Nani anapanga bei za nyumba Bongo?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
nani ana control biashara ya nyumba tanzania?? Ni kila mtu na uamuzi wake??

ni aibu tupu ukiangalia bei za nyumba za tanzania! Bei kubwa kuliko hata nyumba za ulaya! Bei kubwa hakuna barabara ya kueleweka? Umeme? Maji?

yaani sasa tanzania kila mtu anataka kuwa bilionea, nyumba mbovu bei balaa? Halafu mshahara wa mtanzania ni sh500,000 nani ataweza au wanauziana wao kwa wao mabepari????? Au internet ndiyo imeharibu mambo? Watu wanaangalia bei za nyumba za ulaya halafu na wao wanajiwekea??

serikali itaingilia lini kurekebisha hili tatizo? Thamani ya nyumba inabidi iendane na mazingira ya eneo ilipo! Sio mtu anajitungia tu bei yake halafu hata serikali haifaidiki chochote!! Tuache kuiga watanzania thamani ya nyumba na viwanja vyetu bado havijafikia vile vya ulaya hata kidogo!

tutengeneze barabara, tule umeme na maji, tupime viwanja kwa kutumia surveyors then tuongeze bei! Sio tunakurupukia tu fedha wakati hali ovyo! Watu ambao wananunua hizo nyumba kwa bei hiyo kali wana hatari kubwa kwa collapsing ya market kama ilivyotokea usa na australia sababu ukweli wenye uwezo wa kulipa kiasi hicho cha pesa ni kama 9% ya population yote!

later in future wakati wanataka kuuza nobody will buy those properties for the price they are asking! Its a very risk business



 
Last edited:
wadau hii post nimeikuta maeneo flani ikanifurahisha sana)) nami naiwakilisha
 
Last edited:
Hakuna haja ya intervention. Hiyo ni bubble tu. Nyumba zinakuwa ghali hasa sehem ambayo huduma hakuna kabisa. Wengi wanapenda kuishi maeneo ambayo angalau yana huduma. Tatizo hilo lipo hadi kwenye nyumba za kupanga. Kwa kuanzia ni kuweka huduma muhim maeneo mengi. Mf sasa hivi Mbagala kuna barabara, inamaana watu watahamia huko na kigamboni. Kwahiyo bei za nyumba zitapungua maana kutakuwa hakuna wanunuzi. Kwahiyo kinachohitajika kuzirudisha nyumba chini ni huduma muhim. Lakini pia kaufisadi nako kana sehem katika hili. Pesa chafu nazo zinafanya nyumba ghali zipate wanunuzi maana pesa za hivyo haziwekeki benki. Kwahiyo udhibiti wa pesa chafu nao unaweza kusaidia maana nyumba ghali zitakosa wanunuzi
 
Hao ndio watanzania bwana,
wakiambiwa wajenge hospitali bora,wawe na shule zenye waalimu walipe wafanyakazi vizuri,wawekeze kwenye miundombinu wanasema oh sisi ni nchi maskini,sisi ni nchi inayoendelea msitufananishe na marekani na Ulaya,rome haikujengwa siku moja,ilimradi vijisababu milioni kidogo!

sasa waambie mambo ya kipuuzi,kuuza nyumba as if wako Tokyo,or New York hapo ndio mabingwa!waambie wabunge wetu wachague magari ya kufanyia shughuli zao!utakoma,waambie bajeti za vitafunio na mambo ya kipuuzi,wanasahau umasikini wao na zile hoja za sisi ni dunia ya tatu!watakuambia sisi sio masikini,tuna madini na mali asili kibao!watakuambia usituletee elim yako ya kizungu hapa,watakuambia sisi ni "independent nation" we decide what is right for us.watakushushua kwa kila kijembe!

wananchi wa nchi hii ya Tanzania ni Reflection ya Viongozi wetu,nyumba yenye thamani ya millioni 40 itauzwa milioni 700 na kodi italipwa as if iliuzwa milioni 10.nchi hii ni very disturbed.
Sote tunafahamu kuwa katika nchi yenye Malaria,AIDS ya 30% rate,kipindupindu,umeme wa kubabaisha unatosha kabisa kufanya nyumba kushuka bei even below it's construction cost.

USHAURI,tiger countries unazojaribu kuiga sera zao sasa hivi,hawakuvutia wawekezaji kwa kufanya vitu vyao viwe ridiculously expensive but rather the opposite.
 
Last edited:
NANI ANA CONTROL BIASHARA YA NYUMBA TANZANIA?? NI KILA MTU NA UAMUZI WAKE??


NI AIBU TUPU UKIANGALIA BEI ZA NYUMBA ZA TANZANIA! BEI KUBWA KULIKO HATA NYUMBA ZA ULAYA! BEI KUBWA HAKUNA BARABARA YA KUELEWEKA? UMEME? MAJI?

YAANI SASA TANZANIA KILA MTU ANATAKA KUWA BILIONEA, NYUMBA MBOVU BEI BALAA? HALAFU MSHAHARA WA MTANZANIA NI SH500,000 NANI ATAWEZA AU WANAUZIANA WAO KWA WAO MABEPARI????? AU INTERNET NDIYO IMEHARIBU MAMBO? WATU WANAANGALIA BEI ZA NYUMBA ZA ULAYA HALAFU NA WAO WANAJIWEKEA??



Mdau J. KIONGOLI

1.Huo (kwenye kijani)Mshahara uNCLE ni wa Mtanzania kivipi? Una maana ni wa wastani au ndo minimum pay? Mimi ningedhani kwamba mishahara mingi ya wa-Tz iko kwenye range ya 250,000, kwa kuchukulia kwamba ajira iliyo kubwa kabisa hapa nchini ni ya waalimu wa Primary na Sekondary, achilia mbali zile za Private!

Hapo kwenye NYEKUNDU tena unanikanganya mjomba-kaka, unakuwa kama unacontradict sentensi yako ya awali.
 
Free market mzee. Wanaweza kuweka bei hizo kwa sababu demand na willingnes ya wateja kulipa ipo.
 
Supply and Demand ndiyo zinazopanga bei za Nyumba. Let the Market decide the price.
 
NANI ANA CONTROL BIASHARA YA NYUMBA TANZANIA?? NI KILA MTU NA UAMUZI WAKE??

NI AIBU TUPU UKIANGALIA BEI ZA NYUMBA ZA TANZANIA! BEI KUBWA KULIKO HATA NYUMBA ZA ULAYA! BEI KUBWA HAKUNA BARABARA YA KUELEWEKA? UMEME? MAJI?

YAANI SASA TANZANIA KILA MTU ANATAKA KUWA BILIONEA, NYUMBA MBOVU BEI BALAA? HALAFU MSHAHARA WA MTANZANIA NI SH500,000 NANI ATAWEZA AU WANAUZIANA WAO KWA WAO MABEPARI????? AU INTERNET NDIYO IMEHARIBU MAMBO? WATU WANAANGALIA BEI ZA NYUMBA ZA ULAYA HALAFU NA WAO WANAJIWEKEA??

SERIKALI ITAINGILIA LINI KUREKEBISHA HILI TATIZO? THAMANI YA NYUMBA INABIDI IENDANE NA MAZINGIRA YA ENEO ILIPO! SIO MTU ANAJITUNGIA TU BEI YAKE HALAFU HATA SERIKALI HAIFAIDIKI CHOCHOTE!! TUACHE KUIGA WATANZANIA THAMANI YA NYUMBA NA VIWANJA VYETU BADO HAVIJAFIKIA VILE VYA ULAYA HATA KIDOGO!

TUTENGENEZE BARABARA, TULE UMEME NA MAJI, TUPIME VIWANJA KWA KUTUMIA SURVEYORS THEN TUONGEZE BEI! SIO TUNAKURUPUKIA TU FEDHA WAKATI HALI OVYO! WATU AMBAO WANANUNUA HIZO NYUMBA KWA BEI HIYO KALI WANA HATARI KUBWA KWA COLLAPSING YA MARKET KAMA ILIVYOTOKEA USA NA AUSTRALIA SABABU UKWELI WENYE UWEZO WA KULIPA KIASI HICHO CHA PESA NI KAMA 9% YA POPULATION YOTE!

LATER IN FUTURE WAKATI WANATAKA KUUZA NOBODY WILL BUY THOSE PROPERTIES FOR THE PRICE THEY ARE ASKING! ITS A VERY RISK BUSINESS


Mdau J. KIONGOLI

Sasa si ununue tu huko ulaya mkuu? Yanini kuhangaika na Bongo? Waachie wenyewe wanaoweza.
 
Basi kila kitu wangekuwa wanaachiwa wenyewe nadhani tungekuwa hatuna la kujadili hapa
 
Bongo ovyo ovyo tu! Hatuna mambo ya fair market value kwa hiyo watu wanajipangia kiholelaholela tu hizo bei za nyumba.
 
Tatizo ni kuwa sehemu zenye vitu muhimu kama maji, umeme, barabara na usalama ni chache sana hivyo kila mtu anataka kuishi huko. Inabidi serikali iboresha huduma hizi kwingine kama Kigamboni n.k.

Lingine ni pesa zisio za halali ziliingia kwa kasi miaka iliyopita na watu walikuwa wanashindana kununua majumba na viwanja kwa dau kubwa. Na waliouziwa kwa bei hizi mbaya sasa wanataka kuuza ili wapate faida na madalali nao wakiingia kwenye soko ndio hapo sasa tunaona bei za ajabu.
 
Tatizo ni kuwa sehemu zenye vitu muhimu kama maji, umeme, barabara na usalama ni chache sana hivyo kila mtu anataka kuishi huko. Inabidi serikali iboresha huduma hizi kwingine kama Kigamboni n.k.

Lingine ni pesa zisio za halali ziliingia kwa kasi miaka iliyopita na watu walikuwa wanashindana kununua majumba na viwanja kwa dau kubwa. Na waliouziwa kwa bei hizi mbaya sasa wanataka kuuza ili wapate faida na madalali nao wakiingia kwenye soko ndio hapo sasa tunaona bei za ajabu.
 
Watanzania wana hela si mchezo. Unalalama eti bei kubwa kesho nyumba huioni. Ila sasa hivi watu wanaitwa madalali ndiyo wenye nyumba maana unakuta mwenye nyumba anataka sh. 200,000 dalalai anasema 300,000.
 
Back
Top Bottom