana ana extra energy, this you cannot take away from him..

Nishiie hapo wasijesema..Ooh we una m-campaignia.. jamani ni coincidence, nilivosoma humu kuhusu Ridhiwani nikakumbuka nilivosoma ile historia ya January.. Sio kwamba January is perfect, but there is this clear difference between them.
 
kila mtu anamtazamo wake kwa kila jambo na ana haki ya kuwa nao na kuutetea. Kwanza thead ni nzuri kwa ajiri ya kutoa picha kamili ya huyu kijana ingawa CHIFU MASANJA hakuandika upande wa kazi alizofanya mbali ya siasa. Otherwise, kwangu its fine na nimeweza kujua huyu kijana kwanini anang'ang'ania siasa
 
Kikwete namlaumu kwa kushindwa kumpa mikogo Ridhwani ingawa tunasikia wakati wa 2015 Jimbo la BAgamoyo ANAPEWA RIDHWANI na kuna warabu washaahidi pesa za kuhakikisha Ustadh Ridhawan ndio mwinyi wao huko Bwagamoyo hapa ndio anaanza safari yake na kupigiwa Kampeni na Baba anaemaliza Urais.
Ridhwani kama angekuwa smart boy angesubiri Urais wa baba yake uamlizike ndio aoneshe kipaji chake sio ujiko wa BABA.
 
habari za leo wajukuu zangu?

ni kwa kipindi kirefu kweli nimeshuhudia huu mjadala juu ya huyu kijana mwenzenu! kama ilivyo ada yangu, leo nimeamua nijitokeze tena; pamoja na mambo mengine mengi ambayo yametokea hapa karibuni na mwaka huu mpya leo nataka nieleze kwa ufupi juu ya huyu kijana na jinsi ninavyo mjua mimi.........

RIDHIWANI KIKWETE,kama wengin wanavyomjua alizaliwa katika hospital ya wilaya ya bagamoyo tarehe 16 mwezi wa NNE mwaka 1979. kijana huyu alizaliwa toka kwa mama AZIZA bint SABURI na baba JAKAYA MRISHO KIKWETE.

RIDHIWANI ni kijana wa kwanza kwa wazazi hawa na alifuatiwa na mdogo wake anayejulikana kwa jina la SALAMA ambaye kwa sasa ni daktari na mwalimu pale MUHIMBILI chuoni.

kijana huyu alianza shule ya msingi mwaka 1987 pale shule ya msingi MATANGINI,nachingwea mkoa wa LINDI.sababu kubwa za yeye kuanza shule huko ni kazi aliyokuwa akifanya baba yake kipindi hicho. ikumbukwe kuwa bwana Kikwete alikuwa katibu wa CCM ,wilayani hapo. mwaka mmoja baadae, bwana ridhiwani na baba yake waliamia MASASI,mkoa wa MTWARA.akiwa huko alijiunga na shule ya MKOMAINDO kwa masomo yake ya darasa la pili kabla hawajarudi DAR ES SAALAAM, mwaka1989 ambapo alijiunga na shule ya FORODHANI iliyopo maeneo ya posta ya zamani hadi alipomaliza darasa la saba.

masomo ya sekondari aliyapata katika shule ya SHAABAN ROBERT na baadae MKWAWA mkoani IRINGA kabla ya kurudi DAR ES SALAAAM kwa ajili ya elimu ya juu katika CHUO KIKUUU CHA DAR ES SALAAM, sehemu ya mlimani na baadae ENGLAND,kwa masomo ya cheti cha elimu ya juu.

KISIASA
kisiasa kijana huyu alianza akiwa mdogo sana.historia inaanza akiwa nyumbani kwao na babu yake pale bagamoyo, ambapo alishiriki katika shughuli za kucheza gwaride kama chipukizi wa chama na hata alipokwenda huko NCHINGWEA NA MASASI aliendelea na shughuli za kucheza gwaride la chipukizi wa chama cha mapinduzi.

mwaka 1992, alikuwa ni mmoja kati ya vijana walioshiriki kama wajumbe kwenye mkutano mkuu wa chipukizi wa ccm taifa uliofanyika mbeya ambao ulimchagua bwana RAYMOND MANGWALE kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa. ( ikumbukwe bwana RAYMOND ni katibu wa UV-CCM, mkoa wa DODOMA ,kwa sasa). hata hivyo pia, wakati wa enzi hizo za masomo ya shule ya msingi, ridhiwani atakumbukwa kama kijana aliyechangia hela nyingi kwenye mradi wa mabasi ya UV-CCM na hata kupeWa nishani na RAISI mstaafu wa AWAMU YA PILI, ALHAJI ALLY HASSAN MWINYI katika viwanja vya KARIMJEE sherehe ambazo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali na viopngozi wa serikali.

wakati yupo sekondari aliendelea kuwa mwana harakati wa kawaida pale shuleni DAR ES SALAAM na hata baadae IRINGA.Waliosoma naye iringa wanakumbuka pilika zake na wenzake katika siasa za wanafunzi ,na michezoni.alikuwa mcheza mpira mzur sana enzi hizo.sijui siku hizi kama anacheza au bado.kumbukumbu zinaonyesha ushiriki wake katika kampeni za kufanikisha wenzake kupata nafasi za uongozi.

wakati akiwa chuoni, alikuwa mstari wa mbele katika siasa za DARUSO. RIDHIWANI amewahi kuwa katibu wa serikali ya wanafunzi, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA WANAFUNZI WANAOTOKA NCHI ZA NJE, na baadae alikuwa MBUNGE MWAKILISHI TOKA KITIVO CHA WANAFUNZI WA SHERIA, kabla hajawa MWENYEKITI WA DARUSO-KITIVO CHA SHERIA.

katika kipindi hiki tumeona alivyokuwa akishiriki katia siasa za wanafunzi na hata kushirikiana na wenzake kuhakikisha kuwa yale mambo wanayoyataka katika mazingira ya chuoni hapo yanakuwa vizuri.

Wakati yupo chuoni, akiwa mwaka wa tatu, 2002 aliteuliwa kuwa MUHAMASISHAJI WA UVCCM-wilaya ya BAGAMOYO.ikumbukwe kipindi hiki ni kipindi bwana SAIDI MTANDA ambaye kwa sasa ni MBUNGE WA JIMBO LA MCHINGA,LINDI alikuwa ndiyo MWENYEKITI WA UVCCM wilaya ya bagamoyo.ufanisi wa bwana RIDHIWANI katika mambo ya shughuli za vijana ikiwemo kushirikiana na wenzake kufanya makambi ya kuwaandaa vijana kwa shughuli za jumuiya na mchango wake ulimpelekea kuchaguliwa 2004 kuwa MJUMBE WA BARAZA LA UVCCM-PWANI.ikumbukwe kuwa kipindi hiki mwenyekiti wa vijana mki=oa wa pwani alikuwa BW.KULWA SAID.

katika uchaguzi wa ndani wa CCM , mwaka 2007 bwana RIDHIWANI lichaguliwa kwa kura nyingi , tena kwa kuongoza kwa wingi wa kura kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA (nafasi abayo anayo hadi sasa).Pamoja na hillo pia RIDHIWANI katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 lichaguliwa na vijana wenzake wa wilaya ya BAGAMOYO kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA UVCCM-TAIFA na pia MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM YA WILAYA -BAGAMOYO.

nafasi ya ujumbe wa halmashauri ya ccm ya wilaya , inampa nafasi ya kuwawakilisha vijana wenzake ndani ya vijao vya chama ngaz ya wilaya. mwaka 2008 alichaguliwa kuwa MJUMBE WA BARAZA KUU LA VIJANA TAIFA kuwakilisha UVCCM-PWANI na kabla kikao cha baraza kuu akijamchagua yeye kuwa MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM-TAIFA.

RIDHIWANI amekuwa akishiriki katika shughuli za vijana kila siku. kama walivyovijana wengine amekuwa mstari wa mbele kukitetea chama chake cha CCM na pia sera zake. ameshiriki katika mambo yanayohusu vijana wenzake katika makundi mbalimbali hasa yale ya wanafunzi,wanamuziki,wanamitindo,walemavu na mengoineyo mengi.

Kichama ameshiriki kwenye mambo mengi hasa ili la kampeni za chama safari hii. yeye na wenzake akiwemo MAKAMU MWENYEKITI, KATIBU MKUU,NAIBU KATIBU MKUU na wengineo ambao waligawanyika katika makundi mbalimbali wakikinadi chama chao.kubwa zaidi ni jinsi walivyojipanga vijana hasa kukisaidia chama chao kirudi lakini Ukiacha yote ni jinsi kijana alivyokuwa mstari wa mbele kuhahakikisha mambo yanakuwa mazuri.

RIDHIWANI amewahi wakilisha nchi yetu katika mikutano mbalimbali toka akiwa mtoto. mtakumbuka mkutano wa watoto ,ROME 1992, YES-SUMMIT MEXICO 2001,PANEL ON ENVIRONMENTAL SINGAPORE 2005,COMMONWEALTH YOUTH ORGANISATION MALTA 2007- YES-AFRICAN CAUCAS LESOTHO 2006, DEVELOPMENT AND CHALLENGE FACING RULLING PARTIES-SOUTH AFRICA 2008 na mengineyo mengi

RIDHIWANI ameoa na mungu amemjalia mtoto mmoja wa kike anaitwa AZIZA.

ni imani wajukuu zangu sasa mnamuelewa kidogo RIDHIWANI.tunapojadili ndani ya kitivo hiki cha waelewa nafikiri ni vyema tukaanzia hapa.kwamba ridhiwani tunayemjua anafanana hivi. na ni imani yangu kuwa kidogo kama sio kwa msaada swali '' HUYU RIDHIWANI NI NANI, ANAZUNGUMZA KAMA NANI NA ANAFANYA HIVI KAMA NANI LINAWEZA KUWA LIMEPATIWA JIBU''

MNYONGE MNYONGENI, LAKINI HAKI YAKE..................................

Qui bono?

Wasted
 
Inawezekana kijana R1 ana makosa na hii ni kawaida kwa binadamu kuwa anastahili kulaumiwa. Tukitenganisha hizi lawama anazostahili na zile ambazo analaumiwa kwa makosa ya baba yake hatutendi haki.
 
unauliza pesa anapata wapi!! kwani nani mwenye tenda ya kuingiza VX,V8 si riziwan,mbona hii iko wazi!
 
So what!!?? Hakuna shaka kwamba hiyo CV imeandikwa na ridhiwan mwenyewe, sina hakika kama kuna mtu anyefahamu njia aliyopitia ridhiwan kama alivyoiandika yeye mwenyewe au mzazi wake. Naona baada ya kuandamwa kwa muda mrefu sasa ameamua kujisafisha na kutafuta sifa. Ukweli unabaki palepale kwamba ridhiwan kaisha haribu na mpaka sasa tayari amejijengea maadui wengi sana katika safari yake ya kisiasa. Am doubt whether ridhiwan will succeed in politics after the retirement of his father.
 
unauliza pesa anapata wapi!! kwani nani mwenye tenda ya kuingiza VX,V8 si riziwan,mbona hii iko wazi!

Si hayo tu, pia ana vijikampuni kadhaa vya kuleta mafuta toka uarabuni pamoja na magari makubwa ya kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani, msiniulize pesa kapata wapi lakini wanasema kuwa hilo ni pande limepigwa na baba yake na kuweza kukopesheka yeye na rafiki zake huku wakiwa na uhakika wa kupewa tenda kwa mgongo wa Dady JK... halafu hebu jiulizeni kuwa kwa nini siku hizi akina type ya Davis Mosha hawachezi mbali na Riz?...ni kwa sababu ya uhakika wa biashara inayosimamiwa na mwana waukaya
 
Ni nani anashawishika na porojo hizi? Ili tuamini haya yote scan vyeti vyote weka jamvini. "Do not fool the inbornpeople" plz!
 
This country is creating divisions among ourselves walionacho na wasionacho by putting your son riz1 on front of the national page is quite dangerous and don't push tanzanians too far they are so humble people than any other nation in the world but now their about to say enough is enough. Kwakuwa usalama wa taifa na other government machineries huwa zinajitahidi kukushauri juu mwenendo wa uongozi lakini wewe umekuwa mbishi sijui ni sababu ya kuwa upeo mdogo wa kupambanua mambo yaani kuupusha viji-bomu mfano hit-man rebel groups ambao tayari wameanza kuiangamiza mbezi zote mbili kwa mfano wezi wa usiku na vibaka ni rebels na hitmen wa aina ya kisasa kwani hawana njia mbadala ya ku-share cake of the nation kwani mianya yote imezibwa na wachache ambao ni maswaiba wako na kushindwa kutekelezaa ilani ya chama.
 
Back
Top Bottom