Nani anaruhusiwa kuchanganya dini na siasa?

Nani anaruhusiwa kuchanganya dini na siasa?

Rais ambaye ni mwanasiasa huapishwa na Kiongozi wa Dini.
Vikao vya Kisiasa hufanyiwa dua au maombi na viongozi wa dini pindi wanapofanya vikao vyao.
Viongozi wa kisiasa ni waumini au washirika kwa viongozi wa dini (Yaani ni Baba zao wa kiimani)
Viongozi wa dini wanawajibu wa kushauri washirika wao ambao miongoni mwao ni wana-siasa,wafanyabiashara nk.
Viongozi wa Kisiasa wanapoapa hushika vitabu vya dini (kama hawataki Dini ziingie kwenye siasa washike bunduki)
Bado Viongozi wa dini ni walipa kodi za maendeleo hivyo lazima wahoji kama raia au wananchi.
 
Sio kweli, dini na siasa ni vitu viwili tofauti kabisa.
Ni kweli vitu viwili tofauti ila kazi ya viongozi wa dini ni kukemea maovu ktk jamii ikiwemo hayo yanayofanywa na viongozi wa kisiasa bila kujali ni upinzani ama chama tawala, tatizo la nchi hii Kuna watu wanajiona malaika wanataka kusifiwa tu hawataki kuambiwa ukweli pale wanapokosea sasa Maisha hayako hivyo wewe ni nani usikoselewe? Yaani unateka watu unawauwa kisa tu wamekukosoa unataka kiongozi wa dini akae kimya?

Kiongozi wa dini yeyote anayefumbia macho maovu ktk jamii huyo hafai kuwa kiongozi .
 
Japo tunawaona kama watu wawili tofauti, wanasiasa na viongozi wa dini ni kitu kimoja au niseme mapacha walioungana kiunoni. Ukitaka kuliona na kulijua hili angalia yafuatayo:

Wote, huvuna wasipopanda na kupanda wasipovuna. Mfano, wote wanatumia maneno hasa ahadi hewa na za uongo kuwaibia na kuwatuliza wafuasi wao na wahanga kwa ujumla. Wote hutoa ahadi zisizotekelezeka wala kuingia akilini. Wanasiasa uahidi vinono duniani wakati viongozi wa dini uahidi hivyo hivyo peponi. Wote si wana demokrasia. Wanahubiri maji na kunywa mvinyo, unafiki na uongo.

Wote wanawatoza watu fedha na kuzitumia bila kutoa kutaka wala kuwa tayari kutoa maelezo ya zinavyotumika. Wote wanapenda ujiko hata wasipostahili. Pia, chanzo cha dini na siasa ni kimoja, yaani vimeletwa toka ughaibuni kututawala na kutunyonya.

Viongozi wa dini wakisifia watawala, hii siyo kuchanganya dini na siasa bali uzalendo. Wakiwaapisha na kuwabariki, wanafanya vyema. Ila wanapoonya, wanachanganya dini na siasa. Wanasiasa wakichangia shughuli za dini, wanatimiza wajibu wao. Viongozi wa dini wakiwa machawa, ni sawa. Wakikengeuka na kuunga mkono wapinzani, wanachanganya dini na siasa. Kimsingi, dini na siasa vyote ni mifumo ya kikoloni ya kumtawala na kumpumbaza mwanadamu ili kumuibia na kumdhibiti.

Viongozi wakiwapumbaza waumini na kuwasihi waiunge mkono serikali mbovu siyo kuchanganya dini. Wakiwaaminisha wahanga wa jinai hizi kuwa umaskini wao ni wa kuumbwa, wanatenda vyema. Ila wakiwastua wadai haki, wanachanganya dini na siasa.

Wote hujifanya wajuaji hata kwa yale wasiyojua. Na katika hili, hawapendi wala kukubali kupingwa wala kukosolewa. Tuna mashehe waliojigeuza machawa na maaskofu waliokataa uchawa. Wote wanafanya siasa japo wana milengo na makundi tofauti. Kimsingi, dini na siasa vinalala kitanda kimoja na kufanya jambo moja. Hata ukiangalia ukoloni barani Afrika, bila dini, huenda usingefanikiwa haraka na kwa kasi kama iivyotoke

Kiukweli, hakuna kitu kinaitwa kuchanganya dini na siasa bali usanii na gea ya kuwachanganya wahanga wa jinai hizi za kujitakia tulizoletewa na wakoloni.
For sure
 
Back
Top Bottom