LazyDog
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 2,473
- 189
Hakuna haja ya intervention. Hiyo ni bubble tu. Nyumba zinakuwa ghali hasa sehem ambayo huduma hakuna kabisa. Wengi wanapenda kuishi maeneo ambayo angalau yana huduma. Tatizo hilo lipo hadi kwenye nyumba za kupanga. Kwa kuanzia ni kuweka huduma muhim maeneo mengi. Mf sasa hivi Mbagala kuna barabara, inamaana watu watahamia huko na kigamboni. Kwahiyo bei za nyumba zitapungua maana kutakuwa hakuna wanunuzi. Kwahiyo kinachohitajika kuzirudisha nyumba chini ni huduma muhim. Lakini pia kaufisadi nako kana sehem katika hili. Pesa chafu nazo zinafanya nyumba ghali zipate wanunuzi maana pesa za hivyo haziwekeki benki. Kwahiyo udhibiti wa pesa chafu nao unaweza kusaidia maana nyumba ghali zitakosa wanunuzi
Wadau wameelezea kuhusu tahadhari hali kadhalika opportunities. Ni wewe kuchagua upande upi ungependa kuwemo; mpangaji au mwenye nyumba.
Bahati mbaya sana mkulima anapangiwa, anaambiwa ni marufuku kupeleka mazao yako nje ya nchi.
Of course, wataletwa wazungu wa Africa kusini waje kuhodhi ardhi, wao hawatanyimwa kupeleka nje wakitaka. Watalima hapo mkoa wa Pwani, bidhaa zao za second class watapeleka sehemu kama pale GAME, first class itapelekwa nje.
Wakulima wazawa wa Asia sasa hivi wanalalama tu kwa yanayowasibu huko kwao!