Mkurya mweupe
JF-Expert Member
- Aug 10, 2023
- 218
- 740
CCM kama taasisi inayoshika dola na taasisi yenye miradi mingi kulinganisha na taasisi nyingine hasa vyama vya siasa . CCM imempa mwekezaji kujenga soko la CCM kisasa ,kiukwel ni nia nzuri ukiangalia ramani yake linaenda kuwa soko bora na la kisasa ukilinganisha na masoko mengi yaliyopo hapa nchini.
Mwekezaji aliyepewa tenda ya kuboresha hilo soko la CCM Katoro Geita alikubaliana na chama ajenge majengo hayo kwa mkataba wa miaka 9 ,ajenge soko hilo kwa kiwango kinachostahili huku CCM wenyewe wakijiridhisha kila hatua kuwa amejenga kwa kiwango bora ,huku mwekezaji akiwa na umiliki wa hilo soko ,means baada ya miaka tisa akiachie chama ,kiendelee na soko lake.
Ila kinachoendelea kwa sasa ni aibu hasa kwa taasisi inayoshikilia dola kama inashindwa kusimamia mradi wake wenyewe ,kujengwa kwa kiwango kinachostahili ,Je CCM kama taasisi itaweza kweli kusimamia miradi ya serikali mikubwa ?
Majengo yanayojengwa na mwekezaji ni ya kiwango cha chini ,bora mwanzo alianza vizuri ,ila kwa sasa kuna uwezekano ikifika miaka tisa ,anamaliza mkataba wake atakiachia chama magofu .
Kinachoshangaza kuna siku afisa miradi wa Chama wilaya ya Geita alifika katika eneo hilo akagomba sana akilalamika tofali za block zilizokuwa zinatumika kujengea, hata mtoto akipiga ngumi zilikuwa zina uwezo wa kuvunjika ,akaenda nazo wilayani na sample za tofali kureport, lakini alipofika huko akawa mpole kabisa ,ndo maana nikajiuliza kuwa chama Cha Mapinduzi mkoa wa Geita ,kinajihujumu au kinahujumiwa?
Kuna block moja ishakamilika inavuja mpaka Gypsum board zikamwagika ,ina maana kweli chama hakioni hilo ,mpaka wakaanza kuziba upya ,jengo lina miezi 4 ,linavuja ,mpaka linaanza kuzibwa upya ,je chama kikija kuachiwa kwa miaka tisa, si yatakuwa magofu, yaan nyumba zinabomolewa ili zijengwe za kisasa cha kushangaza zinazojengwa zinazidiwa na zilizobomolewa ,hii ni aibu kwa chama kama kinashindwa kusimamia miradi yake ,je kitaweza kusimamia miradi ya serikali kweli?
Kuna majengo ndo yanaendelea kukamilishwa yametumia board za kizaman baadhi ya vyumba badala ya Gypsum board Kama ilivyopendekezwa kwenye majengo ya kisasa ,na hizo board zote si za kununua ni za kutoa kwenye majengo yaliyobomolewa ,kiukweli ni aibu kwa Chama .
Chama Cha Mapinduzi inabidi kiwe mfano katika miradi yake isionekane kina ubabaishaji hadi harufu za rushwa katika ujengaji wake ,haiwezekani Afisa miradi anakagua tofali za block zinavunjwa kwa mkono ,anaenda nazo anagomba baadae anapiga kimya na tofali hzo hzo zinaendelea kutumika hzohzo .
Ona board za kuungaunga zilizotumika View attachment 2844770View attachment 2844771