Nani ataandamana?

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
SIONI taabu kwenye ishu ya kuandamana ila nataka kufahamu NANI ATAANDAMANA?

Ukiamrisha maandamano lazima uwe na mawasiliano na waandamanaji. Mawasiliano yenyewe ni nguvu ya muitishaji maandamano je ni kweli yeye ana nguvu hiyo? Anao ushawishi?

Na vipi Chama kinachoitisha maandamano nacho pia kina ushawishi huo?

Hoja ni Katiba sasa hebu chukua Watanzania wanne tu hapo Kariakoo waulize Katiba ni nini?

Je nini muunganiko wa Katiba na maisha yako ya kila siku? Yaani muuza ndizi soko la mahakama ya ndizi anaelewa kuwa akiandamana bei ya mkungu itapandishwa na Katiba mpya? Akikujibu jibu sahihi najitundika ghalfla nijiua.

Hivi kuna maandamano yaliyowahi kufanikiwa hapa nchini? Nitajie.

Maandamano na migomo kwa Tanzania bado kwasababu Siasa zetu hasa za upinzani zimetekwa na Wanasiasa kwa msingi wa kujineemesha kwanza.

Hivi kabla ya kuandamana kwanini wasingeomba fedha Kwa wafadhili wao jumlisha ruzuku wakapita kuelimisha wanachama wao nchi nzima kuanzia ngazi ya vijiji kuhusu umuhimu wa Katiba mpya.

Unamkurupusha mtanzania wa kule kijijini Ndungu Same aandamane kwa ajili ya Katiba mpya ataelewa kweli?.

Mimi maoni yangu WAITISHAJI MAANDAMANO mnayo nafasi ya kukaa na serikali kuona upande wa pili ili kufikia muafaka hamjachelewa. Rais alishafungua milango hiyo nadhani ni busara mkatumia fursa hiyo.

Ukiandamana ukifanikiwa Iko faida ila ikifeli hasara inakuja kwa mtu mmoja mmoja hasa manundu ya marungu na mbio ambazo hukupanga kuzikimbia.

Kifupi kuandamana bila kujua nini UNAHITAJI yaani kuandamana baada ya kusimuliwa na si kuelimiahwa ni aina mpya ya kichaa.

Watanzania wanauhitaji wa mambo mengi ya msingi tusiwaondoe katika reli ya kupambania mustakabal wao kwa kuwaingiza katika mitego itakayowaletea taharuki mpya isiyoonyesha mwanga wa hatima yao.

Uzoefu unaonyesha kuwa viongozi wa vyama wanapoitisha maandamano huwa hawashiriki kivitendo kwenye zoezi hilo, hiyo ni dharau nafurahi kuona safari hii wamesema wataleta familia zao zishiriki kuandamana kama ni hivyo kwanini basi zamu hii isiwe ya viongozi na watoto wao tu wananchi wa kawaida wakapumzika wakisubiri zamu nyingine?

Siku njema
 
Kwwli kabisa aana srikali yetu ni hatari tupu nani anajua maana ya katiba aseme ni wachache tena walio soma basi na hata walio soma wachache
 
Mara maandamano, mara mgomo, mara kususa na kuzira....

Maani ni zigzaga tu mara serikali 3, mara katiba, mara bandari, mara gharama za maisha yaani ni vulu vulu haijulikani uelekeo ni right, left or center...

Haijulikani dai la msingi ni nini...
maana dandia dandia ni nyingi, pinga pinga kama zote bila ata ya hoja...
 
Vyanzo vyangu vinaniambia, CHADEMA imepokea orodha kubwa ya wanachama watakaotoka mikoani kushiriki maandamano.

Usiishie Kwa kukariri.
 
Back
Top Bottom