Nani atakayetegua hiki kitendawili cha Nabii?

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,483
5,812
UZI HUU SIO WA KIDINI LICHA YA KWAMBA IMETUMIKA MIFANO KUTOKA KWENYE VITABU VYA DINI, HIVYO NAOMBA USIPELWKWE KWENYE JUKWAA LA DINI.

Waislamuini Korani na Wakristo wanaiamini Biblia, wote wanaungana katika hili simulizi moja la mwanzo wa mwanadamu. Wote wanakiri kuumbwa kwa Adamu, wanakiri kuumbwa kwa mkewe, pia wanakiri kuhusu anguko la mwanadamu. Wote wanaikiri Gharika na wanamtaja Nuhu mjenzi wa Safina.
1. Wote wanakiri kuitwa ama kuteuliwa kwa Ibrahimu aliye Baba wa Waisraeli na Waarabu, waumini wa hizi dini mbili wanakiri kuitwa (kuteuliwa) kwa Musa kwenda kuwakomboa “Bana Israel” (wana wa Israeli) kutoka utumwani Misri.
2. Lakini wanaishia kwa Musa, wanapoendelea mbele wanaachana njia panda, kila mmoja anachukua mwelekeo wake, mkristo anakwenda kivyake na mwislamu anakwenda kivyake. Biblia imetungwa kivyake na Korani imetungwa kivyake, tukitumia neno kuandikwa, basi Biblia imeandikwa kivyake na Korani imeandikwa kivyake.
3. Historia ya Biblia ilivyowafikia Waafrika wa leo na historia ya Korani ilivyowafikia Waafrika wa leo inajulikana. Ukweli unaodhihirishwa ni kwamba walioandika Biblia hawakukaa pamoja na hao walioandika Korani hadi kusababisha simulizi nyingi kufanana.
4. Historia ya Biblia na Korani zilivyowafikia Waafrika haionyeshi kwamba waandishi walikaa pamoja kuandika yanayofanana. Hapa ndipo ujumbe wa vitabu hivi unapopata nguvu kwa hao waviaminio, kwamba Yusufu anayetajwa kwenye Biblia pia anatajwa kwenye Korani, kisa kilichosababisha afungwe na habari za mke wa mtu zinarandana. Ilikuwaje?
5. Ilikuwaje Musa atajwe kwenye vitabu vyote viwili vya waandishi tofauti lakini visa, matukio na masimulizi yarandane kama kwamba ilitokea waandishi wa upande mmoja kutazamia ya upende mwingine?
6. Simulizi zinazohusu mwanadamu kuanzia Adamu hadi Gharika haziishii kwenye Biblia na Korani tu, bali vipo pia kwenye maandishi ya kale ya Wababeli (Wababiloni) na Wamisri wao waliitamka “Masri.” Zipo simulizi zinazofanana na yaliyoandikwa kwenye Biblia na Korani.
7. Kwenye maandishi ya Wababeli “Wababiloni” kuna simulizi zinazofanana na kisa cha kwenye Biblia Adamu hadi Nuhu. Tofauti ni majina tu ambapo Biblia inapomtaja Adamu, Wababeli wanamtaja “yule kijana.” Biblia inapomtaja Nuhu simulizi za Wababeli zinamtaja Anastasha.
8. Huko nyuma ulikuwahi kutokea mvutano wanazuoni wa zamani wa Misri “Masri” na Babeli “Babiloni.” Wapo waliodai kwamba kwenye simulizi ya kisa cha Adamu hadi Gharika ya Nuhu, Nabii na Mtume Musa alinakili kutoka kwenye maandishi ya Wababiloni yanayoelezea kisa cha “yule kijana hadi gharika ya Atanastasha” tofauti ni majina tu.
9. Kwenye hiyo “mythology” ya Wababeli kuna simulizi kuhusu Miungu na wanadamu. Wababiloni kama walivyokuwa Wamisri, nao waliamini juu ya miungu wengi waliokuwa chini ya uongozi wa Mungu mkuu mmoja. Hao miungu walimtengeneza kijana wakamweka kwenye Bustani iliyokuwa na matunda ya kila aina. Lakini kilichotokea mmoja wa miungu ya kike alimzimia huyo kijana akataka kulazimisha aoelewe naye.
10. Miungu wenzake walimshangaa wakamwambia haiwezekani yeye aliye kwenye daraja la uungu kuolewa na kiumbe aliye daraja la chini! Hata hivyo huyo mungu mke mapenzi yake kwa kijana yule yalizidi ufahamu wake.
11. Kwahiyo ili kuihujumu nia ya huyo mungu mke, miungu wenzake wakamtengenezea huyo kijana mwanamke (msichana) aliyefanana naye. Kuanzia hapo huyo Mungu mke akawa mwenye chuki kali dhidi ya msichana na adui wa kijana. Pia kuanzia hapo utii wa kijana kwa miungu ulipungua siku baada ya siku.
12. Huyo kijana alipotengenezwa alipewa kazi za kufanya, lakini wanadamu walipoongezeka waliziacha kazi alizopewa baba yao wa kwanza, wakafanya kazi zao wenyewe. Baya zaidi kila walipoongezeka duniani walikuwa wanapiga kelele hadi Miungu ilikosa usingizi.
13. Ndipo Mungu mkuu akaagiza wote waangamizwe kwa gharika, lakini miungu wengine waliokuwa chini yake walimmegea siri hiyo Anastasha akatengeneza safina.
14. Baadaye ghadhabu za Mungu mkuu zilipopoa, alitaka watengeneze tena kiumbe mwingine wa kukaa duniani, ndipo wenzake wakamwarifu kwamba walimficha (walimhifadhi) Atanastasha, Mungu mkuu akamwita naye akaitika, akatoka kwenye safina.
15. Hata ujenzi wa mnara, Wababiloni wanasimulia tofauti, kwamba walioujenga walikusudia kujihami dhidi ya ghadhabu ya Mungu. Walihofia ikiwa watamuudhi, akaamua tena kuwaletea gharika nyingine wasiangamie.
16. “Mythology” ya Wayunani kuhusu mtu aliyeishi kwa furaha, inarandana na ya Wayahudi kuhusu bustani ya Edeni. Jina la Adamu linatokana na neno la Kiebrania “Adamah” linalomaanisha udongo mwekundu wa mfinyazi, waliamini mwanadamu alifinyangwa kutoka kwenye udongo mwekundu wa mfinyanzi, akapuliziwa pumzi ya uhai (uzima wa Mungu) ndipo akawa nafsi hai.
17. Wayunani wana kisa cha mtu aliyeitwa Pandora na zawadi ya kasha la ajabu lililompa furaha, alitunukiwa kasha hilo kwa sharti kwamba asilifungue. Lakini kadri mtu alivyopata raha ndivyo alivyozidi kupata hamu, akitamani kujua kilichokuwamo kwenye kasha na kilichompa furaha ile.
18. Mwishowe uvumilivu ulipofikia kikomo, alifungua hilo kasha, kitu cha kwanza ilichotoka ni mauti, ikamwondolea furaha yake. Yalifuatia mabaya mengine ambayo mtu hakuweza kabisa kuyarudisha tena kwenye kasha. Kisa hiki ndio chimbuko la usemi wa kisheria “opening the pandora box” wanaopendelea kuutumia wanasheria wetu wanapohami jambo wanalodhani litakuwa na athari mbaya kisheria.
19. Kwenye somo la Mythiology na Egyptology sikukutana na dhana ya kiafrika kuhusu uumbaji wa Mungu na mwanadamu, hiyo iliniongezea na mashaka. KWANINI ziwepo dhana za wazungu (warumi na wayunani), wamisri, waashuri, wababeli, waisraeli na waarabu tu? Ni kweli Waafrika hawahusiki na Mungu wala uumbaji wake?
20. Lakini nilipokuwa nikiendelea na utafiti wangu wa Amani na migogoro barani Afrika (1982 – 1997) nilipata mengi kwenye nchi ya Zaire (DRC). Kwa mara ya kwanza niliijua dini ya M’bantu iliyoitwa “Alabba” na Mungu wao waliyemwita “Nkoyi.”
21. Tanzania tuna mengi ya kujivunia tukiirejea historia ya M’bantu kwani makabila mengi ya Tanzania chimbuko lao ni M’bantu. Kabla ya uvamizi wa wazungu na waarabu, Waafrika walijitosheleza, walikuwa na maandiko yao, dini yao na kalenda yao iliyokuwa na majina ya siku na miezi.
22. Watanzania tusijichukulie kirahisi, kwenye ngao yetu ya Taifa kuna picha ya mwanamume na mwanamke aliyefunika kichwa chake kwa vazi asilia linalofanana na “hijab.” Wote wawili wanashirikiana, ile ndio dhana ya M’bantu kwamba “Nkoyi” alimuumba mtu mume na mke, waliumbwa ili washirikiane.
23. Kuna kabila chache za Kaskazini ambazo chimbuko lao linatoka nje, Wachaga walitokea Ethiopia. Lakini huko walipitia tu, chimbuko lao walitoka kabila ya Bejamin lililopo Israeli. Wamasai na Watutsi walitokea Misri, ndio maana huko Uganda Burundi na Rwanda wanaitwa Wahima, katika Tanzania makabila mengine waliwaita “Wahumpha.”
24. Lakini maneno Wahuma na Wahima yanatokana na “Hamitic” au uzao wa Hamu. Msamiati wa “Nilotic” ulitokana na ukweli kwamba hao wahamiaji kutoka Misri walifika Afrika ya mashariki na ya kati wakifuata mto Nile.
25. Wabarabaig, Wahadzabe (Watindiga), na Wairaq walitokea mashariki ya kati Iraqi. Wajaluo, walitokea Nigeria kwenye jimbo la Kano, nao walifika Afrika mashariki wakisafiri kando ya Nile. Kila mahala walipotua kuanzia Sudan, Uganda, Kenya hadi Tanzania, wameacha alama ya majina yao yanayoanzia na “O”
26. Nigeria akina Obasanjo, Obi, Ojwuku, Okalla, Okownko n.k. Uganda hawaitwi Wajaluo wanaitwa Waacholi na Walang’o ndio akina Okello, Obote, Oyite n.k. Tanzania na Kenya ndio akina Oginga, Omolo, Otieno n.k.
27. Kwenye historia ya M’bantu kuna mengi ya kusisimua, chimbuko lake ni Katanga (nchini DRC), dini yake iliitwa “Alabba.” Ukweli kuhusu utawanyiko “the bantu migration” unatofautiana na walichotuandikia wazungu, maana wamepotosha makusudi ili Mwafrika asijue alikotoka, asijue amefikaje hapo alipo, wala asijue ameufikiaje unyonge wake wa sasa, yakiwemo maradhi ya kutokujiamini.
28. Huu ndio ukweli kuhusu Wabantu, Baba yao alizaa watoto 20. Zamani niliyaandika hata majina yao, ila “muniscript” za hicho kitabu changu zilipotelea gerezani Ukonga. Siku moja ilitokea “special search” ambapo wafungwa tulipigwa, virago vyetu vilitawanywa na selo zilimwagiwa maji, kurasa za kitabu changu zikapotelea huko.
29. Baba wa Wabantu alipokaribia kufa aliwausia wanawe kuhusu nchi nzuri, iliyojaa neema, iliyozingirwa na maji mengi. Sijui kama huyo Baba aliiona Paradiso katika roho, ama aliona nchi halisi iliyo duniani, lakini ukweli unabaki ulivyo, kwamba Wabantu walitawanyika, kila yalipowatokea mabalaa kama ya ugomvi (vita) vya wenyewe kwa wenyewe, njaa ama magonjwa yasiyotibika.
30. Walikimbia (walitawanyika) ili kuiendea nchi njema waliyoahidiwa na Baba yao, ndio asili ya makabila mengi ya kibantu kuishi kando ya ziwa ama pembeni mwa mito.
31. Leo nakirejea kitendawili kutoka kitabu cha Waamuzi 9; 8 – 15. Waisraeli walikosea kumtwaza Ebimeleki asiye mwisraeli awe mfalme wao. Nabii akapanda kwenye jabali, akapaza sauti akisema; “nisikieni enyi watu wa Shekemu ili na Mungu naye aweze kuwasikiliza ninyi. Siku moja miti iliyokuwa kwenye Bustani ya Mungu ilitoka ili kuutia mafuta mti mmoja uwe mfalme wao. Iliuambia mzeituni tawala wewe uwe mfalme juu yetu, lakini Mzeituni ukajibu JE, niache mafuta yangu ambayo kwangu mimi watu wanamheshimu Mungu na wanadamu niende nikayonge yonge juu ya miti?”
32. “Kisha miti ikauambia mtini, njoo uwe mfalme utawale juu yetu, lakini huo mtini ukaiambia miti. JE, niache utamu wangu na matunda yangu mazuri niende nikayonge yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mzabibu njoo wewe utawale juu yetu. Huo mzabibu nao ukaiambia JE, niiache divai yangu ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu ili niende nikayonge yonge juu ya miti?”
33. “Ndipo miti yote ikaugeukia mti wa miiba, ikasema njoo wewe utawale juu yetu. Huo mti wa miiba ukaiambia miti, ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme wenu kweli? Mnatumainia nini? Mimi sina matunda! Lakini miti ikasema tutumainie japo kivuli chako.”
34. Mti wa miiba ukasema haya njoni msujudu chini ya kivuli changu. Mti wa miiba ukaifunika miti yote, miiba yake ikaingia kwenye kila mti. Ukatokea mnyukano, miti ikitaka kujitoa kwa nguvu kutokana na maumivu ya miiba.
35. Mnyukano ulipozidi ulisababisha mizizi ya mti wa miiba kung’oka kutoka ardhini. Lakini hakuna mti uliofanikiwa kujinyofoa, mti wa miiba ulikauka na mnyukano ulipoendelea ulisababisha kutokea cheche za moto zilizoufanya mti wa miiba kuanza kuungua moto. Huo moto ukaiteketeza miti yote ya Bustanini.
36. Nabii akahitimisha kitendawili chake akisema ikiwa mmefanya vyema kumtawaza Abimeleki, basi mtafurahi siku zote. Lakini kama mmefanya dhambi kumtawaza huyo mgeni, basi utazuka moto utakaowateketeza ninyi na Mfalme wenu!
 
Back
Top Bottom