Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
Kwangu Mimi ni hayati Baba was taifa.
Kwann?
Ni kipengele kimoja tuu cha kutuunhanisha kua kitu kimoja mbali ya utofauti was makabila yetu na dini.

Yeye ndiye aliyejenga msingi was umoja na mshakiamano wetu ambao viongozi was sasa wanatumia nguvu kuubwa kuvibomoa
 
unamuona wa kawaida, si ni kwa sababu ni mswahili mtu wa pwani, umezoea kumuona akitabasamu sana LAKINI mambo yake kwenye medani ya diplomasia na Amani barani Afrika ni makubwa.

Koffi Annaan na Mzee Mkapa walishafeli kwenye mediation yao huko Kenya, yaani mchakato wao ulishastall. Alipoingia JK kwenye hiyo process, mambo yalikwenda kama kumsukuma mlevi, Amani ikapatikana. Sasa unadhani huyo ni mtu wa mchezomchezo?

JK ni kichwa smart sana ambacho haters wanakichukulia poa
Hapa umepotosha na wewe siyo mtu makini. JK alikwenda kama Rais wa Tanzania tu ku deliver ultimatum ya USA na siyo busara zake ndizo zilimaliza ule mgogoro.

Hata wewe mwenyewe Missile of the Nation Au Paul Makonda mungekuwa ndiye Rais wa Tz wakati ule ungemaliza ule mgogoro tu.

Nampima JK uwezo wake kwa namna alivyoshindwa kumanage tofauti zake na Edward Lowassa, mpaka akaacha tukaangukia kwa yule SHETANI wa Chato
 
Hapa umepotosha na wewe siyo mtu makini. JK alikwenda kama Rais wa Tanzania tu ku deliver ultimatum ya USA na siyo busara zake ndizo zilimaliza ule mgogoro.

Hata wewe mwenyewe Missile of the Nation Au Paul Makonda mungekuwa ndiye Rais wa Tz wakati ule ungemaliza ule mgogoro tu.

Nampima JK uwezo wake kwa namna alivyoshindwa kumanage tofauti zake na Edward Lowassa, mpaka akaacha tukaangukia kwa yule SHETANI wa Chato
Pressure za Marekani kweli zilikuwepo, lakini siyo pressure ya Marekani pekee inayosolve migogoro mfano mmojawapo ni kuwa pressure ya Marekani ilifeli huko Somalia.

Kuna mambo ambayo JK aliyaleta kwenye mazungumzo, kwa mfano, aina ya serikali ya pamoja ambayo Wakenya wanaweza kuunda kama pande mbili hasimu wakizika tofauti zao.

cheki hii paper.
 

Attachments

  • THEROLEOFJAKAYAKIKWETEINTHEMEDIATIONOFTHEKENYANPOST-ELECTIONCONFLICTFINAL.pdf
    307.3 KB · Views: 2
Wapende wasipende historia itamkumbuka Magufuli kwa jinsj alivyoiokoa Tanzania na mataifa mengine yaliyoiga mbinu na falsafa yake kwa namna ya kupambana na corona!
 
Back
Top Bottom