Bongo ni Zaid ya burdaan, Kila mtu anajifanya alikuwa karibu na eneo la Tukio, naskia askari wa kitasha walikuwa wanawahi Maiti za kizungu na kuacha majeruhi weusi!
Watu wangapi walikuwepo kwenye tukio unaowajua wewe na humu ni watu wangapi tumedai kuwepo kwenye tukio? Hebu fanya ulinganifu kidogo........kama thread haikupendezei kaa kimya au post "napita tu" kama ilivyo mila yetu hapa JF
Siku hiyo nilikuwa Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam, nikielekea kazini. Yaani kishindo cha mlipuko kilikuwa ni balaa. Sikujua nini kimetokea mpaka nilipofika kazini ndipo nilipofahamu kuwa Osama ametutumia salamu.
by then hakukuwa na jf, fb wala blogs nadhani. Hata waliokuwa na email addresses wanahesabika na ilichukua masaa kadhaa kwa waliokuwa upcountry kujua kabla DW na BBC hawajasimulia
Siku hiyo nilikua hapo mitaa ya kinondoni vijana,ule mshindo nilidhani roli limepasuka tairi hapo nyuma yangu.baadae naona moshi unapanda juu kisha vibaka kibao wakawa wanatoka mbio kuelekea eneo la tukio